Kuelekea Maandamano ya Maombolezo Septemba 23: Je, Mamlaka Zimejiandaa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kuna kila dalili kwamba maandamano yatafanyika, lakini ni kwa ukubwa gani ni ngumu kutabiri. Kwa wiki nzima hii, kamata kamata imekuwa kubwa sana, hadi vibaka na wezi wameamua kuchukua likizo ya muda.

Tumeshuhudia pia maandalizi makubwa ya polisi wa kutuliza ghasia, polisi wa sare, na wanashughuli wa usalama wakiwa kwenye magari na kila aina ya kifaa na nyenzo za kupambana na yeyote yule.

Hata hivyo, kuna maandalizi mengine ambayo sijui kama yamefanyika.

1. Njia za Kidiplomasia.
2. Magari ya Wagonjwa
3. Vifaa Tiba vya Dharura
4. Wahudumu wa Afya wa Dharura
5. Hospitali za Dharura
6. Mahabusu

Kuwa maandamano ni haki ya kikatiba kwa sheria zetu na za kimataifa. Ni vyema na hayo maandalizi mengine yakapewa kipaumbele pia!


View: https://x.com/LuhagaMpina/status/1837763737027019154?t=jsxIa8hgQXbeOlTYGmfpcA&s=19
 
Hii nguvu kubwa inayotumika kuzima sauti za wananchi ingetumika kuzuia mauaji yanayotokea kila kukicha ingekuwa jambo la msingi sana.

Serikali inatumia resources nyingi kufanya mambo ya kijinga kama haya ya kuzuia maandamano ya amani
 

Ruto: Kwenye demokrasia, Maandamano ni jambo la kawaida
 
 

Attachments

  • 20240922_113907.jpg
    76.9 KB · Views: 2
  • 20240922_113914.jpg
    78.9 KB · Views: 2
  • 20240922_113923.jpg
    78.9 KB · Views: 2
Hii nguvu kubwa inayotumika kuzima sauti za wananchi ingetumika kuzuia mauaji yanayotokea kila kukicha ingekuwa jambo la msingi sana.

Serikali inatumia resources nyingi kufanya mambo ya kijinga kama haya ya kuzuia maandamano ya amani
Mimi inaniuma sana wanapomaliza mafuta ya walipa Kodi Kila siku na ruti zao zisizo za msingi kwenye ile mikweche yao wanaita defender.

Hii wiki magari ni mengi sana barabarani yanazurura Huku yamewajaza hao wahuni huko nyuma wakiwa na mitutu.

Uhuni mtupu wanaufanya.
 
Mimi naona kama Mama kashauriwa azuie haya maandamano, watu hao hawamtakii mema. Watu acha watoe hasira zao, kwa kuongea, kuimba. Wataandamana kwa kutembea na miguu yao, watakapoanzia na kumaliza.

Hakuna hapo uvunjifu wa amani wowote, hawagusi mtu, hawavunji hata kijiti. Polisiccm ndiyo mtaanza kuleta uvunjifu wa amani. Ilitakiwa viongozi mjitafakari, kama kungekuwa hakuna tatizo, hakuna wa kutaka kuandamana. Wakati mwingine si kutumia nguvu, bali akili tu.
 
Maandamano ni lini wakuu? Yanaanzia wapi hadi wapi? Saa ngapi tukutane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…