Kuelekea Pambano la Watani wa Jadi, Simba SC Yanga FC Aprili 29, 2018 Nani Kupapaswa

Kuelekea Pambano la Watani wa Jadi, Simba SC Yanga FC Aprili 29, 2018 Nani Kupapaswa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea pambano la watani wa jadi nchini Tanzania, Simba SC na Yanga FC Jumapili Aprili 29, 2018 nani atapapaswa? Hili ndo swali ambalo linagonga vichwa vya habari upande wa mchezo wa soka kwa wanachama, mashabiki, na wadau mbalimbali wa michezo.

Timu zote mbili Simba na Yanga zimeamua kuweka kambi katika mji wa Morogoro kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Jumapili wiki hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba waliwasili Morogoro wakitokea Iringa ambako wakikipiga na Lipuli FC katika mfululizo wa ligi hiyo ya VPL na kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Samora.

Yanga walitokea mkoani Mbeya ambako walicheza mechi ya ligi hiyo na kutoka sare ya 1-1 na wenyeji Mbeya City.

Mchezo wa Jumapili unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua ambapo Simba watahitaji kushinda ili kujisafishia njia ya ubingwa wakiwa sasa ndo vinara wa (VPL) kwa alama 59 baada ya kucheza mechi 25. Huku Yanga ikawa ya pili kwenye msimamo kwa alama 48 kwa mchezo 23.

Yanga inazidiwa alama 11 na Simba licha ya Yanga kuwa viporo viwili, maana yake ni kwamba ili kutetea ubingwa itabidi washinde Jumapili na washinde mechi zote zilizobaki za ligi kuu, huku wakiwaombea mahasimu wao wapoteze mechi moja. Tukutane uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam April29 tushuhudie yatakayojiri.

IMG_20180425_085938_567.jpg
FB_IMG_1524636878365.jpg
FB_IMG_1524637271005.jpg
 
Ikiwa Mbeya City baada ya kuupiga vilivyo mpira, Yanga wakaona waruweruwe wakasema wachezaji wako 16.

Yamkini Simba SC watakuwa 20 namna Okwi, Bocco na Kichuya watakavyo papasa pale dimba la Mchina.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Tushachinja ngamia mnakufa 2-1.hii ndio yanga
 
Ikiwa Mbeya City baada ya kuupiga vilivyo mpira, Yanga wakaona waruweruwe wakasema wachezaji wako 16.

Yamkini Simba SC watakuwa 20 namna balaa la Okwi, Bocco na Kichuya watakavyo papasa Yanga pale dimba la Mchina.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom