wengi tuwagumu kuombana radhi...
Inaonekana Zitto akuwasiliana na Freeman kabla ya kuchukua form, mawasiliano kama haya hayaitajiki CCM kutokana na ukubwa wake, lakini kwa chama kama CHADEMA ambacho mihimili yake ni Freeman, Slaa na Zitto ni lazima wawasiliane kabla ya hayo maamuzi. Ndiyo ni demokrasia lakini inaonekana kuna vita ya chini chini kati ya Freeman na Zitto..
Usemi wa Zitto kwamba Freeman arudishe form ili kukinusuru chama ni dhairi kwamba hakubaliani na mwenyekiti wake na kunakurukupushani kati ya hao wawili.
Sidhani kama Kibanda angeweza kumshambulia Zitto bila kujua kuwa kuna mvutano kati ya Zitto na Freeman.....
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.
Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.
Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.
Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...
Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.
Katika hili, mmechemsha!
Basi na Freeman achomoe jina!I would be happy if Dr. Kitila kugombea kuliko figure hizi 2 ambazo zinaonyesha something is wrong na hata kama wakinyamaza but wenye nao walishaona siku mingi tu. Ila mkae mje na mbinu mpya maana akina Makamba wanagonga glass za wine.
huyu mh Zitto kama msanii flani niliwahi kusoma kuwa hatagombea ubunge tena, lkn bdae akageuka, na inavyo onekana kwa hatua aliyofikia ya kujitoa naanza kupata hofu labda alitaka kuuza chama kama angeshinda ila alipoona amestukiwa ameamua kujitoa. Ila hofu yangu wasije waka mCHACHA WANGWE kama atakuwa hana msimamo