MawazoMatatu
JF-Expert Member
- Sep 6, 2008
- 505
- 63
Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.
Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.
Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!
Haya ambayo nimeyaandika hapa JF nimewaambia vijana hawa 'face to face' ili waache uwongo, uzandiki, majungu, fitna na chuki.
Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.
Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.
...au Zitto mwenye ataropoka.
asha
Posting yako ina reveal mengi katika Wanademokrasia nyie na hali inatisha ikiwa ni hivyo.
Jambo moja tu la kujiuliza Jee Mbowe ana roho safi nawe kama unavyoonekana wewe? Kama mtakuwa lenu moja sawa lakini kama yeye ni hao Makao Makuu basi aidha Chama kipya chaja au Makamba kupokea Vigogo wa Upinzani .
Wahenga walisema; "UKIONA NGOMA INAVUMA SANA, INAKARIBIA KUPASUKA" na "UKIONA GIZA TOTORO, MAPAMBAZUKO YANAKARIBIA"
Nina mashaka kama Post hii kaandika Zitto mwenyewe ninayemfahamu. Nahisi kuna mtu ana Password yake ndio kaweka haya maneno hapa.This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.
Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.
Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!
Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.
To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?
Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.
Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.
Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia kuwa kamwe sitajiunga CCM. Lengo langu kuu ni kusaidiana na wenzangu kuhakikisha tunaondoa ukiritimba wa chama kimoja ndani ya Bunge. Soma signature yangu! Kwenda CCM is not an option. Wanaonijua wanajua hilo. Wasionijua wanadhani ninaweza hata kufikiria kwenda CCM.
Zitto, wewe ni Kijana tunakubali lakini wadhifa wako ndani ya Chadema si wa vijana, uko juu zaidi. Siyo vizuri kuonyesha upendeleo wa waziwazi hasa kwa mjumbe kwa sababu tu umetoka naye sehemu moja. La hasha hiyo haijengi demokrasia. Mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza. Nadhani una nafasi ya kujifunza mengi na utaendelea kujifunza jinsi muda unavyokwenda. Kama katiba inasema mshindi lazima apate zaidi ya 50% basi na matakwa ya katiba yafuatwe, msipindishe. Na kama mgombea ambaye unamtakia ushindi anakubalika basi atapita tu na wala huhitaji kuhangaika usiku kupiga kampeni.
Zitto, wewe ni Kijana tunakubali lakini wadhifa wako ndani ya Chadema si wa vijana, uko juu zaidi. Siyo vizuri kuonyesha upendeleo wa waziwazi hasa kwa mjumbe kwa sababu tu umetoka naye sehemu moja. La hasha hiyo haijengi demokrasia. Mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza. Nadhani una nafasi ya kujifunza mengi na utaendelea kujifunza jinsi muda unavyokwenda. Kama katiba inasema mshindi lazima apate zaidi ya 50% basi na matakwa ya katiba yafuatwe, msipindishe. Na kama mgombea ambaye unamtakia ushindi anakubalika basi atapita tu na wala huhitaji kuhangaika usiku kupiga kampeni.