Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Kwa kitendo hiki sijamwelewa Zito hata kidogo. Nilidhani alipoamua kugombea alifanya hivyo kwa maslahi ya chama. Sasa amejitoa, anadai kujitoa huko ndiko maslahi ya chama. Kumbe basi alipotaka kugombea ilikuwa iwe kwa maslahi ya nani?
 
Maslahi ya mafisadi, nawashikaji zake....anaokula nao mbuzi.
 
Mzee Mtei alipoacha uenyekiti aliyefwatia ni Mzee BOB MAKANI. Uongo ni mbaya sana....jenga hoja zako kwenye facts mkuu.

Mkuu,
Naona wewe unatudanganya mchana kweupe au hujui kinachosemwa hapa na hujui siasa kwa ujumla. Bob Makani ...... te teteeee. Hata Mbowe mwenyewe hapo ni picha. Siku Mtei akiwa hawezi fanya kitu katika dunia hii, basi hapo ataibuka kiongozi MPYA wa Chadema. Wengine wote hapo wapo/walikuwepo ila mvuta kamba ni Mtei.
 
Tatizo ni kwamba, ikiwa Zitto atajitoa na hata wakimfujuza Chamani atarudi kwenye profesional yake na Mbowe atarudi wapi?

Mbowe ni mfanyabiashara na Zitto ni mwanauchumi mzuri bila shaka ataajiliwa na Mbowe katika biashara zake azisimamie vyema.
 
Hii issue ya Mhe. Zitto inaacha maswali mengi bila majibu. Katika ile thread ya makala ya Kibanda, nilisema, Zitto amechukua fomu kugombea ili kutesti zali na kujipatia sababu ya heshima ya kutimkia CCM.Tangu alipodai hagombei, nilianza kupata mashaka, baadae akaamua atagombea nilijiuliza maswali bila majibu.Niliposikia anagombea uenyekiti kwa stail aliyotumia, nilijua haweza sikia la muadhini wala la mnadi swala, ni mbele kwa mbele..kumbe.Sasa Zitto ameshadhibitisha Chedema ina wenywew na wenyewe ndio wale wale, kinachofuatia atasusa nafasi zoter atakazopewa, baada ya bunge kuvujwa, jamaa nae ndio hapo hapo atakapobainisha msimamo wake ni kuelekea kule kule ambako tayari ameshaahidiwa uwaziri.Sisi yet macho, tusubiri tuone.

Pasco,

Ni muhimu mno uwe na uhakika kabla ya kutoa accusations nzito kama hizo za kwamba Zitto atahamia CCM. Asipohamia sijui utamwomba msamaha mara ngapi?

Nafikiri ifike mahali tutofautiane kwa hoja; hizi dalili za kila aliye na mawazo tofauti basi anatumiwa au anataka kutimkia CCM mimi nafikiri hazitasaidia kujenga demokrasia ndani ya hivi vyama.

Kumbukeni hizi accusations zilielekezwa kwa Wangwe pia pale alipoonyesha nia kwamba huenda angempinga Mbowe.

Hivi kwanini tunaogopa sana mabadiliko? Kwanini tusiamini busara za wananchi au wanachama kufanya maamuzi ya maana?
 
Hiko chama cha wakaskazi wewe Zitto tafuta mkate wako wa kila siku tuu usijaribu kushindana nao wasije wakakuwangwe bure!Bado tunakuhitaji sana kijana katika kujenga taifa hili na haswa kuhusu ahadi yako ya kukiacha chama hicho na kurudi nyumbani hapo mwakani.
Kwa hiyo anatafuta gia ya kupandia ili kurudi nyumbani?😀😱
 
Duuu. Nachoka sana sometimes. Eneway, na burudani iendelee.

By the way kuna watu-maarufu sijawaona hapa. Pse come we need you here as well especially at this time.
 
Wakuu zangu,
Nimesoma baadhi ya hoja humu ndani inaonyesha wazi kuna utata kidogo ktk kuelewa huu uchaguzi wa Chadema hasa ktk nafasi hiyo ya Mwenyekiti..

Tusichanganya issue wakuu zangu kwani yaonyesha wazi kuna watu wanafikiria kwamba ukiwa mwenyekiti wa chama basi ndio unapita kama mgombea wa chama ktk kiti cha Urais mwaka 2010..Sidhani kama utaratibu wa Chadema unasema kuwa Mtu anayeshinda kuwa mwenyekiti wa chama ndiye atakuwa mgombea kiti cha Urais 2010. Ila kinachogombea hapa ni mwenyekiti, Kiongozi wa chama..Kiongozi ambaye anaweza au anatakiwa kuwa na sifa tofauti kabisa na mgombea kiti cha Urais.

Hivyo Zitto anapochogombea hapa ni kuongoza chama na sii maandalizi ya kugombea kiti cha urais 2010. Na kuna sifa zinazoweza kum qualify mtu kugombea nafasi hiyo ya uongozi wa chama. Kuna baadhi ya vitu ambavyo kusema kweli vimetushangaza wengi ni pamoja na Utaratibu wa uchaguzi ktk chama hiki. Mara nyingi kama sii zote majina ya wagombea nafasi ya Mwenyekiti ktk chama hupendekezwa na wajumbe wa mkutano mkuu, kisha zikapigwa kura mshindi akajulikana pale pale ktk mkutano na sii swala la kila mwanachama kuchukua form kugombea kuongoza chama.
Power to the People, inaanza na mapendekezo ya wanachama na sii mtu kufikiria anaweza kuongoza chama, hivyo apewe uhuru na haki ya kugombea.

Pili, Swala la chama Chadema kumweka kitimoto Zitto ikiwa utaratibu wenyewe unaruhusu mtu kuchukua form, ni kithibitisho kamili cha Mapungufu ya chama hicho ktk kuthamini wanachama wake. Aidha Zitto hakutakiwa kushindana au haikuleta picha nzuri ndani ya chama swala hili limekibomoa chama zaidi kwa kuonyesha wazi kwamba chama hiki kina wenyewe na hasa kwa Wadanganyika itakuwa picha mbaya zaidi pale Zitto anapozidi kuongea maneno dhidi ya matokeo..

Ikumbukwe tu hakuna chama wala chombo hapa duniani kisichokuwa na wenyewe! hakuna.. Ilaa wenyewe ni wale wenye kuamini itikadi na mafundisho ya mrengo unaohusiana. Na kati baina ya waumini hao wapo wenye Elimu, Hekima na Busara ambazo zinaambatana na uzoefu ktk kufafanua na kufuata kanuni, taratibu, maadili, miiko na kadhalika ya imani hiyo iwe ktk kusimamia vikao, kuwakilishi falsafa, au kupatanishi watu kwa kutumia misingi ilyiojengwa na mrengo husika. Hawa watu ndio hutakiwa kuongoza imani hiyo na sii kuongoza watu.. Mwenyekiti wa chama huongoza imani ya itikadi ya chama kwa watu na Rais ni kiongozi anayeongoza watu kwa kutumia itikadi husika..

Tatu swali langu linakuja kwamba - Does Zitto has what ita takes kuongoza chama?..kusema kweli binafsi sidhani, so was Mbowe sidhani kama alikuwa na elimu, busara na Uwezo wa kuongoza chama ila wanaweza wote kuwa wagombea wazuri kuwakilisha chama Chadema ktk kiti cha Urais. na hapa ndipo CCM inapotufunga magoli, JK ni mwekeykiti wa chama lakini kabla hajachukua kiti hicho alipitia darsa zito, yaani alipikwa kuelewa nini chama chake kinasimamia hata iwe ni Ufisadi ndani yake au Umafia ni lazima kiognozi wa chombo hiki ale yamini, (Kiapo) kwamba hatasaliti mawazo na fikra za zilizotangulia kwa kujenga agano jipya ndani ya chama..

Mwisho, inasikitisha zaidi kusikia Zitto kajitoa kugombea kiti hiki baada ya mfutano mkubwa baina yake na Uongozi wa Chadema. Ilikuwa ni haki ya Zitto kuchukua form kwa sababu mfumo na utaratibu wa uchaguzi ndani ya Chadema ni mbovu. Hivyo ilikuwa ni jukumu la chama kukubali Zitto aendelee kugombea, hata kama matokeo yapangwe Zitto akaridhia kushindwa kama ilivyotokea Uchaguzi wa kwanza wa TANU kati ya Mwalimu Nyerere na AbdulWaheed. Lakini hii habari ya Zitto kujiondoa na kudai anafanya hivyo KUKIOKOA CHAMA.

Hakika hakiokoi chama ila inanikumbusha kina Lowassa na scandal za Richmond ati kujiuzuru kwao ni kukiokoa chama. Swala hili halikuakiwa kufikia hapa lilipofikia na inaonyesha wazi kuna pengo kubwa la fikra ndani ya uongozi wa Chadema kiasi kwamba swala dogo sana la Ziutto limeweza kutingisha chama..
Zitto hakufanya makosa yoyote zaidi ya kusema sema ovyo kujibu kesi isiyokuwepo. Na Viongozi na Chadema hasa hilo baraza la wazee limeonyesha wazi jinsi lisivyokuwa na hekima wala busara kuchukua na kutangaza upinzani wa Zitto kama vile mhusika yaani Zitto ni mnafiki, muasi na mtoto mpotevu wakati sheria ya chama inamruhusu mtu yeyote kugombea kiti hicho..
 
Last edited:
Wakuu zangu,
Nimesoma baadhi ya hoja humu ndani inaonyesha wazi kuna utata kidogo ktk kuelewa huu uchaguzi wa Chadema hasa ktk nafasi hiyo ya Mwenyekiti..

Tusichanganya issue wakuu zangu kwani yaonyesha wazi kuna watu wanafikiria kwamba ukiwa mwenyekiti wa chama basi ndio unapita kama mgombea wa chama ktk kiti cha Urais mwaka 2010..Sidhani kama utaratibu wa Chadema unasema kuwa Mtu anayeshinda kuwa mwenyekiti wa chama ndiye atakuwa mgombea kiti cha Urais 2010. Ila kinachogombea hapa ni mwenyekiti, Kiongozi wa chama..Kiongozi ambaye anaweza au anatakiwa kuwa na sifa tofauti kabisa na mgombea kiti cha Urais.

Hivyo Zitto anapochogombea hapa ni kuongoza chama na sii maandalizi ya kugombea kiti cha urais 2010. Na kuna sifa zinazoweza kum qualify mtu kugombea nafasi hiyo ya uongozi wa chama. Kuna baadhi ya vitu ambavyo kusema kweli vimetushangaza wengi ni pamoja na Utaratibu wa uchaguzi ktk chama hiki. Mara nyingi kama sii zote majina ya wagombea nafasi ya Mwenyekiti ktk chama hupendekezwa na wajumbe wa mkutano mkuu, kisha zikapigwa kura mshindi akajulikana pale pale ktk mkutano na sii swala la kila mwanachama kuchukua form kugombea kuongoza chama.
Power to the People, inaanza na mapendekezo ya wanachama na sii mtu kufikiria anaweza kuongoza chama, hivyo apewe uhuru na haki ya kugombea.

Pili, Swala la chama Chadema kumweka kitimoto Zitto ikiwa utaratibu wenyewe unaruhusu mtu kuchukua form, ni kithibitisho kamili cha Mapungufu ya chama hicho ktk kuthamini wanachama wake. Aidha Zitto hakutakiwa kushindana au haikuleta picha nzuri ndani ya chama swala hili limekibomoa chama zaidi kwa kuonyesha wazi kwamba chama hiki kina wenyewe na hasa kwa Wadanganyika itakuwa picha mbaya zaidi pale Zitto anapozidi kuongea maneno dhidi ya matokeo..

Ikumbukwe tu hakuna chama sdduniani kisichokuwa na wenyewe! hakuna ila wenyewe ni wale wenye kuamini itikadi na mafundisho ya ya mrengo husika. Na kati baina ya waumini hao wapo wenye Elimu, Hekima na Busara ambazo zinaambatana na uzoefu ktk kufafanua na kufuata kanuni, taratibu, maadili, miiko na kadhalika iwe ktk kusimamia vikao, kuwakilishi falsafa, au kupatanishi watu kwa kutumia misingi ilyiojengwa na mrengo husika.

Tatu swali langu linakuja kwamba - Does Zitto has what ita takes kuongoza chama?..kusema kweli binafsi sidhani, so was Mbowe sidhani kama alikuwa na elimu, busara na Uwezo wa kuongoza chama ila wanaweza wote kuwa wagombea wazuri kuwakilisha chama Chadema ktk kiti cha Urais. na hapa ndipo CCM inapotufunga magoli, JK ni mwekeykiti wa chama lakini kabla hajachukua kiti hicho alipitia darsa zito, yaani alipikwa kuelewa nini chama chake kinasimamia hata iwe ni Ufisadi ndani yake au Umafia ni lazima kiognozi wa chombo hiki ale yamini, (Kiapo) kwamba hatasaliti mawazo na fikra za zilizotangulia kwa kujenga agano jipya ndani ya chama..

Mwisho, inasikitisha zaidi kusikia Zitto kajitoa kugombea kiti hiki baada ya mfutano mkubwa baina yake na Uongozi wa Chadema. Ilikuwa ni haki ya Zitto kuchukua form kwa sababu mfumo na utaratibu wa uchaguzi ndani ya Chadema ni mbovu. Hivyo ilikuwa ni jukumu la chama kukubali Zitto aendelee kugombea, hata kama matokeo yapangwe Zitto akaridhia kushindwa kama ilivyotokea Uchaguzi wa kwanza wa TANU kati ya Mwalimu Nyerere na AbdulWaheed. Lakini hii habari ya Zitto kujiondoa na kudai anafanya hivyo KUKIOKOA CHAMA.

Hakika hakiokoi chama ila inanikumbusha kina Lowassa na scandal za Richmond ati kujiuzuru kwao ni kukiokoa chama. Swala hili halikuakiwa kufikia hapa lilipofikia na inaonyesha wazi kuna pengo kubwa la fikra ndani ya uongozi wa Chadema kiasi kwamba swala dogo sana la Ziutto limeweza kutingisha chama..
Zitto hakufanya makosa yoyote zaidi ya kusema sema ovyo kujibu kesi isiyokuwepo. Na Viongozi na Chadema hasa hilo baraza la wazee limeonyesha wazi jinsi lisivyokuwa na hekima wala busara kuchukua na kutangaza upinzani wa Zitto kama vile mhusika yaani Zitto ni mnafiki, muasi na mtoto mpotevu wakati sheria ya chama inamruhusu mtu yeyote kugombea kiti hicho..

Mkandara,

Wewe unafaa kuliko wote waliogombea; kachukue form ya kuwa mwenyekiti haraka haraka ukiokoe chama.

Ila bado tutasema ni cha watu wa Kaskizini, ngumu kweli kumridhisha mwanadamu.
 
Hi Rufiji,

Bravo for your good commentary on this thread.

This is a naked truth! To be frank,when I heard Mr Zitto's surprise announcement that he would challenge Mr Freeman Mbowe for the chairmanship in the party's forthcoming elections my haert missed some beats. To my mind I surely believed that the plan was engineered from external forces.

I am not sure whether Mr.Zitto seeked an advice from the Party elders or from his Chairman, Mr. Freeman Mbowe. If Kabwe have asked for an advice from these 2 areas he surely won't have been in this mess.

Yes, some can say democracy in CHADEMA have been abused! They can be right or wrong. But when someone thinks critically on this tug of war between Mbowe and Zitto he/she can trace some marks of external forces to split CHADEMA.

Everybody knows that CHADEMA is now becoming one of the most powerful political parties in Tanzania after CCM.Taking into consideration that CCM is now playing a very dangerous game of defending corruption/graft business in Tanzania. CHADEMA has proved beyond reasonable doubt that they can really fight corruption in Tanzania.CCM, the ruling party is doing contrary to many Tanzanians wishes and therefore CCM stands a chance of loosing come 2010 General Election! CCM really knows this!

Now,what can CCM do now to rescue their boat from capsizing? One of their style of doing things in order to make them survive is to apply the split and rule method. They have to use people like Zitto to split other political parties and rule them externally.Believe me or not, before the GE 2010 we shall witness a number of political party members(opposition) migrating from their parties to CCM and vice versa.

CCM can use any member at any cost from any other political party to split and total distabilization of any opposition party. I believe this is now happening in CHADEMA. Zitto Kabwe is now being used by CCM to disintegrate CHADEMA totally! CCM started this kind of business to split and kill CHADEMA through the late Chacha Wangwe(RIP). They tried but failed, now once again they want to use Zitto Kabwe!!!

Zitto Zuberi Kabwe must be clever enough to know and study the tacts of CCM. If he failed and won't be clever enough, CCM can do anything to harm him or use him from a different angle to bring a confusing atmosphere in CHADEMA before 2010 GE!!. I don't like to see what happened to the late Chacha Wangwe happening again to Zitto Kabwe!

I congratulate CHADEMA elders for saving a day for CHADEMA. Let me coclude by saying this:CHADEMA,watch out, the enemy is just knocking at your doors.

Take care!

Makoye
 
Je, Kujitoa Kwako Kugombea Uenyekiti Kunajenga au Kunabomoa Chama?

Ndugu Zitto Kabwe (MB),

Nimeamua kukuuliza swali hili la wazi kwa faida ya Jamii ya Kitanzania kwa ujumla. Ningeweza kukuuliza kwa faragha ila kufanya hivyo kungenisaidia mimi binafsi. Naamini suala hili linapaswa kujadiliwa kwa uwazi na ukweli.

Nilikuwa safarini hivyo nilipitiwa na hizi taarifa za wewe kujitoa kugombea Uenyeketi. Leo baada ya kusoma taarifa hizo katika za Vyombo vya Habari nimepigwa na butwaa. Swali kuu nalojiuliza ni, je, kujitoa kwako kutasaidia kuleta huo umoja ndani ya chama chenu au ndio utakigawanya zaidi?

Swali hilo kuu linazaa maswali haya mengine ambayo naomba uyajibu:

1. Je, hukuona kuwa utakigawanya chama ulipochukua fomu?
2. Je, huoni kuwa ni hatari kubadili msimamo mzito kama huo?
3. Je, haionekani kuwa umewasaliti waliokuomba ukagombee?

Ndugu nitashukuru kama utanijibu maswali hayo ili nisibaki naamini kuwa hata hicho 'chama kina wenyewe'!

Wasalaam,
Mpiga Kura

1. Zitto is pragmatic and statesmanlike to a fault, analeta standard mpya za politics Tanzania.yaani hapa alikuwa na kila right ya kubishana na kukipasua chama aondoke na faction yake, lakini amechukua the high road na ku chill. I gotta give it up to him for that.

2.Ingawaje anaweza kubanwa katika style ya "zero tolerance" na misingi ya "Ready to Die", maswali ya hapo juu si ya kumbana kabisa.

1. Je, hukuona kuwa utakigawanya chama ulipochukua fomu?
2. Je, huoni kuwa ni hatari kubadili msimamo mzito kama huo?
3. Je, haionekani kuwa umewasaliti waliokuomba ukagombee?

1. Katika kinyang'anyiro kama hiki, mara nyingi tu mambo hu evolve na kuchukua "a life of their own" kiasi kwamba kuna mengi hayatabiriki.Inawezekana Zitto kwa nia njema kabisa alitaka kudumisha demokrasia chamani lakini akakuta as well intentioned as that move could be, the division and infighting that it would cause would do more harm to the party than the amount of democratization would do good.

2.Kubadili msimamo si hatari ikiwa kubadili msimamo kutaepusha hatari kubwa kama chama kugawanyika au bad blood na sehemu kubwa ya uongozi wa CHADEMA. Waswahili wanasema "Heri nusu shari kuliko shari kamili". Kwa Zitto ku declare kugombea uenyekiti amenunua nusu shari, kuendelea kugombea kungeweza kuleta shari kamili.Ingawa in principle Zitto yuko justified, lakini in practice move hii ingeweza kuleta mabaya mengi kuliko mazir kama nilivyoeleza juu hapo.Kwa hiyo in a utilitarian way, mchumi wetu huyu amejua ku gracefully bow out.Yaani kama hii ndiyo sababu ya kuondoka katika kinyang'anyiro hiki mimi namuona Zitto mshindi hata baada ya kutoka katika uchaguzi huu.

3. Waliomuomba agombee kama wanamuelewa vizuri wataelewa kuwa "He who fights and run away, lives to fight another day".Tunamuhitaji Zitto, tunaihitaji CHADEMA in one piece. Kama Zitto ameishinda ego yake kwa kuamua kujitoa humbly ili kukinusuru chama mimi naiona hii si betrayal kwa waliomuomba agombee, mimi naiona hii ni quality ya leadership ya hali ya juu.

Jenerali yeyote inabidi ajue timing, wapi na muda gani kushambulia, wapi na muda gani kurudisha majeshi nyuma.huwezi ku front kila sehemu kila saa, inabidi akili kumkichwa.
 
One more confirmation that African politics revolve around rersonalities, not policies.
 
Hakuna demokrasia yeyote ndani ya Chadema, kumbe nao ni Mafisadi wa Demokrasia kama CCM, halafu hiki chama kinataka kipewe kuongoza nchi? Hivyo vibabu vinne si ndio vitakuwa vina maamuzi makubwa katika kila jambo linaloihusu nchi. Chadema ni mufilisi wa demokrasia.
 
Mi nazani chadema sasa wanatakiwa kupima, kuna madudu wanafanyika ila kwa sababu ya ukipofu wetu hatuyaoni, ila Zito na akina kitila wameyaona hayo, mie niwashukuru kwamba wamekuwa waungwana na wanataka kuyabadili hayo madude japo wamekatiliwa mbali, Chacha wangwe alipiga kelele watu wakasema anatumiwa na bangi zinamsumbua, sasa ni kazi kwao sasa wale ambao hawavuti bangi wamekuja kwa namna, na hao ndo akina zito.
 
kwa kitendo wanachotaka kufanya ni sawa na maana ya kwamba hakuna democarsia katika chama ikiwa chama si cha mtu mmoja wala jamii fulani. Chadema wamchemsha
 
Hatuongelei uongozi pekee asilimia kubwa hasa hao wazee wa chama hicho ni familia moja wakina mtei na wenzake
Kimbweka,
Sikutaka kuingilia mjadala uliokuwa ukiendelea. Lakini nadhani ni vizuri kuweka record sahihi. Sidhani kama Wazee wa Chama waliohusika ni wanandugu wote, ukimwacha Mzee Mtei, ambaye it is a historical fact kuwa ni Founder wa Chadema and commands high respect with the Chadema family. Wazee wengine wa Kamati ya Wazee ni
:-i) Balozi P. Ngaiza, Mjumbe wa Kamati Kuu,
2) Prof. Mwesiga Baregu, (ambaye hakushiriki kwa vile alikuwa safari) Mjumbe wa Kamati Kuu.
3) Mhe. Jaffari Kassisiko, Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma.
4) Mhe. Philemon Ndessamburo alishiriki sehemu ya Mkutano
5) Katibu Mkuu kama Returning Officer wa Chaguzi za ndani ya Chadema.
It is therefore not factual kusema kuwa wazee hao wote ni ndugu. Nadhani facts ziwekwe kama zilivyo, bila kujali mtu angependelea kuona au nini kifanyike.
 
Pumbavu chadema mafisadi wa Demokrasia,Mimi sina chama ila naamini demokrasia kuanzia kwenye familia,sasa nyie .......duh aibu...aibu...aibu
 
NIMESIKITISHWA SANA NA KITENDO CHA ZITTO KABWE KUJITOA KWENYE KINYANG'anyiro cha uongozi eto sababu wazee wamemshauri hivyo, sasa vijana lini wataonekana na lini tutaweza kuonyesha uwezo wetu jamani
 
It is time to move on.Wanachama wa Chadema na viongozi wameona ninji watanzania wanataka .Na wao wameona hali halisi ya kisiasa Nchini wameamua kuamua kwa njia hiyo na wao wako focused na kuunda Chadema mpya akiwepo Mbowe inawezekana kabisa .Tuwape nafasi watu wafanye kazi .Zitto ni mwanasiada anaye elekea kukomaa .Mbowe ni mkongwe .Ameona maandiko yetu maoni yetu .Amejua jinsi wa walivyo na mawazo tofauti so naamini sasa kwamba tukiwapa muda wakajipanga waje hapa na majina mapya ya uongozi mpya .Tupambane na mafisaidi.Bora ufasadi huu wa kuweka umoja wa Chama kuliko ule wa kula maliasili za Nchi .Chadema wamakubaliana na tuache kuendelea na maneno ya kejeli.Ila wamesha jua kwamba next tuta taka hata watu 10 kugombea uenyekiti .Wamekinusuru chama kwa sasa lakini haitakuwa tena hivyo wakati ujao .

Chadema nataka kusema kwa uwazi hapa .No sitaki ku spill the beans nita waandikia sirini niwaeleze matatizo ambayo yanapigiwa kelele na naamini whoever whill join Mbowe lazima ayafanyie kazi .Nitaandika kwa wote ambao ni viongozi wa sasa na baadaye nitawakumbusha viongozi wapya .

Kila jambo jema Chadema .Mbowe na Zitto mlishikana mikono iwe kweli na Chadema yetu izidi kupepea.Hongera Mzee Slaa kila mara busara zako zimekuwa mbele sana .Tuko nanyi .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom