Ulimakafu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 31,248
- 13,244
Kigezo gani kimetumika kumteua Matola kuwa kocha msaidizi?Hatuna mipango, tumekalia ulaji.
Hivi ni kigezo gani kimetumika kumteua Milambo kuwa mkurugenzi wa ufundi, kigezo gani kimetumika kumchagua julio kocha wa vijana, kigezo gani kimetumika kumchagua Kidau kuwa katibu mkuu TFF.
Nafasi zote ni za kutangazwa na watu kuomba lakini kwa sababu ya ushikaji wamekaa wanapeana nafasi na hizo ndio nafasi nyeti kwa maendeleo ya soka.
Kama tutatengana na Zanzibar baada ya miaka mitatu hatutawafikia kisoka.