PostGE2025 Kuelekea October 29 2026 mwaka mmoja uliopita ulipiga kura ?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Je, ulipiga kura Oktoba 29, 2025?

  • Hapana

    Votes: 23 76.7%
  • Ndio

    Votes: 4 13.3%
  • Hata sijui nisemeje 🤭

    Votes: 3 10.0%

  • Total voters
    30

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Tarehe 29 Oktoba 2026 itatimiza mwaka mmoja tangu Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo Watanzania walipiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.

Lakini mwaka mmoja baadaye, kuna swali moja ningependa tuliweke wazi kupitia wanachama wa JamiiForums:

WEWE MWENYEWE ULIPIGA KURA?

Si kwa kusikia kwa mtu mwingine. Si kwa taarifa za mitandao. Wewe, kama mpiga kura, siku hiyo ulifika kituoni na kupiga kura au hukupiga?

Na kama ulipiga kura:

🇹🇿 Rais: Ulipiga kura ya Rais?
🏛️ Mbunge: Ulipiga kura ya Mbunge katika jimbo unaloishi?
🏘️ Diwani: Ulipiga kura ya Diwani katika kata unayoishi?

Na kama hukupiga kura, sababu ilikuwa ipi?

Sikufika kituoni.Jina langu halikuwepo/ kulikuwa na tatizo la daftari.Nilikuwa mbali na kituo changu.Nilichagua kutopiga kura.Kulikuwa na sababu nyingine.KWA NINI NINAULIZA?

Taarifa na mijadala mbalimbali kuhusu uchaguzi wa 2025 zimeibua maswali kuhusu ushiriki wa wapiga kura na takwimu za kura katika ngazi mbalimbali.

Badala ya kila mtu kusema “Watanzania wengi walifanya hivi” au “Watanzania wengi hawakufanya vile”, hebu tuanze na data ndogo kutoka kwa watu ambao tuko hapa JamiiForums.

Tunataka kujua kitu kimoja tu:

JE, ULIPIGA KURA AU HUKUPIGA KURA?

Na kwa kuwa uchaguzi ulikuwa na kura tatu tofauti, ningependa tuone kama ushiriki wa wanachama wa JF ulikuwa sawa katika kura zote tatu.

Na kama hukupiga kura kabisa, ni sababu gani iliyokufanya usishiriki?

Muhimu: Poll hii si utafiti wa kitaalamu wa Watanzania wote. Ni picha ya wanachama wa JamiiForums walioshiriki kujibu, ambao ni sehemu ndogo tu ya jamii ya Watanzania.

Lakini pengine majibu haya yanaweza kutupa jambo la kutafakari:

Je, kile tunachosikia kwenye mijadala ya uchaguzi kinafanana na uzoefu halisi wa watu waliokuwa kwenye vituo vya kupigia kura?
 
Yaani dah! Ukimuona kwenye mabango hivi ungefikiri binadamu...

ccmtanzania_1790755804904.jpg
 
Mimi kama ShesRise_1
Sababu kwanini sikupiga kura
👇
1.
Lilipoanza kufunguliwa dirisha la kusajiliwa kwenye daftari la wapiga kura sikujisajili kwa sababu nilikuwa tayari nina kitambulisho ambacho nadhani kingeweza kutumika kwa ajili ya kupiga kura

2. Sikuvutiwa na namna mchakato wa uchaguzi ulivyokuwa ukienda
Kwa kipindi fulani sikuona direction nzuri ya mchakato mzima wa uchaguzi
Haikuwa wazi kwangu ni hatua gani ilikuwa inafuata na mambo yalikuwa yanaelekea wapi kulikua na sintofahamu huku watu wakihimizwa wakapige kura wengine wakiwa na slogan ya October tunatoka au Mo29

3. Sikuona ushindani wa kutosha
Kwa hali ya kisiasa iliyokuwepo uchaguzi ulionekana kama hautakuwa na ushindani mkubwa (baadhi ya vyama vikisusa)
Hilo pia lilipunguza motivation yangu ya kushiriki

4. Sikuvutiwa na mgombea yeyote wa urais I told you bro 😅😅
Kwa upande wa urais, kati ya wagombea waliokuwa wakinadi sera zao hakuna aliyenivutia kiasi cha kunifanya nijisikie nina sababu ya kwenda kupiga kura

5. Sababu yangu kubwa zaidi:
KATIBA uwiiiiiii!
Hii ndiyo sababu muhimu zaidi kwangu Ningeshiriki uchaguzi kikamilifu kama kungefanyika maboresho ya Katiba kwa kufuata maoni ya wananchi hususani yale yaliyowasilishwa kupitia Tume ya Warioba

Kwa hiyo kwa kifupi mimi mwa nanchi gender ke sikushiriki uchaguzi na sikufika eneo la kupigia kura📌

Lakini sikuwa nimejifungia ndani la hasha
Nilikuwa mtaani kwa baadhi ya muda, mpaka karibu saa 11 jioni kabla ya muda wa mwisho wa katazo la kutembea saa 12 jioni

Hivyo kutokupiga kura kwangu hakukuwa kwa sababu sikuwa najua uchaguzi upo au ni wapi kituo changu kilipo hapana kabisa nilijua kwa hakika

Nilikuwa na sababu zangu nilizozifikiria na kuamua kutoshiriki na hizo nilizo ziorodhesha hapo juu!

Kisha baadae sana nilianza kusikia kuna damu zimetapakaq aridhi ya Tanganyika
 
Kwa hiyo kwa kifupi mimi mwanachi gender ke sikushiriki uchaguzi na sikufika eneo la kupigia kura📌

Nimekupenda Bure kabisa............🙂
 
Binafsi sikupiga kura kabisa, na kilichonichochea kutokupiga kura kwanza ni Chadema kutoutambua na kutoshiriki uchaguzi ule, pili ni jinsi mgombea wa chama dola alivyojipitisha kwa ubabe na kuvunja katiba hata ya chama chale

NB: haya ni maoni yangu na yaheshimiwe
 
Back
Top Bottom