Je, Kujitoa Kwako Kugombea Uenyekiti Kunajenga au Kunabomoa Chama?
Ndugu Zitto Kabwe (MB),
Nimeamua kukuuliza swali hili la wazi kwa faida ya Jamii ya Kitanzania kwa ujumla. Ningeweza kukuuliza kwa faragha ila kufanya hivyo kungenisaidia mimi binafsi. Naamini suala hili linapaswa kujadiliwa kwa uwazi na ukweli.
Nilikuwa safarini hivyo nilipitiwa na hizi taarifa za wewe kujitoa kugombea Uenyeketi. Leo baada ya kusoma taarifa hizo katika za Vyombo vya Habari nimepigwa na butwaa. Swali kuu nalojiuliza ni, je, kujitoa kwako kutasaidia kuleta huo umoja ndani ya chama chenu au ndio utakigawanya zaidi?
Swali hilo kuu linazaa maswali haya mengine ambayo naomba uyajibu:
1. Je, hukuona kuwa utakigawanya chama ulipochukua fomu?
2. Je, huoni kuwa ni hatari kubadili msimamo mzito kama huo?
3. Je, haionekani kuwa umewasaliti waliokuomba ukagombee?
Ndugu nitashukuru kama utanijibu maswali hayo ili nisibaki naamini kuwa hata hicho 'chama kina wenyewe'!
Wasalaam,
Mpiga Kura