Kuelekea michuano ya CAF: Yanga SC malengo yenu michuano ya CAF ni kufika hatua gani?

Kuelekea michuano ya CAF: Yanga SC malengo yenu michuano ya CAF ni kufika hatua gani?

Kufuatia gazeti la michezo la Mwanaspoti la leo Mei 6,2022 kuandika kuwa sare ya Simba SC dhidi ya Namungo FC na Azam FC kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Yanga SC yatanguliza kwenye michuano ya CAF.

Kwa kuwa kila timu inaposhiriki michuano yoyote, lazima wajiwekee malengo kwa kile ambacho wanakiamini kuwa wanaweza, baada ya kupata maandalizi ya kutosha.

Kwa kuwa Mwanaspoti wamesema hivyo mapema kabisa..Je katika malengo matano haya, Yanga safari hii malengo yenu kwenye michuano ya CAF ni kufika hatua gani?

1. Makundi.
2. Robo Fainali.
3. Nusu Fainali.
4. Fainali.
5. Kombe la CAF.

Wenu: Ghazwat, Ekuweme
Labda useme kombe la Mapinduzi, Yanga na kimataifa wapi na wapi.

Labda kucheza mechi 2 na kurudi. Yaani Utopolo afike robo fainali klabu bingwa, labda km Kuna nafasi za viti maalumu.
 
Kipaumbele Cha Yanga kiwe kuimarisha timu Kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu wa mashindano na uwezo mkubwa na kuondoa wachezaji wenye viwango vya wastani.

Wakumbuke Yanga inahitaji matokeo isiwe kituo Cha kukuza vipaji waje wachezaji watakao ingia first eleven mojakwamoja na kwenda kwenye mashindano ya Caf na kufikia hatua za nusu au final.
Yaani utoke kigamboni uende ukacheze nusu fainali klabu bingwa, acheni utani na masihara.

Km haya ndiyo mawazo yenu basi itawachukua yanga miaka hamsini kufika hata robo fainali.

Chelsea aliwekeza akachukua UCL baada ya miaka kumi, Manchester City huu ni mwaka wa 12 hawajaweza kubeba pamoja na kuwa na mastaa wote wale.
 
Malengo yao ni kwenda kutetema kwenye Preliminary round then Warudi jangwani kufuga vyura waanze kuandika makala za kuitukana Simba waseme ni ya Peter Banda.
Hapo kwa Peter Banda ulimaanisha Abdi Banda bila shaka.
 
Kipaumbele Cha Yanga kiwe kuimarisha timu Kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu wa mashindano na uwezo mkubwa na kuondoa wachezaji wenye viwango vya wastani.

Wakumbuke Yanga inahitaji matokeo isiwe kituo Cha kukuza vipaji waje wachezaji watakao ingia first eleven mojakwamoja na kwenda kwenye mashindano ya Caf na kufikia hatua za nusu au final.
Jibu mujarab kabisa
 
Hili swali tuulize mara baada ya kukabidhiwa ubingwa wa Ligi kuu na pia ule wa kombe la Shirikisho la Azam.

Kwa sasa akili zetu zote tumezielekeza huko.
Chukueni kombe ila msimu ujao msiposajili wachezaji wazuri nauona mwaka mgumu sana kwa manara na mashabiki wa yanga kiujumla
 
Kipaumbele Cha Yanga kiwe kuimarisha timu Kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu wa mashindano na uwezo mkubwa na kuondoa wachezaji wenye viwango vya wastani.

Wakumbuke Yanga inahitaji matokeo isiwe kituo Cha kukuza vipaji waje wachezaji watakao ingia first eleven mojakwamoja na kwenda kwenye mashindano ya Caf na kufikia hatua za nusu au final.
Yanga hii hii hata makundi hawatoboi ubingwa wenyewe wa kuhonga marefa
 
Chukueni kombe ila msimu ujao msiposajili wachezaji wazuri nauona mwaka mgumu sana kwa manara na mashabiki wa yanga kiujumla
Msimu ujao kama mambo yatakwenda kombo...Yule lopolopo hakawii kusema Yanga si baba yangu wala si mama yangu.
 
Yanga hii hii hata makundi hawatoboi ubingwa wenyewe wa kuhonga marefa
Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Majibu yatapatikana kwenye michuano ya Kimataifa..!
 
Chukueni kombe ila msimu ujao msiposajili wachezaji wazuri nauona mwaka mgumu sana kwa manara na mashabiki wa yanga kiujumla
Lazima tuongeze mshambuliaji mwenza wa kumsaidia Mayele, kiungo mshambuliaji, beki 3 wa kwenda kikosi cha kwanza moja kwa moja, nk.

Lakini hata nyinyi pia mtatakiwa kuongeza nguvu pale mbele aisee. Wale wazee wenu kiukweli wamechoka sana. Mnatakiwa kutafuta wakina Kagere wapya.
 
Hamuwezi kufua dafu Kombe la Shirikisho la Azam.. Huko kwingine kuna dalili..!
Wafungaji Wenu Kule Mbele Wote Butu Siku Hizi, Kupiga Penalty Ndo Kabisaaaa Hamjui [emoji23], Sasa Sijui Mtatutoa Kwa Staili Gani Iyo Nusu Fainali Msimu Huu [emoji23]
 
Simba SC Msiongee Sana Na Kujinasibu Kwingi Wakati Kilichokuwa Kinawabeba Ni Ndumba Tu Mixer Mipaka Meusi Kukatisha Uwanjani Pale Kwa Mkapa [emoji23]...Na Jambo Hilo Lilidhihirika Mnapokuwa Nje Ya Tz Ndo Maana Hamna Mlicho Achieve Cha Maana Zaidi Ya Kuishia Robo Fainali Na Kufungashiwa Virago Na Kukutwa Na Shutuma Za Kufanya Uchawi Hadharani Tena Kwenye Nchi Za Watu Bila Ya Hata Kuwa Na Chembe Ya Aibu, Ptuuu! That's Very Unprofessional, Shame On You!!
 
Lazima tuongeze mshambuliaji mwenza wa kumsaidia Mayele, kiungo mshambuliaji, beki 3 wa kwenda kikosi cha kwanza moja kwa moja, nk.

Lakini hata nyinyi pia mtatakiwa kuongeza nguvu pale mbele aisee. Wale wazee wenu kiukweli wamechoka sana. Mnatakiwa kutafuta wakina Kagere wapya.
Umeeleweka mkuu . Hilo halina ubishi. Nakuunga mkono japo wewe ni mteja wa roporopo Manara ila umeongea kitu cha msingi.
 
Ni swala la kujipanga tu kuonesha usiriazi wa kufika nusu fainali, wafanye usajili wa mapema mno, scouting ikibidi iwe imeshaanza na kuanzisha pre contract kwa wachezaji ambao wanahitaji huduma zao kuelekea msimu ujao, ili inapofunguliwa dirisha tu basi watumie siku chache tu kusainishana mikataba pamoja na kukamilisha vibali vya wachezaji wake wapya, isiwe dirisha linafunguliwa ndio wao wanaanza kupiga ana ana doo tumsajili nani.

Wavunje benki wasajili wachezaji haswa sio wachezaji wa kubahatisha, wachezaji ambao moja kwa moja watapata nafasi kuingia kikosi cha kwanza kwaajili ya kuboresha kikosi penye mapungufu kote.

Preseason waanze mapema sana ikibidi ule upuuzi wa siku ya wananchi wauweke kando kama tu itasababisha ufinyu wa muda wa preseason. Preseason hii iwe sio ya kuiga bali iwe kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi, wacheze mechi za kimataifa za kirafiki isiyopungua nne.

La mwisho ni kujipanga vyema kwa mechi zote zinazochezwa nyumbani kwanza ili away usiwe na presha kubwa ya kuhitaji matokeo zaidi ya sare tu ikupeleke mbele.

Hakuna kinachoshindikana kwenye mpira kama umewekeza vyema, na umejipanga vyema, Petro De luanda hao hapo nusu fainali hakuna yeyote aliyewazania kufika huko
 
Back
Top Bottom