Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuna hoja ambayo haijaulizwa na hivyo kutotolewa ufafanuzi. Hao 975041 wana namba za NIDA tayari. Hao ni sawasawa wafungiwe maana hawana sababu, ni wakaidi; lakini kuna wale ambao hawajapewa namba za NIDA - walianza mchakato tangu mapema mwaka jana, wakapigwa picha nk. lakini hadi leo wanaendelea kufuatilia namba hizo bila mafanikio - nini hatima yao?
 
laini zenyewe hazisajiliki tangu alhamis seva zimezidiwa

ngoja nijaze vocha
 
Kama mmeshindwa jambo hili ni nini mnachoweza?

Sijasajili line zangu kwa MAKUSUDI na ingetokea mkanifungia jana usiku leo ningeenda kusajili ila mmeshindwa.
Wacha nirelaksi maana hakuna mnachofanya na kampeni zimekaribia

Hamtathubutu kuzima simu na hatudanganyiki

MATAGA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hukumsikia waziri Nditiye alisema hekima itatumika halafu kumbe zikizimwa zote kwa wakati mmoja zinaweza pelekea servers za NIDA kuelemewa na mzigo kwa sababu ya wingi wa watu watakaojitokeza kujiandikisha
 
Nilikuwa sina mpango wa kusajili line yangu ya simu ingawa sina sababu ya msingi kabisa NIDA ninayo ile ya mwanzo kabisa ya yule aliyeshitakiwa basi tuu sikuwa nataka usumbufu ila nadhani sasa naweza sajili
Unaadika kama kwamba ulikuwa unafanya jambo la maana sana!. Watu kama nyie mlitakiwa mfumgiwe line na mpewe adhabu ya nyongeza
 
NIDA na RITA wangeunganishwa "Data synchronization" ingekuwa jambo la busara sana..... kwa sasa taasisi hizi mbili za serikali ni sawa na lila na fila (hazitangamani)
 
Sijui kama wasingeamua kutumia busara waliyoitumia kutokuzima line zote ambazo hazijasajiliwa nini kingetokea mpaka sasa

Najiuliza servers za NIDA na mitandao ya simu sijui zingeweza vipi kuwahudumia watu milioni 20 kwa wakati mmoja

Najiuliza sijui wafanyakazi wa NIDA wangewezaje kuwahudumia watu milion 20 kwa wakati mmoja

Ni wazi nchi ingesimama na kuna baadhi ya watu wangetangulizwa mbele za haki na wananchi walio na hasira

Mpaka sasa najiuliza hii busara ya TCRA kuacha kuwaonea watanzania kwa makosa ambayo sio yao wameitoa wapi

Mpaka sasa Jiwe yuko kimya hajatoa tamko lolote sijui akitoka huko ataropoka nini maana ni kawaida yake kutokujali maumivu ya watu licha ya kutoka kabila linalosifika kwa ukarimu sana pengine kuliko makabila yote Tanzania
 
Mikwara tu hiyo tar 20/01/2020. tunaendelea na mawasiliano bila namba za Nida wala kitambulisho. Binafsi nitaenda NIDA watakavyorekebisha usumbufu wao.

Wewe jamaa kama mimi, yani katika kitu sijawahi kuwaza ni kwenda kwenye foleni ya NIDA, mimi nitaenda mara tu watakapo ondoa usumbufu, MTU hapaswi kusibiri kitambulisho miezi 4
 
KISIWAGA,
Yani system ya NIDA ni ya kutunza data, kuadd, kuedit labda kudelete, ila no load balances wala nini... yani issue ikibuma NIDA lazima usubiri TRA, na wengine wote wanaoitegemea
 
mkuu akili za viongozi wa serikali yetu ndio zile zile za wananchi maana kumbuka wanatoka miongoni mwa wananchi

ndio maana waafrika walitakiwa waendelee kutawaliwa na wazungu ambao sio miongoni mwetu
 
Back
Top Bottom