Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Kama Presha imepanda ivo ndani ya CHADEMA nashauri Zitto na Mbowe woote mpumzike, Zitto uendelee na mpango wako wa awali wa kwenda masomoni na kupumzika siasa kwa muda mpaka maji yatakapotuama.Mbowe nawewe kagombee ubunge na uendelee kujenga chama vijijini! maana kwa jinsi ilivo inaonekana kuna makundi mawili makubwa la Mbowe nala Zitto.
 
Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.

Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.

Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!

Haya ambayo nimeyaandika hapa JF nimewaambia vijana hawa 'face to face' ili waache uwongo, uzandiki, majungu, fitna na chuki.

Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.

Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.

Posting yako ina reveal mengi katika Wanademokrasia nyie na hali inatisha ikiwa ni hivyo.
Jambo moja tu la kujiuliza Jee Mbowe ana roho safi nawe kama unavyoonekana wewe? Kama mtakuwa lenu moja sawa lakini kama yeye ni hao Makao Makuu basi aidha Chama kipya chaja au Makamba kupokea Vigogo wa Upinzani .
 
Du washikaji mnapofanya kazi kwa style hii mnakuwa kama askari wa Lucifer wanavyofanya kazi mnashambulia bila huruma.

Swali la kujiuliza mnalipwa nini kufanya hivyo? au ndiyo

damu ya albino au miili ya watoto wadogo(chini ya miaka 18) au miili ya mama wajazito wanaokufa kama kuku kwa upumbavu wa CCM

Mshahara wa dhambi ni mauti!
 
...au Zitto mwenye ataropoka.

asha

Duh, mpaka Asha Abdala leo anasema Zitto "ataropoka"?

Wahariri wenye mahusiano ya CHADEMA wanaita watu "vijana wajinga"...

Adwin Mtei anashutumu wanachama na vijana kwa "kupenyeza hela chafu"...

Zitto nae anamnyooshea vidole Mwenyekiti Mbowe kuwa ni "bepari" anaefukuza wanachama...

Mmenyimana nini huko chamani?

Kama chama kikiparaganyika na kudhoodhika, itakuwa ni kosa la Katibu Mkuu Dr. Slaa (ambae kakaa tu anaangalia sokomoko kama staili ya Kikwete , pamoja na Zitto Kabwe, ambae ameingia kwenye kampeni kwa kumnyoshea vidole Mbowe. Hakuwa na haja ya kufanya hivyo, angesema tu Mbowe amekifikisha chama mahala fulani, na mimi nataka kukisogeza mahala fulani.

Mwenyekiti Mbowe, japo nae yuko kimya kama staili ya Kikwete, kwa sasa anavyofanya nadhani ni sawa kabisa, maana yeye ni mgombea, hatakiwi kuwa refarii wakati huo huo.

Edwin Mtei, Nyerere wa CHADEMA, akae kimya, au akiongea aepuke hotuba za kushutumu watu ufisadi bila uthibitisho.

Huu ni wakati wa uchaguzi, nchi nzima imewatolea macho, sio wakati wa kuanika machafu chafu yenu.
 
Nahisi chama kipya chaja na bunge lijalo lote ni CCM
 
Wahenga walisema; "UKIONA NGOMA INAVUMA SANA, INAKARIBIA KUPASUKA" na "UKIONA GIZA TOTORO, MAPAMBAZUKO YANAKARIBIA"
 
sijui nani kawaroga CHADEMA, bado sipati jibu hivi hawa wazee akina mtei wangeacha mbowe na zitto wakapambana kulikuwa na tatizo gani?? sasa chama kinasambaratika huo uzee wao unaochangia kuvuruga chama ni uzee wa wapi??
 
Zitto, wewe ni Kijana tunakubali lakini wadhifa wako ndani ya Chadema si wa vijana, uko juu zaidi. Siyo vizuri kuonyesha upendeleo wa waziwazi hasa kwa mjumbe kwa sababu tu umetoka naye sehemu moja. La hasha hiyo haijengi demokrasia. Mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza. Nadhani una nafasi ya kujifunza mengi na utaendelea kujifunza jinsi muda unavyokwenda. Kama katiba inasema mshindi lazima apate zaidi ya 50% basi na matakwa ya katiba yafuatwe, msipindishe. Na kama mgombea ambaye unamtakia ushindi anakubalika basi atapita tu na wala huhitaji kuhangaika usiku kupiga kampeni.
 
Posting yako ina reveal mengi katika Wanademokrasia nyie na hali inatisha ikiwa ni hivyo.
Jambo moja tu la kujiuliza Jee Mbowe ana roho safi nawe kama unavyoonekana wewe? Kama mtakuwa lenu moja sawa lakini kama yeye ni hao Makao Makuu basi aidha Chama kipya chaja au Makamba kupokea Vigogo wa Upinzani .

Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia kuwa kamwe sitajiunga CCM. Lengo langu kuu ni kusaidiana na wenzangu kuhakikisha tunaondoa ukiritimba wa chama kimoja ndani ya Bunge. Soma signature yangu! Kwenda CCM is not an option. Wanaonijua wanajua hilo. Wasionijua wanadhani ninaweza hata kufikiria kwenda CCM.
 
Wahenga walisema; "UKIONA NGOMA INAVUMA SANA, INAKARIBIA KUPASUKA" na "UKIONA GIZA TOTORO, MAPAMBAZUKO YANAKARIBIA"

nakwambia mkuu sasa hivi Makamba agonga kilauli tu na mzee chilli
 
Haya ya Zitto sasa yanakatisha tamaa. Attitude ya Zitto ya kulinda heshima binafsi inaweza kuwa very damaging kwa chama na movement nzima ya mageuzi. Ni wazi kuwa chadema is more than Zitto wala haihitaji kusisitizwa hii. Ni wazi pia kuwa ndani vyama (any form of association) kuna differences, lakini namna ya kutatua matatizo si kumwaga mboga baada ya wengine kumwaga ugali! Mbona tumeona watu wengi wanasemwa kwa mabaya sana lakini wamekuwa wavumilivu! Naingiwa na wasiwasi sana na Zitto na uanamageuzi wake na qualities zake za uongozi! Zitto hivi unadhani akina Obama wangekuwa wanareact hivi wangefika kweli! You are now turning into a liability from an asset! Take a few days off.
 
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.
Nina mashaka kama Post hii kaandika Zitto mwenyewe ninayemfahamu. Nahisi kuna mtu ana Password yake ndio kaweka haya maneno hapa.
Ila kama niyeye mwenyewe na hajapiga mvinyo (NAJUA HUU NI MWEZI MTUKUFU) basi something wrong somewhere.
 
Chadema can't grow big! Ukubwa tayari umeshakizidi. Haya ninayoyasoma humu yanashangaza kiasi fulani.

Lakini ndiyo matokeo ya politics of patronage na madhara ya wazi ya mifumo ya kikoministi waliyoturithisha CCM. Kila chama kinaanguka katika utelezi ule ule!!
 
Hivi Zitto kugombea Uenyekiti ni kumu embarass Mbowe?
 
Hili limetusaidi kujau rangi za wengi humu na mnayoyataka yatakuja
 
Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia kuwa kamwe sitajiunga CCM. Lengo langu kuu ni kusaidiana na wenzangu kuhakikisha tunaondoa ukiritimba wa chama kimoja ndani ya Bunge. Soma signature yangu! Kwenda CCM is not an option. Wanaonijua wanajua hilo. Wasionijua wanadhani ninaweza hata kufikiria kwenda CCM.

lakini mkuu zitto vipi mtaondoa ukiritimba wa chama kimoja ndani ya bunge ili hali mnatukosesha usingizi tunawaza inakuwaje? au mmekoseana nini mpaka mnatupa pressure?? ah.... mnakera sana watu tumekuwa na matumaini leo hii ndo tunaambulia kashfa tu mitaani kwetu.....zitto niambie sisi tutajificha wapi dhidi ya kejeli za CCM mtaani kwetu..???
 
Zitto, wewe ni Kijana tunakubali lakini wadhifa wako ndani ya Chadema si wa vijana, uko juu zaidi. Siyo vizuri kuonyesha upendeleo wa waziwazi hasa kwa mjumbe kwa sababu tu umetoka naye sehemu moja. La hasha hiyo haijengi demokrasia. Mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza. Nadhani una nafasi ya kujifunza mengi na utaendelea kujifunza jinsi muda unavyokwenda. Kama katiba inasema mshindi lazima apate zaidi ya 50% basi na matakwa ya katiba yafuatwe, msipindishe. Na kama mgombea ambaye unamtakia ushindi anakubalika basi atapita tu na wala huhitaji kuhangaika usiku kupiga kampeni.

Kwani Kampeni ya wazi ni kosa? Na jee ukiwa kiongozi hupigi kura kwani kupiga kura maana yake ni kumchagua mmoja unaempendelea.

Naona una mtuhumu Zitto bure kwa mambo mawili hayo, iwapo itathibitika kuwa alitumia hongo basi lazima awajibishwe kwa kosa hilo.
 
Zitto, wewe ni Kijana tunakubali lakini wadhifa wako ndani ya Chadema si wa vijana, uko juu zaidi. Siyo vizuri kuonyesha upendeleo wa waziwazi hasa kwa mjumbe kwa sababu tu umetoka naye sehemu moja. La hasha hiyo haijengi demokrasia. Mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza. Nadhani una nafasi ya kujifunza mengi na utaendelea kujifunza jinsi muda unavyokwenda. Kama katiba inasema mshindi lazima apate zaidi ya 50% basi na matakwa ya katiba yafuatwe, msipindishe. Na kama mgombea ambaye unamtakia ushindi anakubalika basi atapita tu na wala huhitaji kuhangaika usiku kupiga kampeni.

Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.

Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.

Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.

Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom