Kuelekea mechi ya Simba vs Yanga: Karatasi yenye maandishi ya Kiarabu yafukuliwa Uwanja wa Taifa

Kuelekea mechi ya Simba vs Yanga: Karatasi yenye maandishi ya Kiarabu yafukuliwa Uwanja wa Taifa

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
10998813_352769171582448_2132759404031821335_n.jpg


Duru zinadai kuwa karatasi nyeupe iliyokuwa na maandishi ya Kiarabu imefukuliwa katika eneo la kuchezea (pitch) ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Karatasi hiyo iliibuliwa jana asubuhi na watu wanaofanya usafi na huduma zingine katika uwanja huo.

Wadau wamehusisha tukio hilo na pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, ambalo linatarajiwa kupigwa wikiendi hii kwenye Uwanja huo huo.

Chanzo: Kwame Kwax
 
Duh kazi ipo..kama kweli ndo maana mpira wa kibongo haufiki mbali
 
Hiyo karatasi itakuwa imewekwa na timu ya simba, si mwenyekiti wao alisema juzi kwenye mkutano kuwa anashangaa kuona timu yake inafanya vibaya kwenye ligi wakati kamati ya ufundi imefanya kazi ipasavyo kwa kwenda kwa waganga huko pemba na kikwa.

Hilo mbona halihitaji kupapasa macho!
 
Simba naona wameweka majina ya wachezaji wote wa Yanga ili kulogelezea...

Teh teh teh!!!
 
Mmmmmh soka ya bongo,
Mambo yote yanayohusu tamaduni za soka LA bongo tumezifuata
 
Akil za kuambiwa unachanganya na zako, karatasi imefukuliwa uwanjani tuseme hao wafagizi au waangaliz Wa viwanja kazi yao kuchimba chimba uwanjan au kufanya usafi?

Sbb uwezi uona kitu kilichopo chin mpaka uchimbe, na pia uwanjan huwa unamwagiliwa maji kama ndivyo hivyo kweli karatasi itoke mpya hvyo?Hebu acha kulisha watu matango mwitu kaka na jiheshimu kidogo, kama mpira unachezwa kwenye makaratasi hvyo sumbawanga kunakosifika na uchawi wangekuwa na timu hata tatu ligi kuu na nigeria angekuwa mabingwa kombe LA dunia na Africa,

Mpira ni mchezo Wa wazi aliyejiandaa vema na kuwa na Bahati ndio anaibuka mshindi.
 
Mleta mada kachora chora tu asumbue watu vichwa cos kamuweka hadi hamis kiiza duh inaonekana hata Mpira na hbr zake afuatilii.
 
Tujaribu kuwa wachunguzi! Hizo sio nyasi za Uwanja wa Taifa.
 
Uwanjani watu wanaingia tu?

Hakuna ulinzi

Yanga tulieni kimyaaaaa...Hajib anapiga Hart trick jumapili
 
nilishasema na ninarudia tena Bongo hakuna soka bali kuna kabumbu
 
East and Central Africa Tanzania inaongioza kwa imani za kishirikina. Kwan nini hawalogi wakashinda mechi zote tujue moja? Kulipa wachezaji mishahara ni kazi kubwa lakini kuwalipa wachawi ni kazi ndogo.

Maendeleo ya mpira kwa mtindo huu itakuwa ndoto Tanzania.
 
hiyo ni sura kwenye "YASIN"ambayo inayosema kuwafunga maadui wako wasifanye lolote ndio unaandika majina yao.
 
Wafanye Usafi Tu Na Mengineyo Hayawahusu. Wao Wanavyorogana Huko Mitaani Kwao Sisi Huwa TUNAWABUGHUDHI? Watuache Na Yetu.
 
Yanga bhana,fanyeni ushirikina wenu tu muwezavyo lakini tar 8 lazima mkae...
 
Back
Top Bottom