Kuelekea mechi ya kwanza ya fainali ya CAFCC siku ya jumapili

Kuelekea mechi ya kwanza ya fainali ya CAFCC siku ya jumapili

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Jumapili ndani ya dimba la Mkapa inaenda kuwekwa historia ya fainali ya kwanza ya mchezo wa CAF kwa ngazi ya vilabu. Ni fainali ya CAF confederation cup, tukumbuke tu kuwa mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi katika michuano hii ilikuwa ni rarehe 12 mwezi wa 2 mwaka 2023 dhidi ya Monastir.

Baada ya hapo Yanga hakuwahi kufungwa tena katika hii michuano, kacheza michezo 9
Vs Bamako (H &A)
Vs Tp Mazembe (H &A)
Vs Monastir (H)
Vs Rivers (H & A)
Vs Marumo (H &A)

Katika michezo hiyo 9 Yanga imeshinda michezo 7 na kutoa sare michezo 2 pekee ( nyumbani sare 1 na ugenini sare 1).

Yanga mpaka sasa ni unbeaten kwa miezi mitatu hadi sasa kwa mechi 9.

Ni timu ambayo imeenda kuvunja mbio za record za timu zingine ambazo ni Marumo, na Rivers ambao wote hao walikuwa wanajivunia record nzuri za kupata matokeo chanya kwenye viwanja vyao, lakini Yanga ndio imeenda kutibua record zao.

Je, USM Alger atauweza kuula mfupa mgumu ulioshindikana hadi sasa? Ngoja tuone kipi kitatokea katika dakika 180.
 
Kuna watu wanatamani kusema hii ni michuano ya ndondo, ila wakikumbuka Mwaka jana pamoja na kuloga bado walifurumushwa mashindanoni na adhabu juu wanabaki kusonya tu[emoji23][emoji23]
 
Yanga ifanikiwe kumalizia padogo palipobakia, kazi ngumu sana imefanyika hadi hapa alipofikia.
 
Back
Top Bottom