Kuelekea mechi ya VPL' Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar, Safari ya Ubingwa Inaendelea

Kuelekea mechi ya VPL' Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar, Safari ya Ubingwa Inaendelea

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kupigwa leo Ijumaa ya September 13, 2019, baada ya kusimama kwa wiki mbili, ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakapopepetana na Wakata Miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar FC, kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC, katika safari yake ya kutetea ubingwa wake, amejidhatiti vilivyo kuhakikisha anadondosha kila timu ya VPL, ambayo atakutana nayo ambapo baada JKT, leo hii ni zamu ya Mtibwa Sugar.

Simba SC chini Kocha Patrick Aussems, imejiandaa kuibuka na ushindi kwa kukusanya alama zote tatu pamoja na kuwapa Wanasimba na Wadau wa kandanda burudani ya kiwango bora kabisa ambacho kilichothibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF.

Utaendelea kupata dondoo kuelekea mechi ya leo....Usikose Ukaambiwa..!

Next Level Simba SC Nguvu Moja
IMG_20190913_094926_226.jpeg
IMG_20190913_094838_499.jpeg
 
Hahahaa. Yupo kajaa tele.

Hiki ndio kilichobakia msimu huu jirani. Hawana kingine Watani zangu labda walete na nyuzi za mechi za kombe la FA. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu Shadeeya hata kwako msimu huu hakuna kitakachoendelea, ni kiasi cha muda tutafahamu[emoji23][emoji23][emoji23]..NguvuMoja
 
Back
Top Bottom