Kwa upande wangu naona hilo ni jambo la busara sana sana,kosa lake ni lile la kutaka kugombea wakati bado wakuu wa Chama yeye akiwa mmojawapo bado wanazo nguvu za kupambana na CCM,ukiangalia kule CUF yule Kuchi(Mzee Mloo) alipojiona mikiki ya kwenda na kurudi mikoani haiwezi tena alijiuzulu na nafasi yake kupewa mtu mwengine ambae ni katika wakuu wa Chama,hivyo ushauri wangu tokea mwanzo ni wale top leaders wa Chama wasio tetereka kutulia katika nafasi zao ,wasifanye tamaa ya kutaka kumpiku alie juu katika wao ,kwani kufanya hivyo ndio kunakokiyumbusha Chama na kukigawa kiundani,wanatakiwa watulie na kukijenga Chama na pia kutayarisha viongozi wa kuwarithi na si kukigawa Chama.Ukiangalia katika CUF huoni kiongozi aliemo katika safu ya uongozi kutaka kugombea nafasi ya juu yake au ya chini yake ,wapo wametulia na ugombezi uko wazi kwa mtu yeyote yule ila ukiangalia kwa makini utaona si kwa aliendani ya uongozi wa juu ,nafasi ipo wazi kwa wanachama walio nje ya uongozi wa juu na ndio demokrasia inavyotakiwa kuwapa uhuru na wengine lakini si kwa walio ndani ya uongozi Mkuu,ikiwa kutazuka mmoja alie ndani kutaka kugombea basi ujue kuna tatizo hapo tena sio dogo.