Wakuu zangu,
Nimesoma baadhi ya hoja humu ndani inaonyesha wazi kuna utata kidogo ktk kuelewa huu uchaguzi wa Chadema hasa ktk nafasi hiyo ya Mwenyekiti..
Tusichanganya issue wakuu zangu kwani yaonyesha wazi kuna watu wanafikiria kwamba ukiwa mwenyekiti wa chama basi ndio unapita kama mgombea wa chama ktk kiti cha Urais mwaka 2010..Sidhani kama utaratibu wa Chadema unasema kuwa Mtu anayeshinda kuwa mwenyekiti wa chama ndiye atakuwa mgombea kiti cha Urais 2010. Ila kinachogombea hapa ni mwenyekiti, Kiongozi wa chama..Kiongozi ambaye anaweza au anatakiwa kuwa na sifa tofauti kabisa na mgombea kiti cha Urais.
Hivyo Zitto anapochogombea hapa ni kuongoza chama na sii maandalizi ya kugombea kiti cha urais 2010. Na kuna sifa zinazoweza kum qualify mtu kugombea nafasi hiyo ya uongozi wa chama. Kuna baadhi ya vitu ambavyo kusema kweli vimetushangaza wengi ni pamoja na Utaratibu wa uchaguzi ktk chama hiki. Mara nyingi kama sii zote majina ya wagombea nafasi ya Mwenyekiti ktk chama hupendekezwa na wajumbe wa mkutano mkuu, kisha zikapigwa kura mshindi akajulikana pale pale ktk mkutano na sii swala la kila mwanachama kuchukua form kugombea kuongoza chama.
Power to the People, inaanza na mapendekezo ya wanachama na sii mtu kufikiria anaweza kuongoza chama, hivyo apewe uhuru na haki ya kugombea.
Pili, Swala la chama Chadema kumweka kitimoto Zitto ikiwa utaratibu wenyewe unaruhusu mtu kuchukua form, ni kithibitisho kamili cha Mapungufu ya chama hicho ktk kuthamini wanachama wake. Aidha Zitto hakutakiwa kushindana au haikuleta picha nzuri ndani ya chama swala hili limekibomoa chama zaidi kwa kuonyesha wazi kwamba chama hiki kina wenyewe na hasa kwa Wadanganyika itakuwa picha mbaya zaidi pale Zitto anapozidi kuongea maneno dhidi ya matokeo..
Ikumbukwe tu hakuna chama sdduniani kisichokuwa na wenyewe! hakuna ila wenyewe ni wale wenye kuamini itikadi na mafundisho ya ya mrengo husika. Na kati baina ya waumini hao wapo wenye Elimu, Hekima na Busara ambazo zinaambatana na uzoefu ktk kufafanua na kufuata kanuni, taratibu, maadili, miiko na kadhalika iwe ktk kusimamia vikao, kuwakilishi falsafa, au kupatanishi watu kwa kutumia misingi ilyiojengwa na mrengo husika.
Tatu swali langu linakuja kwamba - Does Zitto has what ita takes kuongoza chama?..kusema kweli binafsi sidhani, so was Mbowe sidhani kama alikuwa na elimu, busara na Uwezo wa kuongoza chama ila wanaweza wote kuwa wagombea wazuri kuwakilisha chama Chadema ktk kiti cha Urais. na hapa ndipo CCM inapotufunga magoli, JK ni mwekeykiti wa chama lakini kabla hajachukua kiti hicho alipitia darsa zito, yaani alipikwa kuelewa nini chama chake kinasimamia hata iwe ni Ufisadi ndani yake au Umafia ni lazima kiognozi wa chombo hiki ale yamini, (Kiapo) kwamba hatasaliti mawazo na fikra za zilizotangulia kwa kujenga agano jipya ndani ya chama..
Mwisho, inasikitisha zaidi kusikia Zitto kajitoa kugombea kiti hiki baada ya mfutano mkubwa baina yake na Uongozi wa Chadema. Ilikuwa ni haki ya Zitto kuchukua form kwa sababu mfumo na utaratibu wa uchaguzi ndani ya Chadema ni mbovu. Hivyo ilikuwa ni jukumu la chama kukubali Zitto aendelee kugombea, hata kama matokeo yapangwe Zitto akaridhia kushindwa kama ilivyotokea Uchaguzi wa kwanza wa TANU kati ya Mwalimu Nyerere na AbdulWaheed. Lakini hii habari ya Zitto kujiondoa na kudai anafanya hivyo KUKIOKOA CHAMA.
Hakika hakiokoi chama ila inanikumbusha kina Lowassa na scandal za Richmond ati kujiuzuru kwao ni kukiokoa chama. Swala hili halikuakiwa kufikia hapa lilipofikia na inaonyesha wazi kuna pengo kubwa la fikra ndani ya uongozi wa Chadema kiasi kwamba swala dogo sana la Ziutto limeweza kutingisha chama..
Zitto hakufanya makosa yoyote zaidi ya kusema sema ovyo kujibu kesi isiyokuwepo. Na Viongozi na Chadema hasa hilo baraza la wazee limeonyesha wazi jinsi lisivyokuwa na hekima wala busara kuchukua na kutangaza upinzani wa Zitto kama vile mhusika yaani Zitto ni mnafiki, muasi na mtoto mpotevu wakati sheria ya chama inamruhusu mtu yeyote kugombea kiti hicho..