Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Matatizo ya ufahamu mdogo ndio hayo siku zote hawaendi, wakienda milioni kwa mpigo Nida watafanya kazi vp? .Mwingine juzi anasema nijisajili ya nn? Wakati najijua mtanzania na línea kila siku nanunua nyingine😂
 
Ni hakika wengi hawajaweza kusajili simu zao na sababu ni NIDA kushindwa na pia tabia ya wananchi kusubiri deadlines.

Nashauri laini hizi zisizimwe bali tozo ya shilingi 1000 iwekwe kwa kila siku itakapochelewa kusajiliwa. Pesa hizo ziende moja kwa moja Serikalini. Pia zoezi la usajili liwe endelevu.

Usiseme faini, sema zitozwe kodi. Kwa wanavyopenda kutoza kodi, utadhani wao kodi wanalipa.

Kumbuka issue si simu issue ni kodi kwa Kila mtu (wazo Zuri tu). Hili litafanikishwa na nida ndiyo maana Kila kitu nida. Passports nida, driving license - nida, bank accounts - nida.

Atakamuliwa ng'ombe hadi damu.
 
Saa hizi saa moja na dakika 19 usiku, hii ni foleni ya nje ya makao makuu ya tigo, watu akisubiri usajili line kwa salama ya vidole (kumbuka line hizi zilishasajiliwa kwa vitambulisho vingine)

Ndani kumejaa hawa ni walio nje.

Network ya NIDA haifanyi kazi, lakini watanzania hawa wameamua watasubiri tu hadi itakaporudi wasajili.

Binafsi sijaona usumbufu huu watanzania wanapewa kwa sababu gani,,,,,,,, wakati mwingine hata uzuri wooooote wanaojitahidi kuufanya, ukifika kwenye hivi vitu vidogo vinavyomgusa mtanzania vikiharibika, hiyo SGR, Flyover hazina maana.

Maana watanzania hawa ambao simu sasa ni maisha yao, unapotaka kuwafungia leo, watauona umuhimu wa SGR au Mombadia kweli? Maana kinachomoa kula sio SGR Bali simu yake ambayo sasa umeiingilia kwa makosa ya mfumo wako mbovu. Binafsi nimepata namba ya NIDA jumamosi saa moja usiku Juzi, toka jana nimeenda kusajiri kila sehemu mtandao wa Nida haufanyi kazi. Line yangu kwa kweli wazime tu, watawasha watakapojisikia. Tutaonana mbele ya safari, hakuna marefu yasio na ncha.....
20200120_191826.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu watasajili tu na utashangaa kila mtu soon atakuwa na laini iliyosajiliwa. Hata mfumo wa analojia watu walipinga sana kuwa watu hawana uwezo wa kununua vingamuzi mara sijui nini lkn mfumo ulizimwa na hadi leo maisha yanaendelea. Mabadiliko ni threats kwa watu wengi lkn baada ya muda mchache wanazoea na maisha yataendelea kama kawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaelewa point... unazima simu ya mtu kwa kosa la NIDA..??
 
Ni hakika wengi hawajaweza kusajili simu zao na sababu ni NIDA kushindwa na pia tabia ya wananchi kusubiri deadlines.

Nashauri laini hizi zisizimwe bali tozo ya shilingi 1000 iwekwe kwa kila siku itakapochelewa kusajiliwa. Pesa hizo ziende moja kwa moja Serikalini. Pia zoezi la usajili liwe endelevu.
Usitumie kalio kuwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikubaliani na wazo lako. Zizimwe tu, kuwe na "control" ya uhakika ya watumiaji.

Na ndipo NIDA watafanya bidii kwa kila anaestahiki kitambulisho apatiwe haraka sana.
Nakuunga mkono. Zizimwe, anayehitaji sana simu kwa sababu ya maana atafuata utaratibu akaifufue.
Simu hizi zinatugharimu sana, na kinachosababisha tuwe nazo ni urahisi wa kuzipata. Bora zizimwe, ukiritimba huu utasaidia kupunguza watumiaji wa simu, wanunuzi wa data za kuangalizia shilawadu na vitu kama hivyo.
Simu moja kwa wastani inatumia si chini ya sh 10,000 kwa mwezi kwenye anasa isiyokuwa muhimu. Imagine kwa simu zaidi ya milioni 10 ambazo hazijasajiliwa ni pesa ngapi zitaokolewa? Zizimwe tu.
 
Usalama wa Watanzania ni zaidi ya tarakimu. Zizimwe tu.
 
Naomba kujua, ni faida zipi zitakazopatikana kwa kufungia laini za watanzania milioni ishirini kwa sababu zisizo na mashiko?

Kuna watu wanaishi kwa miamala ya simu.

Kuna watu wanaishi kwa kutumia internet.

Miamala ya benki na biashara yote inahitaji simu!

Kadi za NIDA hakuna. Na simu zinazimwa!

Vitambulisho vya kura na leseni hawataki. Wanataka NIDA. Bila NIDA hakuna kusajili.

Hakuna guarantee kwamba NIDA watatoa namba upesi baada ya laini kufungwa.

Kwahiyo watu wataishi bila mawasiliano kwa muda usiojulikana mpaka pale NIDA watakapojisikia kutoa kadi na namba!

Haya yote yanafanywa kwa ajili ya nani? Kuna motive gani nyuma ya huu uovu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Zinazimwa kuokoa pesa zinazopotea kununulia mabando ya kuangalizia shilawadu kwenye youtube na mawasap. Pesa nyingi sana inapotelea kwenye ujinga. Zima zote tuokoe gharama.
 
Vitambulisho vya nida vimeanza kutolewa miaka mingi tu
Mm changu nilipata bila usumbugu mwaka juzi watanzania ni watu wa kupuuza jambo mno
Ndio mana tunawakejeli zaidi wanaohangaika sasa hivi
Waliambiwa wakabeza sana wacha mpambane na hali zenu .anyway ukiwaonea huruma ww inatosha na je nikiwaonea huruma ndio nitawasaidia nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom