The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
View: https://www.youtube.com/live/ZcC1DjuaCGA?si=v690LB1yPXEmkK6v
=======
Kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi CCM, katika kata ya bunju halmashauri ya manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Makalla amefungua sherehe za kuadhimisha miaka 48 ya chama hicho huku akisema CCM ndiyo Chama pekee Checye dhamana na wajibu wa kuwatumikia watanzania.
"CCM ndiyo Chama pekee Checye dhamana na wajibu wa kuwatumikia watanzania hao wengine hawana wajibu wala dhamana yoyote, CCM ndiyo inayoshughulika na Changamoto za Wananchi ndiyo inashughulika kuwaletea wananchi maendeleo”
Aidha amesema kwa upande wa Zanzibar amesema hawatoi kiti waka kabati kwa udiwani uwakilishi na ubunge na Urais
"Ndugu zetu kule Zanzibar wanawapa salamu, hawatoi kiti waka kabati kwa udiwani uwakilishi na ubunge na Urais kule Zanzibar" alisema Makalla
Akitoa shukrani kwa watanzania wote na wananchi waliopo mkoa wa Dar es salaam, dhidi ya ushindi wa asilimia 98 walioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, Makalla amesema hiyo ni salamu kuwa ushindi huo unaakisi kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2025.
"Miaka 48 ni mingi toka vyama vyetu TANU NA ASP vilipounganishwa na kuzaliwa chama cha mapinduzi, wakati tunasherehekea miaka 48 nianze kwa kuwashukuru watanzania wote na wana Dar es salaam kwa kukipa ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, .. uchaguzi mimi nimeshiriki Dar es salaam katika wilaya zote katika majimbo yote nilifurahishwa na wana Dar es salaam muliokataa propaganda, uongo, mkachagua chama cha mapinduzi, na hii ni salamu kama tumeshinda serikali za mitaa kwa asilimia 98 nategemea kabisa ushindi ni huohuo katika uchaguzi mkuu Oktoba utakapofika" alisema.