PostGE2025 Kuelekea October 29 2026 mwaka mmoja uliopita ulipiga kura ?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Je, ulipiga kura Oktoba 29, 2025?

  • Hapana

    Votes: 23 76.7%
  • Ndio

    Votes: 4 13.3%
  • Hata sijui nisemeje 🤭

    Votes: 3 10.0%

  • Total voters
    30
Sisi tuliopiga kura tunajivunia kwa kutimiza haki yetu ya Kikatiba ya kuiweka Serikali halali madarakani inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Ninyi ambao hamkupiga kura; sawa ni haki yenu, lakini MTAKE MSITAKE mtakuwa chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan hadi mwaka 20130. Na HAKUNA mbwa wala kenge wala nyumbu yoyote inayoweza kukana hilo!

Na ndio maana Kuna mjinga na mropokaji mmoja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa yupo ndani chini ya Serikali hii ya CCM na anasubiri hukumu ya kunyongwa hadi kufa na hata hukumu ikitokea, hakuna mbwa, wala kenge, wala nyumbu atakayefanya nywi wala nywinywinywi!

Pumbavu!!!!!!
 
Uzi huu uende viral hili tuone kula za watu na hapo ndipo tutapata picha ya zile asilimia 98%.
 
Uzi huu uende viral hili tuone kula za watu na hapo ndipo tutapata picha ya zile asilimia 98%.
Haina tofauti na mtaani jembe. Ushahidi kuwa watu walipiga kura wenu ni wale mliowakata vidole vyenye wino wa ushahidi wa aliyepiga kura.

Ushahidi mwingine kuwa watu walipiga kura wengi ni kuangalia idadi ya waliokuwa wanahudhuria mikutano ya kampeni ya CCM, wale wote walienda kupiga kura, askari woote walienda kupiga kura maana ni haki yao na ni amri.
 
Waliojitokeza hawazidi 5%, Kwa mfano kuna kituo kimoja Chang'ombe, DSM Walioandikishwa walikuwa 410, bali waliojitokeza kupiga kura walikuwa 31 tu
Uko sahihi kabisa kwa mkoa wa Dar vituo vingi vilivyopigwa kura watu waliopiga kura hawa kuzidi 30 achilia mbali kura kutokuhesabiwa,


Baada ya mauaji kuanza wasimamizi na askari wote walikimbia na kuacha masanduku ya kura vituoni.

Masanduku ya kura yalichukuliwa mara baada ya shule kufunguliwa kuendelea na masomo na ilikuwa baada ya matokeo kutangazwa.

Swali linabaki, Je matokeo ya Rais, wabunge na madiwani kwa mkoa wa Dar waliyapata wapi ikiwa kura hazikuhesabiwa? Je viongozi hao ni halali au haramu? Je idadi hiyo ndogo sana ya wapiga waliojitokeza ina tafsiri gani ktk uchaguzi?
 
Unapigaje Kura Rais yupo Jela
kura ni haki ya msingi.
Msisahau kuweka votes zenu kwenye poll hapo first page
 
Mimi sikupiga kura. Kwa maoni yangu ule haukuwa uchguzi bali ni ubakaji wa demokrasia. Siamini pia kama kuna watanzania milionitano waliojitokeza kupiga kura. Mtaani kwa penye wapigakura takribani 200 hakujitokeza hata watu kumi kwenye kituo cha kura
 
Baada ya hiI Poll ungeweka na matokeo hata ya urais ndo utaelewa kama tunaishi kwenye nchi tofauti ama kuna watu wameamua tu kujitoa ufahamu.
 
Baada ya hiI Poll ungeweka na matokeo hata ya urais ndo utaelewa kama tunaishi kwenye nchi tofauti ama kuna watu wameamua tu kujitoa ufahamu.
Msisahau kuweka votes zenu kwenye poll hapo first page
 
Hakukuwa na uchaguzi
 
29.10.2025 hakukuwa na uchaguzi bali kulikuwa na igizo la uchaguzi lililofuatiwa na mauaji ya maelfu Watanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…