Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Wakati muda ukizidi kutaraa-dadi (kusogea) kuelekea mechi ya kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga SC itakuwa uwanjani Jumapili Oktoba 27, 2019 kuwakabili matajiri Pyramids FC kutoka Misri, Kocha wa Pyramids Sebastian Desabre aishtukia mbinu ya Yanga SC.
Kocha Desabre raia wa Ufaransa ambaye amewahi kuziona klabu kadhaa za Afrika ikiwemo Wydad Casablanca, Ismailia SC, na timu ya Taifa ya Uganda kabla ya kutua Pyramids, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na hana hofu na mbinu ya Yanga kubadilisha uwanja na kuipeleka mechi hiyo jijini Mwanza kwani wachezaji wake ni Professionals hivyo wanajua kubadilika kulingana na mazingira yalivyo.
Desabre ameongeza kuwa timu yake ina wachezaji ambao wamecheza michuano ya Kimataifa kwa muda mrefu na wamepita viwanja mbalimbali kuliko wapinzani wao hivyo itakuwa rahisi kuendana nao.
Amemaliza kocha wa Pyramids FC, Desabre, kwa kusema anawafahamu wapinzani wao kwa kuwa ameishi Afrika Mashariki kwa muda mrefu hivyo atajaribu kufaidika na ufahamu huo.