PostGE2025 Kuelekea October 29 2026 mwaka mmoja uliopita ulipiga kura ?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Je, ulipiga kura Oktoba 29, 2025?

  • Hapana

    Votes: 23 76.7%
  • Ndio

    Votes: 4 13.3%
  • Hata sijui nisemeje 🤭

    Votes: 3 10.0%

  • Total voters
    30
Mimi binafsi, familia yangu na ya zaidi ya waTanzania milioni30 tuliojiandikisha kupiga kura tulipiga kura kwa amani, uwazi, haki na uhuru na kuichagua serikali sikivu ya CCM ambayo inaongozwa na rais Dr.Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia waTanzania wote na kuwaletea maendeleo endelevu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

In fact,
kwa hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ilivyo shwari tangu kumalizika kwa uchaguzi,
huenda zaidi ya waTanzania milioni 45 tukapiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka2030 na kuirejesha tena mamlakani serikali sikivu ya CCM kwa kishindo cha zaidi hata ya kile cha uchaguzi mkuu wa 2025.

Sote ni mashahidi kwamba,
hakuna mTanzania alietumia haki yake ya kupiga kura kikatiba,
anababaika na porojo, mihemko, makasiriko au upotoshaji wa wafuata mkumbo na wasusa uchaguzi humu nchini, nadhani ndio maana our nation chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan is currently more united, more powerful worldwide and more stronger than before.

And nobody can do anything about that light truth
 
Umeulizwa kwa upande wako tu
Hao Watanzania milioni 30 sio swali la mjadala
Soma mada kisha changia kulingana na mada husika Gentleman right ✅️
 
Umeulizwa kwa upande wako tu
Hao Watanzania milioni 30 sio swali la mjadala
Soma mada kisha changia kulingana na mada husika Gentleman right ✅️
ndugu mdau,
ni muhimu zaidi kuzingatia maelezo hayo muhimu ya jumla, mazito na ya maana zaidi
kwa maslahi mapana ya waTanzania wote na itapendeza zaidi.

hakuna haja ya kupoteza wakati na mambo binafsi kwenye jambo la kitaifa tena la kikatiba na lililofanya kizalendo na weledi mkubwa na mamilioni ya waTanzania mwaka 2025.
 
Sikupiga kura maana kiuhalisia lilikuwa ni zoezi la hadaa, kwani washindi tayari walishaandaliwa. Kutokwenda kupiga kura ilikuwa ni sehemu ya kuwaonyesha wanaonajisi uchaguzi kuwa hatuwataki. Tunapokwenda kujazana vituoni hawajali kura zetu, ila wanatumia wingi huo kuonyesha kuwa wao ndio wamechaguliwa na hao watu wengi. Hivyo kitendo cha kutotokea wameona na uhalisia umeonekana kuwa hatuwataki.
 
Weka vote yako kwenye poll hapo juu first page tupate japo picha isiyo kamili kwa kilichotokea October 29
 
Hakukuwepo na uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.
Hapana sikupiga kura
Nilikuwa miongoni mwa mwasimamizi aisee aibu naona mie
Sikupiga wala sitakuja kupiga kura kwa sababu ya uhuni wa maccm
Sikupiga kura
Wakuu nawaomba muwele votes zenu kwenye poll hapo juu first page tupate japo picha isiyo kamili kwa kilichotokea October 29
 
😅😅 ila Samson lol
 
Mi niko Tanzania naelekea tarehe 8/10/2026
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…