Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Majibu ya kitendawili cha 'Governor's Dilemma' yanamkweza Tundu Lissu na kuwashusha Mbowe, Samia na Hussein Mwinyi

Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Majibu ya kitendawili cha 'Governor's Dilemma' yanamkweza Tundu Lissu na kuwashusha Mbowe, Samia na Hussein Mwinyi

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,089
Reaction score
2,725
Lissu.png

"Hata alipokwisha kunena, Yesu alimwambia Simoni Petro, twika mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika” (Luka 5:4-6)

"Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda." (Mathayo 16:18)

Namwona Tundu Antipas Lissu kama jembe la Yesu aliyeitwa Petro, na hivyo jiwe kuu la pembeni katika zama hizi mtanziko wa ugavana (governor's dilemma) ulioigubika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika siasa za Tanzania Lissu anao uwezo kuwa game changer kabla ya 2025 hasa kuputia nafasi ya uenyekiti wa Chadema anayoipigania kwa sasa.

Hivyo, uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa Chadema kwa lengo la kuirithi nafasi ya mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe, umenipa sababu ya kumlinganisha na watu wengine watatu.

Napendekeza kwamba, kiutawala, Samia Suluhu Hassan, Hussein Mwinyi na Freeman Mbowe wanafanana kwa sababu ya dosari moja ifuatayo:

Wote hutoa majawabu ya kubahatisha kila wanapojaribu kutegua kitendawili cha MTANZIKO WA UGAVANA, yaani governor's dilemma.

Kitendawili hiki kinakuja hivi: Ugavana ni kazi ya kuongoza taasisi kwa kusimamia utendaji wa kazi zinazotakiwa kufanyika ili kufikia malengo fulani.

Kwa hiyo, mtawala au gavana ni mtu anayefanya kazi ya utawala au ugavana.

Yaani, gavana wa taasisi ni kama gavana ya mwendokasi wa gari, ambayo huzuia injini isikimbie sana hadi kuungua wala kudorora sana hadi kusimama, ili hatimaye basi liwafikishe abiria salama.

Lakini, hakuna mtawala au gavana anayeweza kuongoza taasisi kwa kufanya kazi zote kwa mkono wake mwenyewe.

Yaani ni kwa nadra sana mtawala atatekeleza majukumu yake kwa kutumia direct governance strategy pekee.

Badala yake, ni lazima kila mtawala afanye kazi zake kupitia wasaidizi wake kadhaa (intermediaries).

Yaani mara nyingi kila mtawala hutekeleza majukumu yake kwa kutumia indirect governance strategy.

Kwa ujumla, mtawala anaweza kufanya kazi zake kupitia wasaidizi wa aina nne.

Wasaidizi hao kwa Kiingereza ni: delegatees, cooptees, orchestratees na trustees.

Nitaeleza kwa ufupi michakato inayozalisha wasaidizi hawa, yaani delegation, cooptation, orchestration na entrustment.

Delegation ni kitendo cha mtawala kumega madaraka yake na kuyatoa kama kasma kwa mtu baki anayekubali kufanya kazi kwa niaba ya na kwa faida ya mtawala.

Mtawala hufanya usimamizi wa msaidizi wake kulingana na mkataba kati ya pande mbili.

Usimamizi huu huweza kufanyika kwa kutumia mbinu za kulazimisha (hard control mechanisms) kabla, wakati na baada ya kupatikana kwa msaidizi.

Aidha, mtawala hubaki na haki ya kutwaa madaraka aliyo nayo mtu baki, siku akitaka.

Cooptation ni kitendo cha mtawala kukodi au kuazima madaraka aliyo nayo mtu baki kwa kumshawishi akubali kutumia madaraka hayo katika kufanikisha malengo ya pamoja kati ya mtawala na huyo mtu baki.

Katika uhusiano huu mtawala hubaki na mamlaka ya kufanya usimakizi kwa kutumia mbinu zashamlazimisha mtu baki kila inapobidi.

Lakini mtawala anakuwa hana uwezo wa kufuta madaraka aliyo nayo mtu baki, kwa kuwa mamlaka hayo hayakutoka kwake mtawala.

Orchestration ni kitendo cha kukodi au kuazima sehemu ya madaraka aliyo nayo mtu baki ili madaraka hayo yatumike katika kufanikisha malengo ya pamoja kati ya mtawala na mtu wa kazi.

Mtawala anakuwa hana mamlaka ya kumlazimisha mtu wa kati kufanya kazi husika.

Mtawala husimamia kazi za msaidizi wake kwa kutumia mbinu za kubembeleza na ushawishi wa hali na Mali (soft control mechanisms)

Aidha mtawala anakuwa hana uwezo wa kutwaa madaraka aliyo nayo mtu wa kati.

Na trusteeship/Entrustment ni kitendo cha mtawala kumega sehemu ya madaraka yake na kuyatoa kwa mtutbaki ili madaraka hayo yatumike katika kufanikisha malengo ya pamoja kati ya mtawala na mtu wa kazt.

Mtawala anakuwa hana uwezo wa kumzuia mtu wa kati kuyatumia mamlaka hayo vibaya baada ya kuwa yamepokelewa.

Tazama viambatanisho kwa ufafanuzi mpana wa mbinu hizi.

Mikakati hii minne ya kiutawala inaweza kufupishwa, kufananishwa na kutofautishwa kwa njia ya jedwali lifuatalo:

1734853550435.png

Kwa hiyo, kufanya kazi ya utawala wa taasisi kupitia watu wa kati kwa ufanisi kunahitaji mtawala mwenye sifa kuu tano.

  1. Mosi, mtawala lazima awe na uwezo wa kujibu swali lifuatalo kwa ufasaha: Ni wakati gani itumike mbinu ya orchestration, entrustment, cooptation, delegation, au mseto fulani wa mbinu hizi za kiutawala?
  2. Pili, mtawala lazima awe na uwezo wa kutofatisha kati ya “intermediate actors mobilization by granting authority to them” na “intermediate actors mbolisation by enlisting authority from them,” na wakati gani atumie mbinu ya kwanza au mbinu ya pili.
  3. Tatu, mtawala lazima awe na uwezo wa kujua ni lini na wapi atumie mbinu za usimamizi zinazohusisha kubembelezana (soft controls) dhidi ya mbinu za usimamizi zinazohusisha kulazimishana (hard controls)
  4. Nne, mtawala lazima awe na uwezo wa kuwatambua na kuwateua watu wa kati wenye weledi wa kutosha tosha kulingana na mahitaji ya kazi wanazotakiwa kufanya.
  5. Na tano, mtawala lazima awe na uwezo wa kusimamia utendaji wa kazi zinazofanywa na watu wa kati aliowateua.
Ni katika mazingira haya, kitendawili cha mtanz8ko wa ugavana, au tiseme mtanziko wa kiutawala, kinakuja hivi:

Katika kutekeleza majukumubyake ya kiutawala, mtawala anaweza kufuata njia mojawapo kati ya njia mbili zifuatazo, lakini hawezi kufuata njia zote mbili kwa mpigo.

  1. Ama kuwateua wasaidizi wenye weledi mkubwa kuliko yeye na hivyo kuwa katika nafasi ya kushindwa kuwasimamia ipasavyo, na hatimaye kukwamisha ujio wa matokeo yanayokusudiwa kwa sababu ya usimamizi hafifu
  2. Au kuwateua wasaidizi wenye weledi hafifu kama yeye na hivyo kuwa katika nafasi ya kuwasimamia ipasavyo, na hatimaye kukwamisha ujio matokeo yanayotakiwa kwa sababu ya weledi hafifu
Yaani, ni vigumu kwa mtawala kuwasimamia kwa ukamilifu wasaidizi wake wenye weledi mkubwa kuliko weledi wa mtawala.

Katika mazingira haya, njia pekee ya kutanzua kitendawili hiki cha mtanziko mkuu unaotengeneza njia panda ya kiutawala ni kuwa na mtawala mwenye weledi mkubwa unaokaribiana na au unaozidi weledi wa wasaidizi wake.

Ni mtawala wa aina hii pekee mwenye uwezo wa kutumia mbinu zote nne za utawala zilizotajwa hapo juu anayeweza kuisadia taasisi yake kutoboa. Mtawala mwenye maarifa haba hawezi kufua dafu.

Ni kwa sababu hii, Mbowe, Samia na Mwinyi wanakosa sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo mkuu wa taasisi kama vile chama cha siasa, kampuni, NGO na dola.

Kuhusu Mbowe hii ndio sababu amekuwa MENTOR anayekimbiwa na MENTEES wake kila kukicha.

Anawaandaa, wanafuzu, kisha anawakwepa, wanakaa benchi, kisa wanao weledi kuliko wake. Hatimaye MENTEES wanaondoka na kutafuta fursa mpya nje ya chama.

Kitendo cha Samia kuwatimua kina Januari Makamba kina sura ile ile ya mtawala kuwaogopa wasaidizi wenye weledi kuliko yeye.

Hussein mwinyi naye analo tatizo kama la Samia. Wasaidizi wake waliopinga mkakati wake wa kuuza visiwa vya Zanzibar kwa wageni aliwatimua bila kujali uzito wa hoja zao.

Lakini Lissu anaweza kuwakabili watu wa kati wenye weledi wa kutosha bila kuwaogopa.

Maana anao uwezo wa kuwafuatilia, kuwasimamia na kuwakosoa kwa hoja thabiti bila kuuma uma midomo.

Mtaani wanasema kuwa Lissu anayo"medula oblangata" iliyopevuka sawa sawa.

Katika jambo hili Lissu hana tofauti sana na hayati Magufuli, japo hawa wawili ni mahasimu katika masuala mengine.

Hivyo, namsihi Freeman Mbokwe akubali kwa moyo mweupe udhaifu wake katika mizania ya mtanziko wa ugavana (Governor's dilemma) na kwa sababu hiyo kukubali kumuunga mkono Lissu kwa faida yake Mbowe, faida ya Chadema na kwa faida ya Tanzania Pana.

Pia namwomba Tundu Lissu atamke bayana kuwa kama atafanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama atawatunza wenyeviti wastaafu akiwemo Mbowe. Kauli ya aina hii itamweka karibu zaidi na Mbowe.

Mwisho niseme kuwa nimeandika maoni haya baada ya kusoma maoni ya kina Yeriko, Mdee , Ngurumo, na wengine.

Wote naina walisahau changamoto kuu tuliyo nayo leo katika taasisi zetu ndani na nje ya serikali: providing wrong answers to the Governor's dilemma.

Mifano iko tele, lakini hapa nataja mitatu pekee:

The president must decide between entrusting monetary policy to an independent central bank able to win investor trust, or maintaining control over monetary policy so that they can stimulate economic expansion. We have so far failed badly to balance control and competence in this area.

The President
must decide between entrusting security management policy to independent security enforcement organs which are capable of winning public trust by consistently protecting human life, property, peace and order, or by maintaining hard control over security management organs through politicised statements telling incompetent security organs what to do after every now and then. We have so far failed badly to balance control and competence in this area.

Legislators must decide between giving delegated powers to government ministries, departments and agencies (MDAs) with sufficient independence that allows them to develop and apply technical capacity and expertise, on one hand, and imposing hard controls to prevent MDAs from succumbing to agency drift and agency shirking, on the other hand. We have so far failed badly to balance control and competence in this area too.

Kwa hiyo, anahitajika game changer kabla ya 2025.

Freeman Mbowe hana sifa hiyo.

Tundu Lissu, wewe ni kama Petro jembe la Yesu.

Twika hadi kilindini.

Unao uweza wa kulisaidia Taifa kutoboa!
1734856835602.png
 
Attachments

Samia Suluhu Hassan, Hussein Mwinyi na Freeman Mbowe wanafanana kwa jambo moja:

Wote hutoa jawabu lile lile kila wanapojibu kitendawili cha NJIA PANDA YA MTANZIKO WA KIUTAWALA, yaani governor's dilemma.

Kitendawili hili kiko hivi: Hakuna mtawala anayeweza kuongoza taasisi kwa kufanya kazi zote kwa mkono wake mwenyewe. Yaani direct governance.

Badala yake, ni lazima kila mtawala afanye kazi zake kupitia watu wa kati, yaani indirect governance.

Kufanya kazi kupitia mtu wa kati kwa ufanisi kunahitaji ufundi wa aina mbili.

Mosi, ni lazima kumteua mtu wa kati aliye na weledi sahihi.

Na pili, ni lazima kuwa na ufundi wa kuzisimamia kazi zinazofanywa na mtu wa kati, ambaye aghalabu anao welding kuliko msimamizi wake.

Kitendawili ni kwamba: Ni vigumu kupata usimamizi thabiti na weledi thabiti kwa mpigo, maana ni rahisi kwa ngamia kupita tundu la sindano kuliko mtawala kumdhibiti kikamilifu mtu wa kati mwenye weledi thabiti.

Katika mazingira haya, njia pekee ya kutanzua kitendawili cha mtanziko mkuu wa njiabpanda ya utawala ni kuwa na mtawala mwenye weledi unaokaribiana na weledi wa mtu wa kati.

Mtu wa kati anaweza kufanya kazi na mtawala kwa njia mojawapo kati ya njia nne zifuatazo: delegation, cooptation, orchestration na trusteeship.

Katika mbinu zote one za utawala wa mzunguko mtawala mwenye maarifa haba hawezi kuisadia taasisi yake kufikia ndoto kuu ya pamoja.

Ni kwa sababu hii, Mbowe, Samia na Mwinyi wanapoteza sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo mkuu wa taasisi kama vile chama cha siasa, kampuni, azaki na dola.

Lissu anaweza kuwakabili watu wa kati wenye ujanja haramu kuliko wao.

Hivyo, namwomba Mbowe kwa moyo mweupe akubali udhaifu wake katika mizania ya Governor's dilemma na kumuunga mkono Lissu kwa faida ya Chadema na Tanzania Pana.

Nimeandika maoni haya baada ya kusoma maoni ya kina Yeriko, Mdee , Ngurumo, na wengine.

Wote waljsahau changamoto kuu tuliyo nayo leo katika taasisi zetu: providing wrong answers to the Governor's dilemma.
Acha kina lucas mwamshamba waje hapa
 
Hivyo, namwomba Mbowe kwa moyo mweupe akubali udhaifu wake katika mizania ya Governor's dilemma na kumuunga mkono Lissu kwa faida ya Chadema na Tanzania Pana.
Mkuu Doctor Mama Amon , kwanza asante kwa the doctrine of “governor's dilemma”, naunga mkono hoja.
Naomba utupige Shule
ya delegation, cooptation, orchestration na trusteeship.

P
 
Samia Suluhu Hassan, Hussein Mwinyi na Freeman Mbowe wanafanana kwa jambo moja:

Wote hutoa jawabu lile lile kila wanapojibu kitendawili cha NJIA PANDA YA MTANZIKO WA KIUTAWALA, yaani governor's dilemma.

Kitendawili hili kiko hivi: Hakuna mtawala anayeweza kuongoza taasisi kwa kufanya kazi zote kwa mkono wake mwenyewe. Yaani direct governance.

Badala yake, ni lazima kila mtawala afanye kazi zake kupitia watu wa kati, yaani indirect governance.

Kufanya kazi kupitia mtu wa kati kwa ufanisi kunahitaji ufundi wa aina mbili.

Mosi, ni lazima kumteua mtu wa kati aliye na weledi sahihi.

Na pili, ni lazima kuwa na ufundi wa kuzisimamia kazi zinazofanywa na mtu wa kati, ambaye aghalabu anao welding kuliko msimamizi wake.

Kitendawili ni kwamba: Ni vigumu kupata usimamizi thabiti na weledi thabiti kwa mpigo, maana ni rahisi kwa ngamia kupita tundu la sindano kuliko mtawala kumdhibiti kikamilifu mtu wa kati mwenye weledi thabiti.

Katika mazingira haya, njia pekee ya kutanzua kitendawili cha mtanziko mkuu wa njiabpanda ya utawala ni kuwa na mtawala mwenye weledi unaokaribiana na weledi wa mtu wa kati.

Mtu wa kati anaweza kufanya kazi na mtawala kwa njia mojawapo kati ya njia nne zifuatazo: delegation, cooptation, orchestration na trusteeship.

Katika mbinu zote nne za utawala wa mzunguko mtawala mwenye maarifa haba hawezi kuisadia taasisi yake kufikia ndoto kuu ya pamoja.

Maana mara nyingi huteua watu wa kati walio dhaifu ili aweze kuwadhibiti, na hivyo kukosa weledi unaotakiwa ili kuleta matokeo sahihi.

Ni kwa sababu hii, Mbowe, Samia na Mwinyi wanapoteza sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo mkuu wa taasisi kama vile chama cha siasa, kampuni, azaki na dola.

Lissu anaweza kuwakabili watu wa kati wenye ujanja haramu. Katika jambo hili hana tofauti sana na hayati Magufuli, japo hawa wawili ni mahasimu katika masuala mengine.

Hivyo, namwomba Mbowe kwa moyo mweupe akubali udhaifu wake katika mizania ya Governor's dilemma na kumuunga mkono Lissu kwa faida ya Chadema na Tanzania Pana.

Nimeandika maoni haya baada ya kusoma maoni ya kina Yeriko, Mdee , Ngurumo, na wengine.

Wote walisahau changamoto kuu tuliyo nayo leo katika taasisi zetu: providing wrong answers to the Governor's dilemma.
Akili kubwa! Bandiko safi sana lililojaa weledi wenye usioegemea upande.
 
TISS wenyewe wanajua kinachoendelea kwenye vijiwe vya ki digital wanajitoa ufahamu tu

Kwenye popular vote Lissu hata agombee na wagombea wote wa CCM na upinzani atafikisha 50+ votes

Watu wa Leo sio wale wa miaka ya 80!!
 
Samia Suluhu Hassan, Hussein Mwinyi na Freeman Mbowe wanafanana kwa jambo moja:

Wote hutoa jawabu lile lile kila wanapojibu kitendawili cha NJIA PANDA YA MTANZIKO WA KIUTAWALA, yaani governor's dilemma.

Kitendawili hili kiko hivi: Hakuna mtawala anayeweza kuongoza taasisi kwa kufanya kazi zote kwa mkono wake mwenyewe. Yaani direct governance.

Badala yake, ni lazima kila mtawala afanye kazi zake kupitia watu wa kati, yaani indirect governance.

Kufanya kazi kupitia mtu wa kati kwa ufanisi kunahitaji ufundi wa aina mbili.

Mosi, ni lazima kumteua mtu wa kati aliye na weledi sahihi.

Na pili, ni lazima kuwa na ufundi wa kuzisimamia kazi zinazofanywa na mtu wa kati, ambaye aghalabu anao welding kuliko msimamizi wake.

Kitendawili ni kwamba: Ni vigumu kupata usimamizi thabiti na weledi thabiti kwa mpigo, maana ni rahisi kwa ngamia kupita tundu la sindano kuliko mtawala kumdhibiti kikamilifu mtu wa kati mwenye weledi thabiti.

Katika mazingira haya, njia pekee ya kutanzua kitendawili cha mtanziko mkuu wa njiabpanda ya utawala ni kuwa na mtawala mwenye weledi unaokaribiana na weledi wa mtu wa kati.

Mtu wa kati anaweza kufanya kazi na mtawala kwa njia mojawapo kati ya njia nne zifuatazo: delegation, cooptation, orchestration na trusteeship.

Katika mbinu zote nne za utawala wa mzunguko mtawala mwenye maarifa haba hawezi kuisadia taasisi yake kufikia ndoto kuu ya pamoja.

Maana mara nyingi huteua watu wa kati walio dhaifu ili aweze kuwadhibiti, na hivyo kukosa weledi unaotakiwa ili kuleta matokeo sahihi.

Ni kwa sababu hii, Mbowe, Samia na Mwinyi wanapoteza sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo mkuu wa taasisi kama vile chama cha siasa, kampuni, azaki na dola.

Lissu anaweza kuwakabili watu wa kati wenye ujanja haramu. Katika jambo hili hana tofauti sana na hayati Magufuli, japo hawa wawili ni mahasimu katika masuala mengine.

Hivyo, namwomba Mbowe kwa moyo mweupe akubali udhaifu wake katika mizania ya Governor's dilemma na kumuunga mkono Lissu kwa faida ya Chadema na Tanzania Pana.

Nimeandika maoni haya baada ya kusoma maoni ya kina Yeriko, Mdee , Ngurumo, na wengine.

Wote walisahau changamoto kuu tuliyo nayo leo katika taasisi zetu: providing wrong answers to the Governor's dilemma.
🙋‍♂️✍️🎯👌👍👊🤝🙏
 
Back
Top Bottom