Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

1. Mtaani wanapita vijana wamachinga na maspika yao, wanatangaza "tunasajili laini kwa alama za vidole". Wanachomoa vimtambo vyao, wanakuomba kitambulisho wanakusajili. Ni nani anaweza kupreserve integrity ya zoezi?

Hivi watu wenye ajenda zao wakiwapa hawa vijana pesa na wakisajili kwa fingerprints za watu wengine zoezi hili umakini wake utakuwaje?

2. Mtandao mmoja mtu anaweza kuwa na laini hadi 5

Je mtu mmoja mwenye kitambulisho akisajili laini kadhaa na kugawa nyingine kwa ndugu, jamaa na marafiki itakuwaje?

3. Huko vijijini ndani ndani kabisa hao wanaosajili kwa alama za vidole capacity yao ya kufika huko ndanindani ikoje?

MY TAKE:
Hii nchi ni nchi ya watu masikini sana, kinachosikitisha ni kwamba pale kunapoanza kutokea mwangaza fulani hivi wa sekta fulani kuanza kuchomoza na kushine ili baadae iwe nguzo muhimu ya kiuchumi na kijamii, huwa zinatokea forces fulani kutoka kwa serikali ileile kuanza kuweka regulation ngumungumu zinazorudisha mafanikio ya wananchi nyuma. Kwa mfano:

a) Wananchi walikuwa wameshapiga hatua kubwa kweli kwenye kumiliki TV, kiufupi nyumba za wananchi wengi vijijini na mijini walishaanza kuona TV kama sehemu ya utamaduni wao. Cha ajabu serikali ikaja na mambo ya kuhama Kutoka Analojia kuja Dijitali, na kusababisha kuleta watu wa ving'amuzi kitu kilichopekekea gharama za kumiliki TV kuwa juu, na matokeo yake nyumba nyingi nchini leo hii TV ni anasa!. Watu leo hii imefikia hafua kuangalia Taarifa za habari Bar, au kuangalia mpira wa ligi yao wenyewe kwenye mabanda ya mpira!
Kiufupi base ya wananchi wamiliki TV, imeshrink mno

b) Leo tena baada ya mafanikio ya wananchi mamilioni kwa mamilioni kumiliki laini za simu, serikali ile ile yenye kawaida ya kuvuruga baada ya mambo kuanza kuonekana kukaa kwenye msitari inakuja na reguation juu ya regulation, leo inataka watu wajisajili kwa vitambulisho vya NIDA plus fingerprints, wakati inajua ipasavyo kuwa capacity ya kuprovide vitambulisho hivyo kwa kasi ni ndogo lakini pia uwezo wa kusajili hizo alama za vidole kwa kasi ya kutosha hadi kucover huko vijijini ni mdogo!
Matokeo ya hili zoezi la usajili wa laini ni ama watu wengi watacheat kwa kutokuwa na usajili sahihi au kupelekea upunguaji wa umiliki wa laini za simu, matokeo yake wamiliki simu watapungua kama ilivyotokea kwenye zoezi la TV
 
Kisaikolojia fanya haya. Kama una smartphone utaendelea na internet kwa wi fi ya mtu mwingine karib. Utaacha aina zote za mikopo ya mitandaon. Utafanya mawasiliano ya kupiga kwa internet tu bila line kwenye whasapp, viber etc. Utarudia mifumo ya kibenk kuhusu pesa hasa huduma ya cardless. Mwisho wa yote utaambulia usumbuf kias lakin kampun zitapoteza makato meng yanayokuhusu na serkali itapoteza mapato ya kodi.
...Asante kwa Kujitahidi Kuniandaa Kisaikolojia, Mkuu Rwazi1...[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania tuna tatizo la kutokuwa na sera za taifa. huduma, elimu, uchumi afya na usalama zinatakiwa kuwa sera za taifa hata aje kichaa gani angebanwa na katiba na sheria lakini aya mambo ya kufata matakwa ya mtu mmoja ndio yanatughalimu kama nchi.

Unamwambia babu wa miaka 70 akajipange foleni nida kujaza form ya kusajili line seriously? mzee atoke kijijini kwenda wilayani kutafuta namba? unakuta mtu anatembea km 50 kwa baiskeli au kwa miguu nenda rudi nenda rudi bila mafanikio. huduma ni haki ya kila mtu kuwafungia watu line kwanza ni uvunjifu wa katiba.
 
Mimi nahisi ndio mtanzania pekee ambaye line yangu inaenda fungiwa kwa uzembe wa NIDA

Mwaka mmoja na nusu nimejiandikisha lakini hizo namba zao hazifanyi kazi

Yani bora ingekuwa taarifa hazionekani ili nijue naanza upya

Majibu waliyoniambia ni mpaka kitambulisho changu wakiprint alafu nilipe 20000 ndio waweze kurekebisha

Mwaka mmoja na nusu sasa bado hawajakiprint.

Dah! 😭😭😭😭 so sad sana kuna mambo muhimu zaidi ya namba ya simu nashindwa kukamilisha 😭😭😭
 
Na makampuni ya simu wanasema tatizo ni System za Nida teh teh ili ni picha la kutisha
Wale wenzagu na mimi magwiji na makonki wa kufanya tukio siku ya deadline!
Tunasikitika sana tangu jana jion na leo jumamosi, na kesho jumapili mtandao wa kusajili simkad kwa alama ya vidole hautapatikana!

Ni rai yangu tutaongezewa mda simu zetu hazitazimwa.
Imetolewa na mwenyekiti wa!

WASUBIRI DEADLINE!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Mtaani wanapita vijana wamachinga na maspika yao, wanatangaza "tunasajili laini kwa alama za vidole".
Wanachomoa vimtambo vyao, wanakuomba kitambulisho wanakusajili. Ni nani anaweza kupreserve integrity ya zoezi?. hivi watu wenye ajenda zao wakiwapa hawa vijana pesa na wakisajili kwa fingerprints za watu wengine zoezi hili umakini wake utakuwaje?

2. Mtandao mmoja mtu anaweza kuwa na laini hadi 5, Je mtu mmoja mwenye kitambulisho akisajili laini kadhaa na kugawa nyingine kwa ndugu, jamaa na marafiki itakuwaje?

3. Huko vijijini interior kabisa hao wanaosajili kwa alama za vidole capacity yao ya kufika huko ndanindani ikoje?

MY TAKE:

Hii nchi ni nchi ya watu masikini sana, kinachosikitisha ni kwamba pale kunapoanza kutokea mwangaza fulani hivi wa sekta fulani kuanza kuchomoza na kushine ili baadae iwe nguzo muhimu ya kiuchumi na kijamii, huwa zinatokea forces fulani kutoka kwa serikali ileile kuanza kuweka regulation ngumungumu zinazorudisha mafanikio ya wananchi nyuma. Kwa mfano:

a) Wananchi walikuwa wameshapiga hatua kubwa kweli kwenye kumiliki TV, kiufupi nyumba za wananchi wengi vijijini na mijini walishaanza kuona TV kama sehemu ya utamaduni wao. Cha ajabu serikali ikaja na mambo ya kuhama Kutoka Analojia kuja Dijitali, na kusababisha kuleta watu wa ving'amuzi kitu kilichopekekea gharama za kumiliki TV kuwa juu, na matokeo yake nyumba nyingi nchini leo hii TV ni anasa!. Watu leo hii imefikia hafua kuangalia Taarifa za habari Bar, au kuangalia mpira wa ligi yao wenyewe kwenye mabanda ya mpira!
Kiufupi base ya wananchi wamiliki TV, imeshrink mno

b) Leo tena baada ya mafanikio ya wananchi mamilioni kwa mamilioni kumiliki laini za simu, serikali ile ile yenye kawaida ya kuvuruga baada ya mambo kuanza kuonekana kukaa kwenye msitari inakuja na reguation juu ya regulation, leo inataka watu wajisajili kwa vitambulisho vya NIDA plus fingerprints, wakati inajua ipasavyo kuwa capacity ya kuprovide vitambulisho hivyo kwa kasi ni ndogo lakini pia uwezo wa kusajili hizo alama za vidole kwa kasi ya kutosha hadi kucover huko vijijini ni mdogo!
Matokeo ya hili zoezi la usajili wa laini ni ama watu wengi watacheat kwa kutokuwa na usajili sahihi au kupelekea upunguaji wa umiliki wa laini za simu, matokeo yake wamiliki simu watapungua kama ilivyotokea kwenye zoezi la TV
Hayo mambo ya digital vs Analogy Tvs umenikumbusha mbali sana nakumbuka mawaziri wa awamu ile ya JK walitetea sana, inaonekana hata wao walikuwa hawajui namna mfumo wa digiti utakavyofanya kazi.
Katika suala la Fingerprints zinazosajiriwa mitaani hilo ni bomu linalokuja, nakumbuka wakati tunaanza kusajiri laini miaka 2009 hivi, Mimi laini yangu ya Airtel nilisajiria pale Kijitonyama cha kushangaza miaka michache baadaye nikapigiwa simu na hao wenye mtandao nikiambiwa Majina yaliyosajiriwa katika laini yangu nikatajiwa nikakuta siyo yangu wakasema yameingiliana, nilichokuja kugundua ni usajiri wa mtaani unamatatizo, kwani kuna wakala wa usajiri na yule wa makao makuu ya mtandao walibadilisha majina
 
Amani iwe nanyi wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu.

TCRA ngoja tu niwaambie ukweli kutoka moyoni, Nasubiri kwa hamu sana mfunge laini yangu nipotee hewani kwa muda wa kama mwaka hivi maana nimechoka sana kupigwa na wajanja wa mitandao wa haya makampuni ya simu.

Kila siku kila siku nimechoka bhana nyie fungune mtupunguzie na shida tutengeneze na vibubu vya kutunza pesa siyo kila siku kuyachangia makampuni.

Sababu ya pili, Mkifunga nitafurahi sana maana nimechoka kupigiwa pigiwa simu na wana ambao hawana hata michongo yeyote.

Yaani ukipigiwa simu story zao ni oya Mayala vipi uko maskani nataka nikupitie twende Igoma yaani hawana jipya.

Fungeni tu bhana tumechoka.

LONDON BOY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu tunavyoandika humu watu wamatuona wazeeeembe kutokuwa na no za nida, hawajui wengine tumejiandikisha tangu 2012 nimekikanyagia hadi wilaya ikagawanywa lakini waaapi.
Haya wakatoa no za kuangalia no zako za Id kwenye simu nao ndio nikachoka kabisa ati wanasema taarifa zangu hazijakamilika.
Nimehama mkoa nikaenda tena nida mwaka jana mwezi wa 9 na ile risiti ya 2012 ati wananiambia nirudi tena Dar aseee.!!? Fungeni mamayo nyie.
 
Kuna tatizo ukifanya hivyo? Muhimu si kusajili tu?
Huwezi elewa we subiria hiyo tar20 watufungie cheap zetu ndio utaelewa humu jf kwenyewe wengi tutashindwa kuingia achilia mbali maswala ya kupiga simu kijijini tutarudi enzi za kusikiliza taarifa ya habari kwa m/kiti wa kijiji.

Je baada ya kuzuia mikutano ya siasa hawa watu wana hofu ya wananchi kumiliki simu?
Kwamba kampeni zikianza mamilioni ya wananchi watafikiwa kirahisi kupitia hizi simu kwa hiyo inabidi baadhi ya watu haswa wa huko vijijini inabidi wawekwe offline lkwa muda?
 
Back
Top Bottom