Kuelekea mechi ya CAFCL, Kocha: Tunaanza kesho kupambana tunajua Nchi na Simba nini wanataka

Kuelekea mechi ya CAFCL, Kocha: Tunaanza kesho kupambana tunajua Nchi na Simba nini wanataka

Tunakwenda na Mgunda .... #nguvumoja
Kabisa hatuna namna.. Kocha Zaron Maki ameondoka ghafla na Klabu wangefanya nini kwa siku hizi mbili.

Hata angekuja Pitso Mosimane angeishia kukaa Jukwaani tu..[emoji881] Nguvu Moja
 
Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda, amezungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini Malawi kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL, dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi, huku akitanabaisha kuwa wanaanza kupambana kuanzia kesho kwasababu wanajua klabu ya Simba hitajio lao na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

"Tunaanza kesho kupambana, tunajua nchi inataka nini na Simba inataka nini, kubwa kwetu ni kutimiza wajibu wetu."

"Nimewaona wapinzani wetu, nimeangalia baadhi ya video zao, ni timu ambayo sio ya kubeza, wanacheza kitimu na wanacheza nyumbani, tahadhari zote tutachukua".

"Ukishakubali kuvaa gwanda wewe ni mwanajeshi, naamini Vijana baada ya kuzungumza nao wanaelewa majukumu yao, naamini kesho watajitoa kwa ajili ya Simba SC".
Kocha Mkuu Juma MgundaView attachment 2351403
Huyu jamaa alivyo kama professor @isee!
 
Back
Top Bottom