Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Selous!

Thanks a lot umemkumbusha huyo kijana ZZKabwe kwamba sio wote tuna short memory kama yeye. Tunataka majibu aliposhabikia kwamba mitambo ya DOWANS inunuliwe kwa manufaa ya taifa je alitumwa na wapiga kura wake wa huko Kigoma au alitumwa na RA. That mistake was the last nail in his political coffin. In fact politically he is in the morgue ila kwa staili ya Kinganganizi ya CCM bado anajiona ana nguvu. Hao watoto wa kijiweni anaowazuga na pesa chafu ili wampambe kuna muda utafika watangamua kwamba yeye ni bua na watamwacha solemba.

Hakuna mtu atakayekula ngawira za RA akaacha kufulia kama mnabisha kamuulize JMK hicho kigigumizi amekipta wapi ni kwa sababu ya ushirika wake na swahiba RA SI NDIYE aliwakodishia Ndege kwenda Dodoma BOYZ to men I mean yeye na kipenzi chake Teddy Lowasa lakini marehemu Julius Kambarage Nyerere akawashtukia mnafikiri tunasahau. Kwa taarifa yenu sisi ndio watupa maganda hatusahau ngodo!!
 
MH,Zitto

Poleni na mambo ya uchaguzi,Ila nina mambo kadha nataka kukueleza,kwanza usilalamike sana kuhusu mama yako mzazi kuongelewa kwenye mambo yaliondelea inavyonekana na kwa jinsi ulivyoandika inaonyesha dhairi kabisa mama yako anashiriki kwa karibu saana kwenye mambo yako yakisiasa kwa hiyo ujue kama anajiusisha basi iko siku hata mbeleni atazungumziwa tu,hilo huwezi kulikataa,mpaka labda siku ikiamua kutojiusisha na mambo ya siasa kiundani saana.


Mifano tunayo kama pale tulipoona wakati wa uchaguzi kule marekani ,wakati Obama alipolalamika kuwa wamuache kuongelea familia yake ,ndipo watu walipoibuka nakusema kama hutaki tusimuongelee mkeo basi asipande majukwaa,kwa hiyo bwana mkubwa vumilia tu.

Mh, punguza mambo ya kumwaga data za mambo yanayoendelea kwenye chama chenu !!. yani umeamua hata kutangaza matokeo humu wakati ulitakiwa utulie mpaka wahusika watangaze halafu wewe ndio labda uibuke na kutueleza unachojua ,ila nimegundua kila kikitokea kitu kwenye chama chenu wewe unaibuka na ka breaking News kako, anagalia saana hiyo ni siasa na unapambana na wanene wa hicho chama !!

Hayo mambo ya chuki na fitna inabidi uyazoee ndio siasa usianze kulilia mapema mambo bado saana kama ni bado utakua unania ya kuusaka uonngozi wa juu zaidi ''you have not seen nothing yet''

politics is a dirty game

Take care
 

Yaani mwisho wake kwa sababu yeye amesema\/ ni ukiwa mwisho wake nani anafaidi? jamani ebu muwe mnawaza glabally kabla ya kuropoka

Nina mashaka kama Post hii kaandika Zitto mwenyewe ninayemfahamu. Nahisi kuna mtu ana Password yake ndio kaweka haya maneno hapa.
Ila kama niyeye mwenyewe na hajapiga mvinyo (NAJUA HUU NI MWEZI MTUKUFU) basi something wrong somewhere.

Ni lini watu watakubali kuwa wakweli na kuwa tayari kusikiliz ukweli, kama ni yeye ameandika, kwa nini usikue katika post hiyo na kuona hali halisi ya siasa ya nchi yako.What is he is confessing!!



You have done the same thing Mkandara1 kila ulichoandika kimekujia na wewe, kuna neno linaitwa KUGHAFIRIKA, kama unaona kuna mapungufu siyo kusema hivi, mtafute huyo Zitto ujue hali yake kwa sasa na anapitia mambo gani, WE ALL SOMETIME DOING FOOLISH THINGS, it aonly needs a man not a boy to think beyond that na kuweka mambo sawa. Kuwa mwenyekiti si kuwa malaika ndio maana tuna akina Kikwete, Hitler, tuna akina Obama. Obama juzi naye alisema foolish coments regarding yule polisi aliyemuarrest black professor! the same obama we all know about.
The question is if you believe in Zitto what is real happening now in his life??

You need tto make a change no just to wait some people doing that.

What is your take??? this is question for you, na post hii umefanya jambo la maana la kumuokoa Zitto au umekaa pembeni kama mshabiki??

We are just human, here we are

''In Our Darkest Hour
In My Deepest Despair
Will You Still Care?
Will You Be There?
In My Trials
And My Tripulations
Through Our Doubts
And Frustrations
In My Violence
In My Turbulence
Through My Fear
And My Confessions
In My Anguish And My Pain
Through My Joy And My Sorrow
In The Promise Of Another Tomorrow
I'll Never Let You Part
For You're Always In My Heart''
Michael Jackson


Problem is that we think we know TOO MUCH!



 
duh zitto kwa uhakika tu na kama unaelewa huu ndo mwisho wa kuvuma kwako,nadhani umri unakuponza kichwa kikakua,sasa unaleta vurugu katika chama na wala hauleti uelewano,wewe kama kiongozi wa juu na mwenye akili na mtaka mageuzi hukupaswa kwanza kuwa na MAKUNDI sasa,unataka kutuambia ungeshinda uenyekiti ndo ungefanyaje?ungeadhibu wale usiowapenda then chama kinadhoofika,wewe kwa ufupi huwezi madaraka,hufai kabisa,kama umepewa hela kuharibu demokrasia si useme?
 


Hakuna cha mwisho
hao wanaoandika humu na kuleta habari ni viongozi wa juu wa chadema,ama kosa la kuisha kwa Zitto ni kujisajiri kwa jina lake halisi.?

Haishi mtu ukweli lazima tuuseme ukweli ,hakuna cha siri hizi siri mnazoongelea ni hizo za staili ya kumpoteza Wangwe ama siri zipi?
 
This is why CCM will always win in every election for many years to come.

CHADEMA is going down. And this time, it is going down for real and it is, because you leaders have chosen so. Wallah, wakati mnakua ndio mnapoanza kufifia? Every five years, we see new party arising and then slwly dying.

Mimi mara zote nimekuwa nikiamini kuwa chama mbadala katika nchi hii kinaweza (japokuwa kwa mbaaaali) kuwa CHADEMA. With this development, I wonder if the dream will ever come true. It is your party, Sir. Kill it if you want. And trust me, this is exactly how to do it.
 

CHADEMA haiendi kokote mkuu.
 
zitto duh! what a dissapointment!
yaani unakubali kuwa ulikuwa mmoja wa waliomzulia uongo chacha wangwe , kisha unakuja hapa unaropokwa!
ndio tukuone mwema sana kwa kuwa leo umesema ukweli baada ya kuzuliwa na wewe?

hufai kabisa kuwa katika siasa, kwa sababu hikma kwako ni sufuri......hata kama ulimzulia wangwe na umejutia, ulitakiwa uingie nalo kaburini.....kulisema hapa LEO hakusaidii chadema, hakukusaidii wewe wala wanachama wa chadema.

kisha unatoa shutuma kuwa chadema kuna ukabila pia ( rejelea maneno yako kuhusu nipashe,ippmedia na machame na mtei) .....

hivi hasa lengo lako ni nini pale unapoandika?
 
Mkuu naomba kuuliza maswali madogo tu. Hivi ndani ya CHADEMA kama mgombea mmoja akidhulumiwa au kuhujumiwa katika uchaguzi hakuna taratibu za kufuata (ikiwemo kukata rufaa) ili kuhakikisha anapata haki yake? Na je, wewe kama kiongozi mkubwa kabisa ndani ya CHADEMA, hukuweza kutumia uwezo wako kuhakikisha mtu huyo anapata haki sahihi kwa kufuata kanuni sahihi za chama na hata kuweza kuona wanaohusika kuminya haki za mwanachama huyo wanachukuliwa hatua? Je, kama yote hayo hayakuwezekana, unadhani chama kina uwezo wa kuhakikisha yanawezekana katika siku chache zijazo?

Maana kama hali itaachiwa kuendelea kuwa hivyo, ni dhahiri kuwa aidha mtaumizana sana kwenye chaguzi zenu, au haki itaendelea kuminywa na wenye uwezo kama wewe na wengine waliomo kwenye hicho chama. Mkuu, hakikishia umma kuwa wanacho chama ambacho mmekuwa mkikililia kila mara kuwa kitaleta ukombozi katika nchi hii. Tunayoanza kuyaona sio dalili za chama kama hicho.
 

Labda atakuwa ameteleza kidogo kiuandishi ...... siasa na pesa ni shetani
 
MkamaP,
Mkuu tumesha elezwa kwamba mwandishi ni mmoja wa viongozi wa Chadema, sikushangaa wala kusikitishwa zaidi ya kusoma na kuelewa kinachoendelea.. hakutajwa jina la mtu wala watu wala habari za vifo..
Mkuu wapo wengi tunawafahamu humu JF kuwa ni viongozi wa Chama Chadema au hata CCM wamo humu kwa majina ya bandia.. Ifahamike tu kwamba JF wapo watu wa kila aina na baadhi tunafahamu iwe wanatumia majina yao au bandia tunawajua vizuri tu.

Sisi sio watoto wadogo mkuu wangu tunaweza kuchambua pumba toka ktk mchele tena kwa kupeta tu..Pumba zitamwagika ardhini na mchele kubakia ktk ungo.. ndio JF inavyofanya kazi zake.
 
yawezekana kuwa zitto na kundi lake walitaka wachukue uongozi kamili wa chama.
zitto uenyekiti na wafuasi wake Baraza la wazee na Baraza la Vijana ili labda waendeshe chama kidemokrasia LAKINI njia walizotumia sizo!

wamesababisha vurugu la hali ya juu ndani ya chama, na badala ya kufanya damage control, ndio kwanza anakuja hapa anatuhadithia alivyomfanya chacha wangwe na kuzidi kukipaka matope chama kuwa kuna ubaguzi!

hivi zitto ulijitoa kugombea uenyekiti kwa kuwa ulete umoja ndani ya chama kweli? kwa sababu hii kuropokwa siri za chadema hapa JF hakuonyeshi kutafuta umoja, kunaonyesha kubomoa tu
 

Siku za Zitto kuhamia CCM zimeanza kuhesabiwa. Zitto ingia chama la kijani "ukapigane kutokea ndani".
 
Tumehuzunishwa sana na Makundi ya wakina Zitto na wenzake, Mambo kama haya yaishie ndani sio humo ndugu zangu. Hivyo kuna haja ya wakini Zitto kuwa makini na vitu na ngoma inayovuma kama hiyo wangalie isjie kupasuka..Maana kama watu wanashindwa kuwa makini sasa watu walio nje wataonekana vipi??
 
"What you see in Zitto is what you Get"........Once said by my friend Bob Mkandara and confirmed by Zitto himself....somewhere in JF..........damn!
 
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
 
NAsikia harufu ya damu!!!!!! Jamani hebu tusalimisheni kwa kuzungumza kwa staha kidogo. Mambo mengine munapitiliza sana. Hii haisaidii kabisa
 
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote

Zitto arudi kwa wenzie aombe radhi kwa kuleta details zao huku JF halafu waanze upya. It is not too late jamani. We can still win!!!
 
...haya na leo napata kali zaidi zitto nae na mamaake ndani,hiki chama nadhani ni saccos

Hiyo na mimi imeniacha hoi, sina mbavu.

Zitto analalamika watu wamemwingiza mamaake kwenye hili zogo la viongozi, lakini unapofanya kampeni na mamaako (kama ilivyoripotiwa) unategemea nini, of course siasa mchezo mchafu. people are gonna drug your mother into the mess.

Zitto anasema watu wanamvunjia heshima, lakini na yeye yupo mstari wa mbele kuita watu "wapumbavu." Vijana kama Mnyika, hata kama unaona ni vipumbavu, you don't say that in public, hususan kama unasema umeshawaambia uso kwa uso. Unajenga mahasimu ndani ya chama, you don't need more bitter enemies!

Cha ajabu ni kwamba hata hapa kwa ma strangers wa JF, Zitto huwa haiti watu "wapumbavu...wajinga," lakini leo anawaita CHADEMA wenzake wapumbavu.

Kwenye nchi zilizoendelea kiuchaguzi, ukurupukaji na hulka (temperament) ya kiongozi ni kitu muhimu sana kwa wapiga kura. John McCain kilichosaidia kuangushwa kwake ni ukurupukaji na hasira hasira. Siku za nyumba alikuwa haishi kuwaambia wabunge wenzake "https://jamii.app/JFUserGuide you" etc. etc.... Kirekodi kikamganda. Hasira za mkizi.

Imefika mpaka Zitto anaitangazia dunia kwamba kweli CHADEMA ni chama cha kikabila. Duuuh!

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…