Nyumbu
Senior Member
- May 22, 2008
- 141
- 2
Zitto ataweza?
Maswali Magumu: Na Ansbert Ngurumo
Source: Tanzania Daima
NIMEFARIJIKA kusikia na kusoma kwamba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameamua kugombea uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa shinikizo la wapambe, si kwa hiari yake; kwani maswali ya awali niliyokuwa najiuliza niliposikia anagombea uenyekiti, si kama ana weza au la.
Nilitaka kujua Zitto ana haraka gani, na kama anagombea kwa uamuzi wake binafsi au kwa shinikizo la watu wengine; na kama ni kweli, ni kina nani.
Nilitaka kujua pia kama anajua athari ya uamuzi wake huo kwa muda mfupi na mrefu kwenye chama chake na yeye binafsi.
Vile vile, nilitaka kujua kama chama chake kilichomtambua, kikamlea na kumfunda kisiasa kimemwandaa kugombea nafasi hiyo au anakwenda kama mgombea binafsi ndani ya chama.
Lakini kwa sababu ameshajibu swali moja hapo juu, na kwa kuwa bado yapo maswali mengi yanaulizwa juu yake, hasa kwa kuwa ameibua mjadala kitaifa, nimeona leo niandike makala hii kumlinda na kumsaidia kama mdogo wangu, msomi mwenzangu, mwanaharakati mwenzangu, kijana mwenzangu na rafiki yangu; na kwa kuwa mimi na Zitto tuna mengi tunayokubaliana na kutofautiana.
Zitto amethubutu kufanya kile ambacho vijana wengi wa umri wake wanaogopa kufanya. Anajaribu kuutumia umaarufu wake karama yake na mvuto wake wa kisiasa vikiwa bado juu ili asonge mbele na kujijenga kisiasa.
Tumzuie? Tumruhusu? Tumpinge? Tumuunge mkono? Tumshabikie? Tumshauri au tumwache? Tumjali au tumpuuze? Je, tuna uwezo wa kufanya lolote miongoni mwa hayo hapo juu?
Jambo moja liko wazi.
Kila anayemjadili Zitto leo, si tu kwamba anamjadili Mbunge wa CHADEMA, bali anamjadili pia mbunge wa taifa.
Uamuzi aliochukua na athari au hatima yake vina mwangwi mkubwa kitaifa.
Kwa sababu hiyo, hatuwezi kumpuuza Zitto. Na mimi nitajaribu kufanya nitakaloweza katika hayo niliyoyataja hapo juu.
Bahati nzuri kuna walionitangulia. Rafiki yangu mwingine, ambaye pia ni rafiki ya Zitto, Absalom Kibanda, katika safu yake ya Tuendako, wiki hii, amemsema sana mbunge huyo katika kile alichokiita anguko la Zitto.
Mimi nitajadili anguko la CHADEMA. Lakini kabla ya kwenda mbali, hatuna budi kujiuliza: Nani angependa na kushabikia anguko la Zitto au la CHADEMA? Kwa manufaa gani? Je, kuna watu wanaomwandalia Zitto na kumsindikiza katika anguko lake au la chama chake? Je, anguko la Zitto ni kuupata au kuukosa uenyekiti wa CHADEMA? Je, Zitto kuupata au kuukosa uenyekiti wa CHADEMA ni heri kwa Tanzania?
Maswali ni mengi, lakini lipo hili ambalo Kibanda amelidokeza katika makala yake, akalichochea na kulifafanua zaidi katika barua pepe kwa umma; la kusema Zitto anatumiwa na CCM bila kujua ili kuivuruga na kuibomoa CHADEMA, mithili ya NCCR-Mageuzi na CUF.
Nataka kumtetea Zitto kidogo. Naamini kwamba hatumiwi na CCM bila kujua. Kwangu mimi, Zitto ameshavuka viwango vya kutumiwa bila kujua. Zitto ni mjanja vya kutosha, kiasi kwamba akiamua kutumika, atafanya hivyo kwa hiari yake.
Kwa vyovyote vile, Zitto anajua analofanya. Hivyo, wanaomlaumu na wanaomtetea wasizunguke mbuyu; waseme kile wanachokusudia kusema. Wamwambie.
Kama wanakerwa na vikao vya siri anavyofanya na vigogo kadhaa wa CCM, waseme; na watutajie majina. Kama ni Joseph Sinde Warioba au Dk. Ahmed Salim au Rostam Azizi au Edward Lowassa au Rais Jakaya Kikwete au Lawrence Masha au William Ngeleja; waseme wazi.
Kilicho wazi ni kwamba Zitto anajaribu kujenga himaya yake kisiasa ndani na nje ya CHADEMA. Wakati mwingine anajisikia fahari kuzungukwa na kushauriwa na vigogo kama hao.
Katika umri wake mdogo, anaona heshima na fahari ya pekee kupata joto na ushauri wa vigogo kama hao, hata kama baadhi yao hawana majina mazuri kisiasa na kijamii. Kwake, kisiasa, anaona kama anawekeza kwa malengo ya muda mrefu.
Maana kinachozungumzwa sasa ni kwamba mojawapo ya ajenda za Zitto kuutaka uenyekiti ni ahadi aliyopewa na baadhi ya vigogo wa CCM kwamba wanatamani kujiengua na kujiunga na CHADEMA iwapo tu, ataweza kumwangusha Freeman Mbowe katika nafasi ya uenyekiti.
Uongo wanaotumia ni kwamba wakishajimega kutoka CCM wataiwezesha CHADEMA kupata wabunge wengi mwaka 2010, na hata kuipa uwezekano wa kuwa na waziri mkuu kutoka chama cha upinzani.
Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.
Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.
Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.
Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.
Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyanganyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.
Tunajua mbinu walizokuwa wanatumia, na tumeshuhudia wakifurukuta tangu mwaka 2007; lakini wameshindwa kwa sababu CHADEMA imekuwa na watu shupavu na mahiri, huku ufisadi wa wanamtandao ukichangia kuwamaliza makabakaba na kusaidia harakati za kuwabana.
Zitto amekuwa mmoja wa mashujaa katika vita dhidi ya ufisadi, lakini akiwa mkweli atatuambia bila kificho kuwa watu wale wale waliokuja kufahamika baadaye kuwa mafisadi, ndio waliokuwa wanaomba CHADEMA iwape nafasi walipokuwa hawajaipata CCM.
Kwa hiyo, kupata kwao nafasi katika CCM ndio ulikuwa wokovu wa CHADEMA, maana leo hii ndiyo ingekuwa inashambuliwa kwa ufisadi kama wanamtandao wangejiunga nayo, hata kama wasingefaulu kushika madaraka.
Ndiyo maana wengi wetu tunatarajia kwamba Zitto angepaswa kuwa mwangalifu sana anapoletewa masharti ya namna hii na vigogo wa CCM wanaomuahidi kujiunga CHADEMA kwa kishindo iwapo atamuondoa Mbowe.
Hili ni sharti lenye hila; na woga wao kwa Mbowe unapaswa utumiwe kama nguvu ya CHADEMA dhidi ya CCM, na sifa ya ziada ya kiuongozi ya Mbowe.
Wana CCM hawawezi kuwachagulia wana CHADEMA kiongozi bora. Na kama kweli wanamtuma Zitto (ingawa yeye amekanusha) wanajua wanachokitaka.
Pili, Zitto na wapambe wake wanapaswa wajue kuwa nguvu na uhai wa CHADEMA haviwezi kutoka CCM. Na kama ikitokea hivyo, vigogo wa CCM wakameguka na kujiunga CHADEMA, hilo ndilo litakuwa anguko la kwanza la CHADEMA.
Sababu ni moja. Baadhi ya hao wanaoionea huruma CHADEMA kwa staili hiyo, ni makapi ya kisiasa huko waliko. Siamini kama ni jambo jema kutarajia kuijenga CHADEMA kwa kutumia makapi ya CCM.
Wanaotaka kuijenga CHADEMA bora wawekeze katika damu mpya, kizazi kipya kisicho na mawaa ya ufisadi.
Kazi ile ile iliyofanyika kuwatambua kina Zitto, John Mnyika, John Mrema, Halima Mdee, Mhonga Ruhwanya na vijana wengine wengi wanaoendelea kuchangamsha siasa za CHADEMA na kuchochea harakati, iendelee kufanyika kuendeleza kazi nzuri iliyokwishaanza chini ya uongozi wa sasa wa kina Mbowe, Dk. Willibrod Slaa na Zitto mwenyewe.
Kwa hiyo, kama makundi haya ya wana CCM yanamwaminisha Zitto kwamba njia pekee ya kuijenga CHADEMA ni kumwondoa Mbowe, kumweka Zitto na kuwaruhusu wao kujiunga, Watanzania wanaoona mbali watamuonya yeye na watu wake kwamba sasa wanavuka mipaka ya demokrasia, wanajiingiza katika uhujumu, usaliti na uhaini ambao unamfanya Zitto sasa aanze kuwashambulia viongozi wenzake kwa maamuzi yaliyofanyika ndani ya vikao halali (kwa mfano kuhusu kuwasimamisha watu uanachama au kuwafukuza kabisa), wakati naye alishiriki, tena kama kiongozi mwandamizi wa chama.
Na jambo hili linazua hoja kwamba labda akifanikiwa kuwa mwenyekiti hatachukua hatua zozote dhidi ya wazembe, wasaliti, mafisadi na watovu wa nidhamu ndani ya chama.
Ikumbukwe kuwa ni vigumu Zitto kukiri kuwa anatumiwa na CCM. Inawezekana watu wanamuonea tu kwa sababu ya hisia, lakini ninavyokumbuka mimi tuhuma hizi zimetokana na mambo kadhaa.
CCM wanaogopa nguvu ya CHADEMA; na wanatafuta pa kupumulia, baada ya kuthubutu na kushindwa kwa miaka mitatu mfululizo.
Wanadhani wakifanikiwa kuwapambanisha vigogo wa chama unaweza kuwa mwanya wa kujenga ufa ndani ya chama na wao kupona.
Wanahofia umaarufu wa Zitto unaweza kuwadhuru wasipokuwa karibu naye. Njia rahisi wanayodhani inaweza kumlainisha ni kukiri umaarufu wake, kuutambua na kumfanya ajisahau, alewe umaarufu wake, wamtumie.
Ndiyo maana Zitto alipojisahau akaanza kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans, akidhani umaarufu wake ungeweza kubadili mjadala wa kitaifa na upepo wa kisiasa, wapambanaji wenzake walimsikitikia sana, na tuhuma za waziwazi zikaanza kurushwa dhidi yake kwamba kuna waliomharibu.
Hata leo, kauli yake kuhusu Dowans imemjeruhi sana kisiasa, hasa inapochangiwa na kile wachunguzi wanachokiita vikao vyake vya siri na wabaya wa CHADEMA. Na kama baadhi yao ndio wanaojitokeza leo kumshabikia na kumpongeza hadharani kwa hiki anachofanya, ni vigumu kuzuia hisia za wananchi dhidi yake. Itamchukua muda mrefu kujisafisha.
Na katika siku za hivi karibuni, Zitto amesikika akizungumza katika Radio Sauti ya Ujerumani akidai kwamba tofauti ya msingi kati yake na Mbowe katika kinyanganyiro cha uenyekiti ni kwamba Mbowe ni bepari, Zitto ni mjamaa!
Lakini Zitto anajua kuliko wengi wetu kuwa kiitikadi CHADEMA haijawahi kuwa chama cha kijamaa.
Anajua kuwa watu pekee wanaojidai kuwa na itikadi ya ujamaa hapa nchini ni CCM, ingawa nao wanaishi kwa siasa za ubepari wenye ulemavu.
Katiba ya CHADEMA, ambayo Zitto ameshiriki kuiandika upya mwaka 2006, akiwa mbunge na kiongozi mwandamizi, inaeleza vema itikadi ya chama chake. Miaka mitatu baadaye, Zitto amegeuka na kuwa mjamaa katika chama cha kibepari? Lipi limemsibu Zitto?
Zaidi ya hayo, Zitto amepata bahati ya kukosolewa na vyombo vya habari visivyomilikuwa na CCM, huku akisifiwa na kupongezwa na kupewa moyo na vyombo vya CCM au vinavyomilikiwa na makada wa CCM.
Ikumbukwe pia katika migogoro mingine iliyopita ya uongozi ndani ya CHADEMA, ya kweli na ya kupandikizwa, vyombo hivyo hivyo vilikuwa vinawaunga mkono na kuwashabikia waliojitokeza kuisumbua CHADEMA au Mbowe.
Hii si neema ya kisiasa kwa Zitto. Wana CCM wanamsifu makusudi ili kumchafulia jina mbele ya wana CHADEMA na wananchi wengine waliomwamini kwa muda mrefu, ili baada ya muda naye awe kapi la kisiasa kama wao.
Sisi wengine tungependa kumzuia asiende huko kama atasikiliza. Vinginevyo, iwapo atakifikisha chama chake katika unyonge, udhalili na hatimaye kifo kama kilichowakuta NCCR-Mageuzi, au kama hataki kujikumbusha jinsi CCM ilivyoisambaratisha CUF, anaweza kuchagua kutumia ubishi na umaarufu kukuza haiba yake kisiasa na kuua taswira ya taasisi iliyomlea na kumkuza.
Nimekuwa nafuatilia wanasiasa wanaompongeza. Ni vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na TLP; vile vile ambavyo vimeshughulikiwa na CCM, na baadaye vimekuwa katika ushindani na wivu dhidi ya CHADEMA, ambayo inakua, vyenyewe vinafifia, kiasi cha kuathiri hata ushirikiano wa kisiasa uliokuwa umeanzishwa.
Hizi ndizo pongezi anazotafuta Zitto? Anazihitaji? Anapochanganya hizi na za CCM, anapata jawabu gani?
Kwa elimu na uzeofu wake, Zitto anapaswa kuelewa kwa nini watu wanapigia kelele uamuzi wake wa kugombea uenyekiti sasa, katika mazingira haya, na kwa staili aliyoamua kutumia.
Watanzania hawako tayari kumsamehe binadamu yeyote atakayeshiriki kwa kujituma au kutumiwa kudhoofisha nguvu iliyopo sasa ya CHADEMA Bara na CUF Visiwani. Na kama yupo, asiwe Zitto.
Ni haki yake kugombea na kuongoza. Lakini lazima atumie busara inayomlinda yeye na taasisi yake. Nyota yake kisiasa bado ni changa na inawaka. Hana sababu ya kujiingiza katika jitihada za kuizima mapema hivi.
CHADEMA inaweza kumwandaa Zitto kuwa kiongozi mkubwa kitaifa baadaye, iwapo atakubali kufanya kazi na viongozi wenzake na kujijenga pole pole.
Naamini kwamba hata Mbowe asingefika hapo alipo kama angekurupuka au kama angegombea kwa mbinu zinazotiliwa shaka, na katika mazingira kama haya ya sasa. Tungemshauri kama tunavyofanya kwa Zitto leo.
Hata hivyo, ninapotafakari mbinu alizotumia Zitto, nafika mahali nadhani Zitto hajadhamiria kushinda, bali anataka kumtikisa Mbowe na chama, kuleta msisimko wa kitaifa kuhusu uchaguzi ndani ya CHADEMA, kujenga hisia na ufuasi wa hapo baadaye, ili atakapokuwa amefuzu, na chama kiko tayari, iwe rahisi kwake kupitishwa, kugombea na kushinda.
Kwa sasa naona anatumia njia ile ile iliyotumiwa na Jakaya Kikwete kuusaka urais mwaka 1995, ambao aliupata baada ya miaka 10 ya kujijenga, kujitangaza na kukua kidogo.
Tuombe tu kwamba umaarufu uambatane na uwezo; maana kama alivyosema Kibanda, ya Augustine Mrema na Kikwete yametufundisha ukweli kwamba kuna tofauti kati ya kutoa hotuba nzuri, kuhamasisha umma na kuwa kiongozi.
Navijua CHADEMA na CCM; nawajua vizuri Mbowe na Zitto. Najua uwezo na udhaifu wao, na sababu ya CCM kuiogopa CHADEMA ya Mbowe.
Kama CCM wamehangaika kwa miaka mitatu mfululizo wakashindwa, na kama wataweza kuibomoa CHADEMA hii kabla ya Uchaguzi Mkuu 2010, ibilisi awape nini!
Si lazima wamwangushe Zitto, maana anaweza kujikwaa, au hata akaanguka na kusimama pale pale alipo au akasimamia pengine. Lakini iwapo CHADEMA itaanguka haitaamka; na itatuchukua muda mrefu sana kupata nguvu nyingine na uwanja wa mapambano; walau si kabla ya 2010.
Wasioona anguko la CHADEMA katika mpambano wa Zitto na Mbowe, waendelee kutafakari, na wajiulize sababu za ushabiki wa wazi wa wabaya wa CHADEMA katika pongezi wanazompa Zitto.
Natambua kuwa Zitto amefanya kazi nzuri bungeni na majukwaani. Aendelee kuifanya, maana anaiweza, na taifa linamhitaji kuelekea 2015 akiwa na viongozi wenzake waandamizi wa CHADEMA.