Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara,
Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kupigwa leo Ijumaa ya September 13, 2019, baada ya kusimama kwa wiki mbili, ambapo
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakapopepetana na
Wakata Miwa wa Tuliani, Mtibwa Sugar FC, kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC, katika safari yake ya kutetea ubingwa wake, amejidhatiti vilivyo kuhakikisha anadondosha kila timu ya VPL, ambayo atakutana nayo ambapo baada JKT, leo hii ni zamu ya Mtibwa Sugar.
Simba SC chini Kocha
Patrick Aussems, imejiandaa kuibuka na ushindi kwa kukusanya alama zote tatu pamoja na kuwapa Wanasimba na Wadau wa kandanda burudani ya kiwango bora kabisa ambacho kilichothibitishwa na
Shirikisho la Soka Afrika CAF.
Utaendelea kupata dondoo kuelekea mechi ya leo....
Usikose Ukaambiwa..!
Next Level Simba SC Nguvu MojaView attachment 1206150View attachment 1206151