Kuelekea Tanzania mpya tuvikatae Visingizio vyote

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Ukweli, haki, nia, dhamira nk, havijifichi:

Sikiliza wanasiasa wote Samia, Majaliwa, Mbowe, Zitto, Lissu, Lipumba nk.

Wasikilize kina Ndugai, Kabudi, Msukuma, Polepole, Bulembo, Nape nk

Ni kitu gani bado hakijulikani?

Kwa hakika watake wasitake Tanzania mpya inakwenda kuzaliwa.

Chile hawa hapa:

IMG_20211223_103348_100.jpg

Tuzikatae longo longo zao zote:

1. Mtu mzima ni miaka 18 na kuendelea.
2. Binadamu wote ni sawa.
3. Demokrasia ni wengi wape katika mazingira huru, yenye usawa na haki.
4. Uchaguzi wowote usiokuwa huru, haki wala kuwa na usawa hauna maana.

Nje ya hapo ni kujaribu kuleta visingizio visivyokubalika.
 
35 years kuwa president? I doubt hata sheria zetu kama zina support hilo, bado tupo gizani kwa mambo mengi sana.

Kumbe ndio maana kila siku tunaimbishwa majina ya wanasiasa yale yale huku nasi tumeshazoea kuyasikia, hatujiulizi kizazi kipya kiko wapi.

Matokeo yake tumekuwa watumwa wa wanasiasa hata wakiwa vigeugeu wasioishi wanachokihubiri bado tumeendelea kuwa watumwa wao kwasababu hakuna backup.
 
Africa bado tunaamin vijana hawawezi kuongoza nchi, ni wazee na watu wa makamo tu ndio wana busara, uwezo na hekima za kuongoza nchi tunasahau kuwa ata wapumbavu na wajinga nao ukua na kuzeeka
 
35 years kuwa president? I doubt hata sheria zetu kama zina support hilo, bado tupo gizani kwa mambo mengi sana.

Kumbe ndio maana kila siku tunaimbishwa majina ya wanasiasa yale yale huku nasi tumeshazoea kuyasikia, hatujiulizi kizazi kipya kiko wapi.

Kwetu kuna kipengele cha kibaguzi chenye kuhitaji minimum age 40 years.

Huu ni ubaguzi na mwendelezo wa visingizio ule ule.

Jingine ni hili la kutaka kuwaaminisha watu kuwa demokrasia kila mahali wana yao.

Longo longo hizi za kujitafutia uhalali wa kujipenyezae nafasi za udikteta hazipaswi kupewa nafasi.
 
Africa bado tunaamin vijana hawawezi kuongoza nchi, ni wazee na watu wa makamo tu ndio wana busara, uwezo na hekima za kuongoza nchi tunasahau kuwa ata wapumbavu na wajinga nao ukua na kuzeeka

Visingizio hivi havina dhamira wala nia njema.

Kwanini kutaka kulisemea sanduku la kura?

Kwanini mpiga kura na mchaguliwa kuwe na mazingatio tofauti ya umri?
 
Kwetu kuna kipengele cha kibaguzi chenye kuhitaji minimum age 40 years.

Huu ni ubaguzi na mwendelezo wa visingizio ule ule.

Jingine ni hili la kutaka kuwaaminisha watu kuwa demokrasia kila mahali wana yao.

Longo longo hizi za kujitafutia uhalali wa kujipenyezae nafasi za udikteta hazipaswi kupewa nafasi.
Kwamba demokrasia sio coca cola, ili ionekane Tanzania tuna demokrasia yetu ya kuwapiga wapinzani na kuwafunga midomo ili wao pekee ndio waendelee na siasa, hii ni demokrasia au udikteta wa kidemokrasia?
 
Tofautisha Age (Miaka) na (Maturity)..., vijana wengi Husasan Tanzania sio Mature wana mambo bado ya mihemko na utoto mwingi..., kwahio mtu kuonyesha vigezo vyako sio mpaka upewe uskani.., anza from the trenches na kuendelea huku unapata uzoefu na kuiva the same guy at 15 au 30 (ingawa anaweza kuwa kiongozi exceptional) lakini at 40 atakuwa better kuliko alivyokuwa at 30

Unaweza ukawa na miaka 70 lakini uzoefu na kujihusisha na uongozi una miaka 5; vilevile unaweza ukawa na miaka 30 lakini uzoefu katika uongozi ni miaka 20.... Ila on average logic inatwambia the more mature you are the better, and the more time you are into doing something the better your are....
 
Hawa ni wa kuwakomalia. Lazima wajue demokrasia ni moja. Kuna demokrasia na udikteta, hakuna katikati.

Kama ilivyo kwa coca cola wanavyotaka kubeza, na demokrasia ni hivyo hivyo. Demokrasia ni moja.

Unaweza kuwa dikteta au democrat hakuna fraction.
 
Tofautisha Age (Miaka) na (Maturity)..., vijana wengi Husasan Tanzania sio Mature wana mambo bado ya mihemko na utoto mwingi..., kwahio mtu kuonyesha vigezo vyako sio mpaka upewe uskani.., anza from the trenches na kuendelea huku unapata uzoefu na kuiva the same guy at 15 au 30 (ingawa anaweza kuwa kiongozi exceptional) lakini at 40 atakuwa better kuliko alivyokuwa at 30

Unaweza ukawa na miaka 70 lakini uzoefu na kujihusisha na uongozi una miaka 5; vilevile unaweza ukawa na miaka 30 lakini uzoefu katika uongozi ni miaka 20.... Ila on average logic inatwambia the more mature you are the better, and the more time you are into doing something the better your are....

Kwanini kulisemea sanduku la kura? Anayefaa si atachaguliwa na watu?

Kwamba vijana waafrika ni immature? Mbona kutaka kujidhalilisha hivyo? Kwanini kutusemea na wengine tusiokuwamo humo?

Binadamu wote ni sawa na demokrasia ni moja. Si zaidi si pungufu!

Kusema kweli zinachosa siasa hizi zilizojaa dhuluma na ubinafsi uliopitiliza.
 
ndio
hashtag #MATAGA

Huyo bwana alitukosea sana. Angalia mawili haya kujiridhisha kuwa alikuwa mzigo:

3. Demokrasia ni wengi wape katika mazingira huru, yenye usawa na haki.
4. Uchaguzi wowote usiokuwa huru, haki wala kuwa na usawa hauna maana.

Huyo bwana kwa hakika aliturudisha nyuma miaka mingi sana kwenye ujenzi wa Tanzania mpya.

Ya wasiojulikana yalikuwa ni yatokanayo na kukosa kwake ridhaa.

Zingatia: "Wenzake kindaki ndaki wakiwamo kina Bulembo, Nape, Makamba, Kinana nk, kwani wanasema je?"
 
Kwanini kulisemea sanduku la kura? Anayefaa si atachaguliwa na watu?
Kama unadhani anayefaa ndio huwa anachaguliwa basi pole ndugu yangu Kwanza kabisa demokrasia popote duniani iliyopo wanaochagua ni wanaonominate yaani mpiga kura anapewa choice ya kuchagua kati ya aliochaguliwa na wenye power of nomination.... hio ni moja alafu kama public ingekuwa informed kina Adolf Hitler au Trumps (Populists na Extremists wangekuwa hawashindi
Kwamba vijana waafrika ni immature? Mbona kutaka kujidhalilisha hivyo? Kwanini kutusemea na wengine tusiokuwamo humo?
ambao hawamo humo ingieni kundini pia Comment yangu inasema vijana wengi husasan watanzania ni immature (refer ujinga unaofanywa na wakuu wa wilaya etc, yaani ubabe ubabe na utoto mwingi) nadhani ungejua maana ya immature ungeelewa immature inaondolewa na experience ambayo ni direct proportional na muda (immature ni kwamba not fully developed) kwahio which means huyo huyo ambae leo ni immature kesho atakuwa matured, thus atumie muda wake wakati anaendelea ku-develop akiwa katika industry husika akionyesha umahili wake
Binadamu wote ni sawa na demokrasia ni moja. Si zaidi si pungufu!

Kusema kweli zinachosa siasa hizi zilizojaa dhuluma na ubinafsi uliopitiliza.
Kuhusu Demokrasia I have a different take..., Hii Demokrasia as is right now is not working (sio kwa Tanzania wala America) tuhahitaji kuibadilisha kuendana na wakati (ukipata muda pitia hapo chini, ingawa sijamalizia)

Tofautisha Age (Miaka) na (Maturity)..., vijana wengi Husasan Tanzania sio Mature wana mambo bado ya mihemko na utoto mwingi..., kwahio mtu kuonyesha vigezo vyako sio mpaka upewe uskani.., anza from the trenches na kuendelea huku unapata uzoefu na kuiva the same guy at 15 au 30 (ingawa anaweza kuwa kiongozi exceptional) lakini at 40 atakuwa better kuliko alivyokuwa at 30

Unaweza ukawa na miaka 70 lakini uzoefu na kujihusisha na uongozi una miaka 5; vilevile unaweza ukawa na miaka 30 lakini uzoefu katika uongozi ni miaka 20.... Ila on average logic inatwambia the more mature you are the better, and the more time you are into doing something the better your are....
Kwa mtazamo wangu, silaha kubwa ya kiongozi yeyote duniani bila kujali umri alionao, au taaluma yake, ni hekima.

Kiongozi akishajua ni wakati gani aseme nini, au asiseme nini, wakati gani afanye nini, au asifanye nini, kwa kutambua kabla athari za maamuzi yake atakayofanya/kusema baada ya kusema, huyo kwangu ndie.

Hili halijalishi umri, tumeshakuwa na viongozi wa umri mkubwa lakini tumeona wanavyosumbuliwa na emotions, mambo madogo wanalipiza visasi, matokeo yake wanawaumiza walio chini yao kimamlaka bila kosa lolote kwasababu hawana mtetezi.

Mambo mengine yanayohusisha utendaji kazi kama uzoefu n.k hayo yatakuja yenyewe kwakuwa kiongozi atakuwa tayari kupokea ushauri wa wasaidizi wake kama ataona una manufaa na kuufanyia kazi.
 
Kwa mtazamo wangu, silaha kubwa ya kiongozi yeyote duniani bila kujali umri alionao, au taaluma yake, ni hekima.

Kiongozi akishajua ni wakati gani aseme nini, au asiseme nini, wakati gani afanye nini, au asifanye nini, kwa kutambua kabla athari za maamuzi yake atakayofanya/kusema baada ya kusema, huyo kwangu ndie.

Hili halijalishi umri, tumeshakuwa na viongozi wa umri mkubwa lakini tumeona wanavyosumbuliwa na emotions, mambo madogo wanalipiza visasi, matokeo yake wanawaumiza walio chini yao kimamlaka bila kosa lolote kwasababu hawana mtetezi.
Hekima inapungua au inaongezeka na umri ?

Kiongozi ni kiongozi pale unapokuwa ngazi ya juu au ngazi yoyote unaweza ukawa kiongozi ?

Hivyo basi utaona kama ilivyo wine (it gets better with time) yaani ina-mature, kwahio hao madogo wenye ndoto za kuwa viongozi waingie kwenye ngoma waanze kuicheza kwa kuangalia na kujichanganya na wengine huku wakiendelea kuiva vizuri (watatokea wachache exceptional) ila wasiulizwe wana miaka mingapi bali wameshafanya nini ku-deserve hio position kwahio ni vema zaidi wakianzia position ndogo ndogo huku wakipanda na kuonyesha umahili wao (kuongea pekee hakusaidii) tumeshaona wengi they can talk a good game lakini matokeo sifuri (ndio maana mimi nikasema miaka ya umri kwangu haina tija sana nachoangalia ni miaka kwenye industry husika) ili uongoze hio industry miaka yako / experience katika hio sekta is what counts...

Ila hapa unaongea na mtu anayeamini system zaidi na taasisi kuliko mtu..., kwahio huenda nikawa biased (kwangu mimi katika hizo system imara kiongozi anakuwa symbolically tu) hata ukiweka sanamu au robot mambo yanakwenda (chombo kinachohitaji hands on 24/7 ni chombo kibovu)
 
Kama unadhani anayefaa ndio huwa anachaguliwa basi pole ndugu yangu Kwanza kabisa demokrasia popote duniani iliyopo wanaochagua ni wanaonominate yaani mpiga kura anapewa choice ya kuchagua kati ya aliochaguliwa na wenye power of nomination.... hio ni moja alafu kama public ingekuwa informed kina Adolf Hitler au Trumps (Populists na Extremists wangekuwa hawashindi

ambao hawamo humo ingieni kundini pia Comment yangu inasema vijana wengi husasan watanzania ni immature (refer ujinga unaofanywa na wakuu wa wilaya etc, yaani ubabe ubabe na utoto mwingi) nadhani ungejua maana ya immature ungeelewa immature inaondolewa na experience ambayo ni direct proportional na muda (immature ni kwamba not fully developed) kwahio which means huyo huyo ambae leo ni immature kesho atakuwa matured, thus atumie muda wake wakati anaendelea ku-develop akiwa katika industry husika akionyesha umahili wake

Kuhusu Demokrasia I have a different take..., Hii Demokrasia as is right now is not working (sio kwa Tanzania wala America) tuhahitaji kuibadilisha kuendana na wakati (ukipata muda pitia hapo chini, ingawa sijamalizia)

Msitumie nguvu nyingi kutaka kutuaminisha katika yale yaliyo na maslahi kwenu ambayo labda mngependa yadumu.

Nia yetu iko wazi, na hii ndiyo Tanzania mpya tunayoitaka:

1. Binadamu wote kuwa sawa.
2. Wote wenye akili timamu na zaidi ya miaka 18 wanastahili haki zote kama raia.
3. Chaguzi kufanyika katika mazingira ya usawa, uhuru na haki.
4. Chaguzi kuwa ndizo pekee zenye kuamua washindi.
5. Nchi kuongozwa kwa misingi ya wengi wape (maana halisi ya demokrasia popote).

Hizi zako zingine ni porojo tulizozizowea ambazo vizuri kujua mwisho uko karibu:

"Kwani Trump yuko wapi? Wakuu wa wilaya vijana unaowaongelea wamechaguliwa na nani?"

IMG_20210704_143127_720.jpg

Uniform zao unazitambua?

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.

Nchi si mali binafsi.
 
Hekima inapungua au inaongezeka na umri ?

Kiongozi ni kiongozi pale unapokuwa ngazi ya juu au ngazi yoyote unaweza ukawa kiongozi ?

Hivyo basi utaona kama ilivyo wine (it gets better with time) yaani ina-mature, kwahio hao madogo wenye ndoto za kuwa viongozi waingie kwenye ngoma waanze kuicheza kwa kuangalia na kujichanganya na wengine huku wakiendelea kuiva vizuri (watatokea wachache exceptional) ila wasiulizwe wana miaka mingapi bali wameshafanya nini ku-deserve hio position kwahio ni vema zaidi wakianzia position ndogo ndogo huku wakipanda na kuonyesha umahili wao (kuongea pekee hakusaidii) tumeshaona wengi they can talk a good game lakini matokeo sifuri (ndio maana mimi nikasema miaka ya umri kwangu haina tija sana nachoangalia ni miaka kwenye industry husika) ili uongoze hio industry miaka yako / experience katika hio sekta is what counts...

Ila hapa unaongea na mtu anayeamini system zaidi na taasisi kuliko mtu..., kwahio huenda nikawa biased (kwangu mimi katika hizo system imara kiongozi anakuwa symbolically tu) hata ukiweka sanamu au robot mambo yanakwenda (chombo kinachohitaji hands on 24/7 ni chombo kibovu)
Umri sio kigezo cha kuwa na hekima, nimeshakuonesha pale juu viongozi wenye umri mkubwa wanavyopata tabu ku control emotions zao.

Suala la experience nalo unaturudisha nyuma kule kule tunapotaka kutoka, mbona wazee wa zamani kina Salim Ahmed Salim, Nyerere, na wengine walianza kuongoza wakiwa na umri mdogo, kwanini sasa hivi isiwezekane?

Hata kigezo cha kusema wakati ule hapakuwepo na wasomi wengi kwangu nakipinga, hata kama siku hizi wasomi wapo, ndio wanatakiwa wawepo vijana wengi zaidi kwenye uongozi ili kuendana na dunia inavyokwenda, lakini sio wazee waendelee kuongoza.

Nashangaa siku hizi watu wanafikisha miaka hamsini kwenye uongozi lakini bado wanaitwa vijana, kule UV CCM panachekesha sana, sasa vijana wa miaka 35 wataonekana lini?
 
Msitumie nguvu nyingi kutaka kutuaminisha katika yale yaliyo na maslahi kwenu ambayo labda mngependa yadumu.

Nia yetu iko wazi na hii ndiyo Tanzania mpya tunayoitaka:
Naanza kupata mashaka na mtu ninayoongea nae kuhusu reasoning yake..., Naona wewe hapo una wao wanaotumia nguvu nyingi na nyie wenye nia ya Tanzania mpya.., hatuwezi kuelewana sababu wewe unaongelea Tanzania ya nyie na wao wakati mimi nina ndoto za Tanzania moja yaani (Tanzania Yetu) ingawa ningependa dunia yetu (ila that's a dream too far)...
1. Binadamu wote ni sawa.
2. Wote wenye akili timamu na zaidi ya miaka 18 wanastahili haki zote kama raia.
3. Chaguzi kufanyika katika mazingira ya usawa, uhuru na haki.
Hakuna aliyebisha wala sikatai hata kama mtu ni exceptional na ana miaka 12 anaweza kufanya kitu asikifanye, ila naongelea logic huyo mtu wa miaka 12 akifika miaka 20 atakuwa bora zaidi kwahio hekima inaniambia (hekima sio sheria) kabla sijampa huyo dogo nchi wa miaka 12 kwanza tumpe wilaya, mkoa n.k. (sio kumpima tu bali kuendelea kumpika) na hio ni reasoning yangu kwa manufaa ya nchi sio kwa manufaa kwamba sasa hii ni zamu yetu hao zamu yao imekwisha...
4. Chaguzi kuwa ndizo pekee zenye kuamua washindi.
Kama unadhani wananchi ndio wanachagua viongozi kwenye hizi demokrasia za sasa.., think again...
5. Nchi kuongozwa kwa misingi ya wengi wape (maana halisi ya demokrasia popote).
Wengi wape huku ukiangalia haki za wachache kuepuka Tyranny of the Majority (Kama Mbwa mwitu watatu na Kondoo mmoja wakipiga kura kuhusu kitoweo cha jioni basi ni Kondoo pekee ndio atakayejikuta kikaangoni)
Hizi zako zingine ni porojo tulizozizowea ambazo vizuri kujua mwisho uko karibu:

"Kwani Trump yuko wapi? Wakuu wa wilaya vijana unaowaongelea wamechaguliwa na nani?"
Trump yupo na kuna uwezekano akarudi tena..., Trump alichaguliwa na so called forgotten Man kwa ku-promise what the forgotten man wanted to hear alishinda (thus my point kuhusu the un-informed voter) na watu kama Trump wataendelea na wanaendelea kushinda kila siku kutokana na weakness ya demokrasia... qouting Socrates in the book Republic....

The sweet shop owner can make the argument against the doctor that “he gives you bitter syrups and pokes holes on you, cuts your skin and take your blood,” but he can offer you many sweets and candies. Surely no one with their right mind would vote for the doctor would it?

Kwahio the point about Trump ni kwamba kiongozi anaweza kuchaguliwa kwa kuwahadaa wananchi kwa kuwaambia achaguliwe matatizo yao yatakwisha (offering empty promises) wakuu wa wilaya ni point yangu hawa madogo wengi waliochaguliwa bila kuiva na kuleta utoto mwingi hence kuharibu maisha ya watu (sio kwamba watu matured hawawezi kufanya hivyo..., ila labda hao madogo wangeshapevuka wasingefanya leo waliyoyafanya jana)
 
Umri sio kigezo cha kuwa na hekima, nimeshakuonesha pale juu viongozi wenye umri mkubwa wanavyopata tabu ku control emotions zao.
Tunakwenda mbele na nyuma huwezi kuwa na hekima at 18 alafu at 25 hekima ika-evaporate..., na uongozi sio kitu pekee cha wewe kufanya mambo unaingia kwenye system at whatever age na kupambana ila unapewa utmost job / baada ya kupikwa
Suala la experience nalo unaturudisha nyuma kule kule tunapotaka kutoka, mbona wazee wa zamani kina Salim Ahmed Salim, Nyerere, na wengine walianza kuongoza wakiwa na umri mdogo, kwanini sasa hivi isiwezekane?
Hapa tunaongelea kuanza kuongoza au kupewa uongozi wa juu kabla ya kuanza kwenyewe huko kuongoza..., kabla ya kuanza kwao huko kuongoza walifanya nini example kabla ya Salim kwenda OAU alitokea wapi ?
Hata kigezo cha kusema wakati ule hapakuwepo na wasomi wengi kwangu nakipinga, hata kama siku hizi wasomi wapo, ndio wanatakiwa wawepo vijana wengi zaidi kwenye uongozi ili kuendana na dunia inavyokwenda, lakini sio wazee waendelee kuongoza.
Wasomi ndio mengine hayo hayo..., tunayopotea kila siku.... Unachagua mtu sababu amesoma na sio sababu anauwezo wa kuongoza, kuongoza ni Karama sio kila mtu anaweza kuongoza, kiongozi ni mtu mwenye charisma anayesikilizwa anaweza asiwe mjuvi kuliko wengine lakini anaweza kuunganisha hau wajuvi, wajuzi na wataalamu kuwa kitu kimoja....
Nashangaa siku hizi watu wanafikisha miaka hamsini kwenye uongozi lakini bado wanaitwa vijana, kule UV CCM panachekesha sana, sasa vijana wa miaka 35 wataonekana lini?
Hapo ndio kosa lenyewe huko kwenye vijana ndio wangeazia kupikwa hata kama wana miaka 18, na hata kama sio huko mtaani na underground wanaweza wakaform movement za kuwaunganisha watu na kuwaongoza sio mpaka wawe Rais ndio tuseme wanaongoza.... Mwisho wa siku naangalia CV ya mtu katika the highest Job, na kama ni highest Job ni vema akiwa amepitia kwenye ngazi tofauti
 
Back
Top Bottom