Kuelekea "sikukuu yetu" ya Jumamosi: Hali za kambi zikoje?

Kuelekea "sikukuu yetu" ya Jumamosi: Hali za kambi zikoje?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
NDALA SC

Kwa taarifa za uhakika nilizozipata toka Mkoani Morogoro [ambazo hazina chembe chembe za mashaka], ambapo “ndugu zetu” wameweka kambi ni kua.. hadi kufikia mda huu, ni yapata siku ya pili, MVUA kubwa zinaendelea kunyesha mfululizo. Naposema mfululizo namaanisha kua.. Mchana Mvua, Usiku Mvua. Suala hili limekwenda kuiathiri kambi hii kwa kiwango kikubwa sana.

SIMBA SC

Hali ya hapa kisiwani Unguja ni shwari kabisa, program za kocha zinaenda kama zilivyopangwa. Kwa wachezaji waliokuja huku kambini, hakuna majeruhi.. wote wapo fiti. Molari iliyopo kambini ni kubwa sana [sijawahi ona molari kama hii katika siku za hivi karibuni]. Vijana wanasubiri tu siku ifike, wafanye MAANGAMIZI.

NB:
Kwa hali ilivyo mpaka sasa.. Naona kabisa Jumamosi itakua "Sikukuu" ambayo haijawahi kufanyika kwa Mbabe Mmoja.. Na "Msiba Mzito" uliojaa vilio na majonzi tele kila kona, kwa Mnyoge Mmoja.

NDALA SC, mlipo tupo.. Tukutane Jumamosi.
 
Sio mageni kwao......
Hata kwao si yanajaa maji na wanacheza hivyohivyo AU tuseme umesahau????

PAMBANA NA HALI YAKO.......

Ukitaka kwenda vitani, lazima ufahamu vyema mbinu na njama anazotumia adui ili umkabili vyema. Kwahiyo utake usitake.. tunapamabana na Hali zote, za adui na za kwetu.
Na jumamosi gharika tunalowaandalia lipo pale pale.
 
Ajibu hatrick sima anafungwa kama stend united
 
Tunaokufahamu Sembo hautupi shida sababu hiki ndicho kipindi chako cha majivuno na mbwembwe but amini nakwambia kabla Jogoo hajawika ifikapo April utakuwa ushakimbia na kuwa eneo Korofi.
 
Ajibu hatrick sima anafungwa kama stend united

Nadhani unaukumbuka vyema huu ulinzi tuliomuwekea Agosti 23.

HAJIB NA MBONDE 2.jpg

HAJIB ANAWAACHA.jpg

HAJIB NA MWANJALI.jpg

HAJIB ULINZI.jpg


Sasa ulinzi tunaoenda kuuweka Oktoba 28.. Ni maradufu zaidi ya huo.. Kiwango cha Umakini wake hakina tofauti na kile cha Makomandoo wa North Korea wanaoutoa pindi wanapolinda vinu vyao vya Nyuklia 🙂🙂🙂
 
Back
Top Bottom