Kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga SC dhidi ya Pyramids FC, kocha aishtukia mbinu ya Yanga

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wakati muda ukizidi kutaraa-dadi (kusogea) kuelekea mechi ya kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga SC itakuwa uwanjani Jumapili Oktoba 27, 2019 kuwakabili matajiri Pyramids FC kutoka Misri, Kocha wa Pyramids Sebastian Desabre aishtukia mbinu ya Yanga SC.

Kocha Desabre raia wa Ufaransa ambaye amewahi kuziona klabu kadhaa za Afrika ikiwemo Wydad Casablanca, Ismailia SC, na timu ya Taifa ya Uganda kabla ya kutua Pyramids, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na hana hofu na mbinu ya Yanga kubadilisha uwanja na kuipeleka mechi hiyo jijini Mwanza kwani wachezaji wake ni Professionals hivyo wanajua kubadilika kulingana na mazingira yalivyo.

Desabre ameongeza kuwa timu yake ina wachezaji ambao wamecheza michuano ya Kimataifa kwa muda mrefu na wamepita viwanja mbalimbali kuliko wapinzani wao hivyo itakuwa rahisi kuendana nao.

Amemaliza kocha wa Pyramids FC, Desabre, kwa kusema anawafahamu wapinzani wao kwa kuwa ameishi Afrika Mashariki kwa muda mrefu hivyo atajaribu kufaidika na ufahamu huo.

FB_IMG_1572072652243.jpeg

FB_IMG_1572072652243.jpeg
FB_IMG_1572072835733.jpeg
 
Mpira tumeumaliza tayari huu. Ngoja tuone Pyramids anafungwa tu.
Hofu ipo kwa wenyeji wa mchezo huu..Kwa maana hakuna hata zile ndoto za ushindi na kelele zao yaani wamekuwa baridiiii mno...![emoji23]
 
Haya Mkuu..Usije kuleta visingizio tu hapo baadaye, na wa kwanza atakuwa BanaKongo..!
Mpira tumeumaliza tayari huu. Ngoja tuone Pyramids anafungwa tu.
 
Dunia nzima leo wanafuatilia mechi ya karne kati ya mabingwa wa kihistoria YANGA AFRIKA na Pyramids Ya Misri, mpaka mbu mbu mbu wameitosa timu yao mbovu ya Simba inayocheza na Singida United leo, wako makini kuwafuatilia mabingwa wa kihistoria YANGA AFRIKA.
 
Eti mabingwa wa kihistoria hamuoni hata ganzi kujiita hivyo..[emoji23][emoji23]Hivi kuna kombe linaitwa historia dunia hii?
 
Dunia nzima leo wanafuatilia mechi ya karne kati ya mabingwa wa kihistoria YANGA AFRIKA na Pyramids Ya Misri, mpaka mbu mbu mbu wameitosa timu yao mbovu ya Simba inayocheza na Singida United leo, wako makini kuwafuatilia mabingwa wa kihistoria YANGA AFRIKA.
Yondani akosa mazoezi kisa chai
 
Nawatakia kila la kheri Pyramid. Hao kwasukwasu wapigwe bao 5:0 ili wawe na adabu.
 
Wakati muda ukizidi kutaraa-dadi (kusogea) kuelekea mechi ya kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga SC itakuwa uwanjani Jumapili Oktoba 27, 2019 kuwakabili matajiri Pyramids FC kutoka Misri, Kocha wa Pyramids Sebastian Desabre aishtukia mbinu ya Yanga SC.

Kocha Desabre raia wa Ufaransa ambaye amewahi kuziona klabu kadhaa za Afrika ikiwemo Wydad Casablanca, Ismailia SC, na timu ya Taifa ya Uganda kabla ya kutua Pyramids, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na hana hofu na mbinu ya Yanga kubadilisha uwanja na kuipeleka mechi hiyo jijini Mwanza kwani wachezaji wake ni Professionals hivyo wanajua kubadilika kulingana na mazingira yalivyo.

Desabre ameongeza kuwa timu yake ina wachezaji ambao wamecheza michuano ya Kimataifa kwa muda mrefu na wamepita viwanja mbalimbali kuliko wapinzani wao hivyo itakuwa rahisi kuendana nao.

Amemaliza kocha wa Pyramids FC, Desabre, kwa kusema anawafahamu wapinzani wao kwa kuwa ameishi Afrika Mashariki kwa muda mrefu hivyo atajaribu kufaidika na ufahamu huo.

View attachment 1245536

View attachment 1245536View attachment 1245537
Mwana Kulitaka,Mwana Kulipewa.

Pyramid anaua mtu leo kirumba, Wale wa kubet hela ndio hii.
 
Back
Top Bottom