Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Je, serikali ina majibu ya kuwaeleza Watanzania ambao mpaka leo vijiji vyao havijapatiwa umeme nini sababu inayochelewesha ili hali kila siku tunahadithiwa kwamba hela zipo tutembee kifua mbele. Vipi mpango wa kunusuru kaya masikini unaendeleaje? Je, zoezi linaenda kama lilivyopangwa? Huduma za jamii zimeimarika kwa asilimia ngapi? Matumizi ya mashine za EFD yanaongezeka au yanapungua siku hadi siku?
Baada ya kukataza pengine mikutano ya kisiasa na bunge live. Je nini faida iliyopatikana au nini changamoto zilizojitokeza? Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha upatikanaji wa ajira nchini unaimarika zaidi na zaidi? Vipi uboreshaji wa michezo nchini ili itumike kama mbadala wa ajira kuendana na ulimwengu wa sasa?
Katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya tano kipato cha mwananchi mmoja mmoja kimeimarika zaidi au kimedumaa? Vipi vituo vya afya vinavyojengwa na ambavyo tayari vimekamilika nchini vimepatiwa watumishi wa kutosha au ndo bado janja janja?