...au Zitto mwenye ataropoka.
asha
Duh, mpaka Asha Abdala leo anasema Zitto "ataropoka"?
Wahariri wenye mahusiano ya CHADEMA wanaita watu "vijana wajinga"...
Adwin Mtei anashutumu wanachama na vijana kwa "kupenyeza hela chafu"...
Zitto nae anamnyooshea vidole Mwenyekiti Mbowe kuwa ni "bepari" anaefukuza wanachama...
Mmenyimana nini huko chamani?
Kama chama kikiparaganyika na kudhoodhika, itakuwa ni kosa la Katibu Mkuu Dr. Slaa (ambae kakaa tu anaangalia sokomoko kama staili ya Kikwete , pamoja na Zitto Kabwe, ambae ameingia kwenye kampeni kwa kumnyoshea vidole Mbowe. Hakuwa na haja ya kufanya hivyo, angesema tu Mbowe amekifikisha chama mahala fulani, na mimi nataka kukisogeza mahala fulani.
Mwenyekiti Mbowe, japo nae yuko kimya kama staili ya Kikwete, kwa sasa anavyofanya nadhani ni sawa kabisa, maana yeye ni mgombea, hatakiwi kuwa refarii wakati huo huo.
Edwin Mtei, Nyerere wa CHADEMA, akae kimya, au akiongea aepuke hotuba za kushutumu watu ufisadi bila uthibitisho.
Huu ni wakati wa uchaguzi, nchi nzima imewatolea macho, sio wakati wa kuanika machafu chafu yenu.