Umesema kweli kabisa kwa sababu Zitto anaweza kuyaona makosa upande wa pili tu lakini yeye kashindwa kutazama jinsi watu wake wanavyopiga kampeni chafu against chama..Ebu someni habari aloandika zote hapa kisha tudini mkasoma kule - Kitabu cha Wangwe chaanika Ukweli tunaotakiwa kuujua.
Moja kwa moja utagundua kwamba hizi habari zinatoka ndani ya Chadema na sio CCM.. kisha utaanza kujiuliza tunakwenda wapi na how bad things are! yaani demokrasia ni nguvu na uwezo wa mtu kugombea nafasi ya Uongozi jamanai.. Hivi kweli mama Migiro alichukua form kugombea nafasi yake au alipendekezwa kwanza! Kina Salim wakati wa UN walipigwa vita lakini uume ni kuvumilia na kuanza upya .. Malecela jina lake lilienguliwa ktk kugombea Urais, Salim alinyimwa kura kurudiwa mara tatu, yote haya ni machafu ya siasa, huwezi sema haikutumika Demokrasia kwa sababu tu mtu fulani hakuhusishwa kutokana na mapungufu yake..Kuenguliwa jina la mgombea kutokana na mapungufu yake ni sehemu ya Demokrasia inayozungumziwa..
Kukomaa kwa mtu kisiasa ni uwezo wa kutambua yote haya, kuweka maslahi ya chama mbele ya maslahi binafsi, na yale ya Taifa mbele ya maslahi ya chama.
Ukweli unaoanikwa hapa ni kuonyesha wagombea wote wanathamini maslahi yao binafsi mbele ya chama..Ufisadi sio Uporaji na wizi pekee ila ni pamoja na uharibifu kama huu.