Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Nhee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mna kelele mno. Mara mlalamike mara mjitape kuonyesha hamguswi na tcra. Tulieni mshuhudie mchezo. Wazima wasizime ni juu yao kuamua.

Fateni sheria,msipigane na teknolojia
 
...Na wale ambao walituma fomu na picha na wakaambiwa na NIDA Wajiandikishe upya na bado hawajafanya hivyo, wakizimiwa simu zao kosa linakuwa la nani hapo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mbona wanachelewa kuzima tu, wazime aisee, nasema wazimee!
 
Hapana utulivu wake ulimfanya asisikiwe na wale mabinti watatu.. na binti aliyefuata alisema anatamani aolewe na muoka mikate wa mfalme
Hii tabia yako ya kifala sana, kila thread unaandika huu utumbo wako. Hapa hamna watoto wenzako
 
Nawajua watanzania wengi wenye akili timamu waliohangaika kupata vitambulisho miaka kadhaa iliyopita lakini hawakuwahi hata kupata namba. Kwa wale waliofanikiwa mapema ni sawa kuwatukana hawa, kwani mnaweza kudhani mchakato ulikuwa mwepesi mno kwa wote. Hiyo ndio hulka ya watanzania.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Binadamu bwana ilipofika muda wa kuhamia digital system kutoka analogue system malumbano yalikuwa makali lkn ikapita na maisha yanaendelea ikaja issue ya visimbuzi wakapiga kelele weee lkn mwisho wake unajulikana na maisha yakaendelea,Kila zama zina mambo yake na yanapita tunasonga mbele watu wameumbwa na midomo waache waseme mwisho wata lala.

Leo wanaponda ndege nk jana waliponda hata uwanja wa taifa kujengwa walipinga kujengwa daraja la mkapa hao ndiyo binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa hawewezi kutoa bure waseme tuvilipie, ila huu utaratibu sijaupenda, hivi vilitakiwa visiwe na expire date
 
Namba yako haijahakikiwa kwa alama za vidole, tafadhali tembelea ofisi ya NIDA ili upate kitambulisho. Tembelea ofisi/duka au wakala wa Halotel aliye karibu yako ili kuhakiki taarifa zako. Asante
Naona ujumbe wao wa vitisho umesitishwa. Kumbuka hizi kampuni zipo kibiashara zaidi. Ngoja tuone kama watazima. Zimebaki dk chache ifike tarehe 21
 
Baada ya kujaribu kusajili saa mbili asubuhi na kukwama na kupata nafasi tena saa kumi na mbili had I saa tatu,nimekwama line ya Voda,Airtel sijapata uthibitisho nikipiga *106# hakuna usajili wa biometric.. Wadau mtanisahau kidogo kama watazima..Pole in advance kwa wahanga wenzangu.Huenda miamala kesho itapungua,pengine network zitakuwa na kasi kwenye data kwa kuwaza watumiaji watakuwa wachache.
 
Ukisikia TBC, BBC au KTN alafu ukapita kwenye vibanda au miamvuli yenye mawakala wanaosajili unaweza kugundua tupo wapi.

Kupitia media tajwa hapo juu nimegundua hili swala limechukuliwa kama mwisho wa dunia, maana nilipopita eneo moja nimekuta Watanzania wamekaa tu, sababu wanasema network inasumbua hivyo wanasubili.

Baada ya kufuatilia sana nikagundua siyo network bali ni watendaji wa NIDA wanashindwa kumudu wingi wa taarifa zinazotumwa kwao kutoka kwa mawakala nchi nzima kiasi kushindwa ku_conferm kwa wakati na kurudisha majibu.

Muda huu bado Wananchi wanaangaika kwa Mawakala ili line zisizimwe.
Kuondoa hofu line hazizimwi.
 
Duh mbona mimi hata sina hofu na hii issue
 
Ulisajiandikisha lini mkubwa maana hapa kuna watu walijiandikisha kabla ya krismas lakini hawajui nini kinaendelea
Nimejiandikisha mwezi wa nane mwaka jana nimeenda nida zaidi ya mara kumi bila mafanikio nikapewa namba ile kutafuta kwenye simu nikuwa natuma sms mpa usiku wa manane,, Leo mchana wamenitumia wenyewe namba ya kitambulisho changu,,, nida kiboko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wanao chukua data kwa ajili ya kuandaa kitambulisho, walitakiwa wawe wanapewa namba kabisa, wakisha jaza data za mteja kwenye fomu, wakidhibitisha amejaza kwa usahihi, tayari kwa kumtengenezea kitambulisho palepale anapewa no yake, ambayo pia inajazwa moja kwa moja kwenye fomu.

Nida wangewapa kabisa no hawa mawakala wao, tatizo lisingekuwepo kabisa, ila sasa wanawagarimu watanzania wengi, kwa kuto tu waza mbali.

Huku vijijini hali ni mbaya zaidi kuliko mijini, twende hivi hivi, ila kuna siku tutafika, leo mtu akikosa mawasiliano, ni umemkosesha maendeleo, ni sawa na mtu alikua anatumia umeme, alafu umeme uondolewe, akiwa anaishi nyumba ileile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wenzangu tutakuwa salama maana tumekataa mambo ya MARK OF THE BEAST! Hutapiga simu wala kupigiwa simu.
LIST OF MARK OF BEAST
LUKU
SIM CARD
LICENCE
PASSPORT
Mungu hakutuwekea mipaka ya hivi..huyu shetani anatawala dunia..
Hahahah jana niliota hivyo baada ya kuwaza sana usajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…