Moto wa
Mnyama Mkali Simba SC, Mabingwa wa Nchi kuendelea Kuwaka tena kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania
TPL, dhidi ya
Mbao FC kutoka jijini Mwanza.
Simba SC pamoja na kukusanya mapato ya alama tatu tatu kutoka kila timu hasa katika mzunguko huu wa mwisho, imemaliza maandalizi yake ya mwisho hivyo kujiweka tayari kwa mchezo huo siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri Stadium mkoani Morogoro.
•••Kulipewa Mwana...Kulitaka Mwana
Kikosi cha
Simba SC, Mnyama Mkali chini ya Kocha Patrick Aussems kipo tayari kwa kipute hicho na kimeaahidi kufanya vema na kuweza kuibuka na ushindi hivyo kukusanya alama tatu sambamba na burudani ya aina yake.
Kikosi cha
Simba SC ambacho kinaupiga mpira mwingi sana Tanzania kwa mechi za ligi kuu na za Kimataifa, kitaingia kwa tahadhari kwani
Mbao FC walibahatisha kuchafua ubao mzunguko wa kwanza hivyo kwa maandalizi yaliyofanywa klabu ya
Simba SC ni dhahir Mbao zitachanika.
View attachment 1058457View attachment 1058458