Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Habari Tanzania na Kote Duniani..!
Kuelekea siku ya Jumapili February 13, 2022 hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC kupigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa (Mkapa Stadium), ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC anakamuana na ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast.
Ni mchezo mkubwa kwa timu kubwa zitakapombana kutafuta matokeo chanya kwenye michuano hii ya pili kwa ukubwa baada ya CAFCL.
Neno kutoka kwa M/kiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema kuwa
"Hii ni hatua kubwa na vile vile ni utamaduni wa kawaida wa Klabu ya Simba, kuweza kushiriki katika mashindano haya, kama tunakumbuka tangu historia ya mpira wenyewe katika miaka ya 70, 80, na 90 Simba SC imekuwa ikifanya vizuri na kwa kipindi cha miaka minne mitano tumekuwa na mfululizo wa kushiriki mashindano ya Kimataifa na kufikia ngazi ya makundi na ngazi ya robo fainali, na tunaamini kwa Kikosi tulichokuwa nacho mipango ya bechi la ufundi na management tutahakikisha timu yetu inafanya vizuri na kufikia hatua ya juu zaidi".
Naaam Wanasimba na mdau wa Kabumbu, maandalizi yote yanaendelea hivyo nasi ni jukumu letu kujiandaa kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi na kushangilia mwazo mwisho huku tukishuhudia kandanda safi liliothibitishwa na CAF kutoka kwa Mkali wa Soka Nchini, Simba SC.
Karibu kwa yakayojiri kabla ya mchezo wenyewe..Usikose Ukaadithiwa.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
============
Update;
Naibu Spika Mh. Mussa Azzan Zungu, atakuwa mgeni Rasmi kwenye mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
=========
Kocha wa Simba SC Pablo Franco amesifu uwezo wa wapinzani wao ASEC Mimosas huku akisema timu hiyo ipo vizuri kwenye mipira ya kutengwa.
Naye Kocha wa ASEC Mimosas Julien Chevalier amekimwagia sifa uwezo wa Simba SC huku akitanabaisha kuwa timu hiyo inapenda mashindano makubwa.