1.Mtaani wanapita vijana wamachinga na maspika yao, wanatangaza "tunasajili laini kwa alama za vidole".
Wanachomoa vimtambo vyao, wanakuomba kitambulisho wanakusajili. Ni nani anaweza kupreserve integrity ya zoezi?. hivi watu wenye ajenda zao wakiwapa hawa vijana pesa na wakisajili kwa fingerprints za watu wengine zoezi hili umakini wake utakuwaje?
2. Mtandao mmoja mtu anaweza kuwa na laini hadi 5, Je mtu mmoja mwenye kitambulisho akisajili laini kadhaa na kugawa nyingine kwa ndugu, jamaa na marafiki itakuwaje?
3. Huko vijijini interior kabisa hao wanaosajili kwa alama za vidole capacity yao ya kufika huko ndanindani ikoje?
MY TAKE:
Hii nchi ni nchi ya watu masikini sana, kinachosikitisha ni kwamba pale kunapoanza kutokea mwangaza fulani hivi wa sekta fulani kuanza kuchomoza na kushine ili baadae iwe nguzo muhimu ya kiuchumi na kijamii, huwa zinatokea forces fulani kutoka kwa serikali ileile kuanza kuweka regulation ngumungumu zinazorudisha mafanikio ya wananchi nyuma. Kwa mfano:
a) Wananchi walikuwa wameshapiga hatua kubwa kweli kwenye kumiliki TV, kiufupi nyumba za wananchi wengi vijijini na mijini walishaanza kuona TV kama sehemu ya utamaduni wao. Cha ajabu serikali ikaja na mambo ya kuhama Kutoka Analojia kuja Dijitali, na kusababisha kuleta watu wa ving'amuzi kitu kilichopekekea gharama za kumiliki TV kuwa juu, na matokeo yake nyumba nyingi nchini leo hii TV ni anasa!. Watu leo hii imefikia hafua kuangalia Taarifa za habari Bar, au kuangalia mpira wa ligi yao wenyewe kwenye mabanda ya mpira!
Kiufupi base ya wananchi wamiliki TV, imeshrink mno
b) Leo tena baada ya mafanikio ya wananchi mamilioni kwa mamilioni kumiliki laini za simu, serikali ile ile yenye kawaida ya kuvuruga baada ya mambo kuanza kuonekana kukaa kwenye msitari inakuja na reguation juu ya regulation, leo inataka watu wajisajili kwa vitambulisho vya NIDA plus fingerprints, wakati inajua ipasavyo kuwa capacity ya kuprovide vitambulisho hivyo kwa kasi ni ndogo lakini pia uwezo wa kusajili hizo alama za vidole kwa kasi ya kutosha hadi kucover huko vijijini ni mdogo!
Matokeo ya hili zoezi la usajili wa laini ni ama watu wengi watacheat kwa kutokuwa na usajili sahihi au kupelekea upunguaji wa umiliki wa laini za simu, matokeo yake wamiliki simu watapungua kama ilivyotokea kwenye zoezi la TV