Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
katika nchi za wenzetu kama marekani, mnaweza kugombea nafasi moja lakini baada ya Uchaguzi, wagombea wote wanaheshimiana, aliyeshindwa anamtambua aliyeshinda na aliyeshinda vile vile anamheshimu aliyeshindwa. Ndiyo maana Obama alimheshimu mama klintoni na kumpa cheo kikubwa sana serikalini kwake. Walifanya hivyo pia marais kama Kennedy aliyemteua Johnson kuwa makamu wake, na Rais Reagan alimteua George Bush (sr) kuwa makamu wake.
Tatizo la kwetu, mkigombea wawili, baada uchaguzi yule aliyeshinda anafanya kila liwezekanalo kummaliza mpinzani wake kisiasa, yaani uchaguzi unageuka kuwa ugomvi wa kudumu. Hapo ndipo ninapoona tatizo kwa CHADEMA