Uko sahihi mkuu:Umri sio kigezo cha kuwa na hekima, nimeshakuonesha pale juu viongozi wenye umri mkubwa wanavyopata tabu ku control emotions zao.
Suala la experience nalo unaturudisha nyuma kule kule tunapotaka kutoka, mbona wazee wa zamani kina Salim Ahmed Salim, Nyerere, na wengine walianza kuongoza wakiwa na umri mdogo, kwanini sasa hivi isiwezekane?
Hata kigezo cha kusema wakati ule hapakuwepo na wasomi wengi kwangu nakipinga, hata kama siku hizi wasomi wapo, ndio wanatakiwa wawepo vijana wengi zaidi kwenye uongozi ili kuendana na dunia inavyokwenda, lakini sio wazee waendelee kuongoza.
Nashangaa siku hizi watu wanafikisha miaka hamsini kwenye uongozi lakini bado wanaitwa vijana, kule UV CCM panachekesha sana, sasa vijana wa miaka 35 wataonekana lini?
Haya mambo hayahitaji maneno mengi, simply kama iliwezekana kwa hao wakati huo, kwanini leo isiwezekane?Uko sahihi mkuu:
1. Akiwa 22 Salim alikuwa balozi wa Tanzania Egypt.
2. Nyerere alipokuwa 35 alikuwa kinara TANU kwenye kupigania uhuru.
3. Nyerere alipokuwa 39 alikuwa waziri mkuu wa Tanganyika.
4. List ni ndefu
Ushahidi kuwa age "is just a number" kote juu na hata chini.
Visingizio vyote ni vya kupigwa vita.
Bottom line binadamu wote ni sawa.
Yeyote 18 and above anastahili kupiga na hata kupigiwa kura.
Matokeo ya kura ya haki ndiyo pekee yaliyo halali.
AFRIKA HUWEZI KUWAPA VIJANA UTAWALA, HAWAWEZI KUJICONTROL NA MARA ZOTE HUJIONGEZEA MIULA. KWANGU MIMI TUNGEONGEZA UMRI WA KUGOMBEA URAIS NA KUFIKIA 50.Africa bado tunaamin vijana hawawezi kuongoza nchi, ni wazee na watu wa makamo tu ndio wana busara, uwezo na hekima za kuongoza nchi tunasahau kuwa ata wapumbavu na wajinga nao ukua na kuzeeka
AFRIKA HUWEZI KUWAPA VIJANA UTAWALA, HAWAWEZI KUJICONTROL NA MARA ZOTE HUJIONGEZEA MIULA. KWANGU MIMI TUNGEONGEZA UMRI WA KUGOMBEA URAIS NA KUFIKIA 50.
Basi na MASHOGA waachiwe mzee, mbona mnapenda uhuru wa kipuuzi kiasi hiki??Hayo ni mawazo yako. Kistaarabu huwa mawazo yakigongana kura ya maoni huamua.
Utolewaji elimu kabla ya kura ni haki ya kiraia. Tukutane huko. Mawazo mgando hayajengi.
Naanza kupata mashaka na mtu ninayoongea nae kuhusu reasoning yake..., Naona wewe hapo una wao wanaotumia nguvu nyingi na nyie wenye nia ya Tanzania mpya.., hatuwezi kuelewana sababu wewe unaongelea Tanzania ya nyie na wao wakati mimi nina ndoto za Tanzania moja yaani (Tanzania Yetu) ingawa ningependa dunia yetu (ila that's a dream too far)...
Hakuna aliyebisha wala sikatai hata kama mtu ni exceptional na ana miaka 12 anaweza kufanya kitu asikifanye, ila naongelea logic huyo mtu wa miaka 12 akifika miaka 20 atakuwa bora zaidi kwahio hekima inaniambia (hekima sio sheria) kabla sijampa huyo dogo nchi wa miaka 12 kwanza tumpe wilaya, mkoa n.k. (sio kumpima tu bali kuendelea kumpika) na hio ni reasoning yangu kwa manufaa ya nchi sio kwa manufaa kwamba sasa hii ni zamu yetu hao zamu yao imekwisha...
Kama unadhani wananchi ndio wanachagua viongozi kwenye hizi demokrasia za sasa.., think again...
Wengi wape huku ukiangalia haki za wachache kuepuka Tyranny of the Majority (Kama Mbwa mwitu watatu na Kondoo mmoja wakipiga kura kuhusu kitoweo cha jioni basi ni Kondoo pekee ndio atakayejikuta kikaangoni)
Trump yupo na kuna uwezekano akarudi tena..., Trump alichaguliwa na so called forgotten Man kwa ku-promise what the forgotten man wanted to hear alishinda (thus my point kuhusu the un-informed voter) na watu kama Trump wataendelea na wanaendelea kushinda kila siku kutokana na weakness ya demokrasia... qouting Socrates in the book Republic....
The sweet shop owner can make the argument against the doctor that “he gives you bitter syrups and pokes holes on you, cuts your skin and take your blood,” but he can offer you many sweets and candies. Surely no one with their right mind would vote for the doctor would it?
Kwahio the point about Trump ni kwamba kiongozi anaweza kuchaguliwa kwa kuwahadaa wananchi kwa kuwaambia achaguliwe matatizo yao yatakwisha (offering empty promises) wakuu wa wilaya ni point yangu hawa madogo wengi waliochaguliwa bila kuiva na kuleta utoto mwingi hence kuharibu maisha ya watu (sio kwamba watu matured hawawezi kufanya hivyo..., ila labda hao madogo wangeshapevuka wasingefanya leo waliyoyafanya jana)
Kwan wazee hawawezi jiongezea mda wa kubaki madarakani?AFRIKA HUWEZI KUWAPA VIJANA UTAWALA, HAWAWEZI KUJICONTROL NA MARA ZOTE HUJIONGEZEA MIULA. KWANGU MIMI TUNGEONGEZA UMRI WA KUGOMBEA URAIS NA KUFIKIA 50.
Basi na MASHOGA waachiwe mzee, mbona mnapenda uhuru wa kipuuzi kiasi hiki??
Afrika ni bara giza huwezi mpatia kiongozi mwenye umri wa chini ya miaka 40 au chini ya 50 na asiwe na tamaa ya kujiongezea Muhula, Rejea NKURUNZIZA, J KABILA, KAGAME, NENDA AFRIKA MAGHARIBI utajionea hayo.
Sio kila kinachokujia kichwani ni cha maana vingine ni UPUPU tu mzee.
Kaa chini tafakari, hii nchi ashinde POLEPOLE, KHERI JAMES, ZITTO KABWE, NK. Huwezi iga demokrasia ya Sehemu fulani wakati unajua fika kwako haiwezi kufit. Mbona hamtolei mfano URUSI?
UHURU USIO NA MIPAKA SIO UHURU NI VURUGU MZEE.