Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
Kama wanashindwa kuwa na Hekima tutawafundisha, maana wanapotaka kwenda huko siko kuzuri sana, Kuna haja ya kuwa na Hekima kubwa sana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mwakani, Majeraha yoyote yale wanaweza kutumiwa na CCM na Kuharibu sifa ya CHADEMa ambao wao wameijenga kwa muda mrefu sana. Sasa kama wao wanashindwa tutawaelekeza cha kufanya katika hekima na Busara zote na Sio hivi kama wao wanaenda sasa hivi
 
Zitto arudi kwa wenzie aombe radhi kwa kuleta details zao huku JF halafu waanze upya. It is not too late jamani. We can still win!!!

JF ni sehemu ambapo tunaongea kwa uwazi, hatumfichi mtu kwa hilo zitto hajakosea. Kama kuna anayelalamika kwa kusemwa humu JF naye amwage hapa nyanga zake tuzichambue.
 
JF ni sehemu ambapo tunaongea kwa uwazi, hatumfichi mtu kwa hilo zitto hajakosea. Kama kuna anayelalamika kwa kusemwa humu JF naye amwage hapa nyanga zake tuzichambue.

Zitto hajachelewa bado kurudi nyumbani (ccm). Wewe unaonaje hizo "nyanga"
 
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
Na Tena sasa naona kama Busara wanazidi kukosa. Tutawafundisha kwa maslahi ya Tanzania na CHADEMA. Ni vitu vya aibu sana kuona mambo kama haya katika wakati kama huu muhimu sana kwa CHADEMA.
 
Umesema kweli kabisa kwa sababu Zitto anaweza kuyaona makosa upande wa pili tu lakini yeye kashindwa kutazama jinsi watu wake wanavyopiga kampeni chafu against chama..Ebu someni habari aloandika zote hapa kisha tudini mkasoma kule - Kitabu cha Wangwe chaanika Ukweli tunaotakiwa kuujua.

Moja kwa moja utagundua kwamba hizi habari zinatoka ndani ya Chadema na sio CCM.. kisha utaanza kujiuliza tunakwenda wapi na how bad things are! yaani demokrasia ni nguvu na uwezo wa mtu kugombea nafasi ya Uongozi jamanai.. Hivi kweli mama Migiro alichukua form kugombea nafasi yake au alipendekezwa kwanza! Kina Salim wakati wa UN walipigwa vita lakini uume ni kuvumilia na kuanza upya .. Malecela jina lake lilienguliwa ktk kugombea Urais, Salim alinyimwa kura kurudiwa mara tatu, yote haya ni machafu ya siasa, huwezi sema haikutumika Demokrasia kwa sababu tu mtu fulani hakuhusishwa kutokana na mapungufu yake..Kuenguliwa jina la mgombea kutokana na mapungufu yake ni sehemu ya Demokrasia inayozungumziwa..

Kukomaa kwa mtu kisiasa ni uwezo wa kutambua yote haya, kuweka maslahi ya chama mbele ya maslahi binafsi, na yale ya Taifa mbele ya maslahi ya chama.
Ukweli unaoanikwa hapa ni kuonyesha wagombea wote wanathamini maslahi yao binafsi mbele ya chama..Ufisadi sio Uporaji na wizi pekee ila ni pamoja na uharibifu kama huu.
 
Mkandara hueleweki kosa gani Zitto kafanya? Robin Cook aliyekuwa waziri wa nje wa Labour aliweka wazi uozo wa Chama chake kwenda Iraq.soma ROBIN COOK THE POINT OF DEPARTURE ISBN 0-7432-5255-1
plz mwache Zitto yeye wamemzuia na mgombea wake kazuiliwa haki iko wapi?
 
Zitto amezuiliwa au kajitoa?
 
kwa watu wanavyojua spinning ....nasubiri baada ya masaa kudhaa kuambiwa kuwa "wasiomtakia wema Zitto wali hack account yake JF na kuja kusema waliyosema" ............manake i c that as the only way out kwa zitto kwa hili, credibility yake imeporomoka mno ndani ya masaa 24 tu!
 
Pole sana ndugu yangu. Naelewa feelings zako na za wengine humu ndani. Ninawahakikishia kuwa tutainuka, tutajipakusa vumbi na kukimbia tena pamoja. Mchakato huu waweza kuwa na matokeo ya kukikuza na kukikomaza chama sana. Tunajifunza katika changamoto hizi. Hatuwezi kukubali kuingia katika historia ya kuua CHADEMA. Kuna masuala fulani fulani ya msingi kabisa kuhusu mahusiano yetu na marafiki zetu ambayo lazima tuyashughulikie asap.

Deep in my heart i believe truth will prevail and the party will come up strong.

Mkuu, inatia faraja kuwa bado una imani kuwa chama chako kitaweza kuendelea kuwa imara hasa baada ya mambo hayo yaliyotokea na kufikia umma kwa njia ya magazeti na JF.

Kuna vitu vitatu ambavyo nahisi ingefaa kuwa itikadi yenu ndani ya chama. Uvumilivu, kuheshimiana na kulinda siri za chama chenu. Katika siasa (najua unafahamu sana tu), mambo hayo matatu hapo juu ndio silaha ya ukweli kwa mwanasiasa na kwa chama cha siasa popote duniani. Tafadhalini fahamuni kuwa umaarufu wa chama chenu umetokana na mambo hayo ambayo yalianza kuonekana, na sasa yanafifia kwa haraka. Kupanda mlima, ni kazi kuliko kushuka. Maana unaweza kushuka kwa kujiachia tu.

Mkuu, ningependa ukaiga wanasiasa mashuhuri wa ndani na nje ya nchi. Wanasiasa ambao kwa uvumilivu na subira zao wamefanikiwa na kudumu kwa muda mrefu sana kwenye siasa. Ukiweza kufanya hivyo, si tu kuwa utakomaa kisiasa, bali pia utakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa jamii unayotaka kuihudumia. Nahofia kuwa wanasiasa wengine kutokana na kutokuwa wavumilivu, wamekuwa "POPCORN POLITICIANS". Wanajitutumua kwa muda mfupi, mpaka wanapasuka halafu wanakuwa exposed inside out na kuishia kuwa useless. Ni hasara sana kutumia muda mrefu kujijenga kisiasa na baadae kuisha kiurahisi.
 
soma maelezo yake kasema kuna kundi lililofanya hila asiwe Mwenyekiti Taifa. tafrisi nyepesi kazuiliwa huna haja ya kuuliza swali hili.

Yaani unataka kuniamulia hata cha kuuliza?!
 
Mkandara hueleweki kosa gani Zitto kafanya? Robin Cook aliyekuwa waziri wa nje wa Labour aliweka wazi uozo wa Chama chake kwenda Iraq.soma ROBIN COOK THE POINT OF DEPARTURE ISBN 0-7432-5255-1
plz mwache Zitto yeye wamemzuia na mgombea wake kazuiliwa haki iko wapi?
Mkuu kwani kwenda Iraq ilikuwa mbinu ya chama against huyo Robin Cook?

Soma vizuri mkuu, nazungumzia kuthamini maslahi ya chama mbele ya maslahi Binafsi na Robin alisimamia maslahi ya Taifa mbele ya yale ya chama. sii ya Zitto kuweka maslahi yake mbele yale ya chama kuwa kigezo cha hoja na madai yake.
Elewa tofauti hizo utanipata nilichoandika hapo juu..
 
well yeah i made a mistake ....zitto anaweza ku pleadge temporay insane.......manake hii alotuachia leo si ya kawaida
 
Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.

Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.

Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.

Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.
Mkuu naomba kuuliza maswali madogo tu. Hivi ndani ya CHADEMA kama mgombea mmoja akidhulumiwa au kuhujumiwa katika uchaguzi hakuna taratibu za kufuata (ikiwemo kukata rufaa) ili kuhakikisha anapata haki yake? Na je, wewe kama kiongozi mkubwa kabisa ndani ya CHADEMA, hukuweza kutumia uwezo wako kuhakikisha mtu huyo anapata haki sahihi kwa kufuata kanuni sahihi za chama na hata kuweza kuona wanaohusika kuminya haki za mwanachama huyo wanachukuliwa hatua? Je, kama yote hayo hayakuwezekana, unadhani chama kina uwezo wa kuhakikisha yanawezekana katika siku chache zijazo?

Maana kama hali itaachiwa kuendelea kuwa hivyo, ni dhahiri kuwa aidha mtaumizana sana kwenye chaguzi zenu, au haki itaendelea kuminywa na wenye uwezo kama wewe na wengine waliomo kwenye hicho chama. Mkuu, hakikishia umma kuwa wanacho chama ambacho mmekuwa mkikililia kila mara kuwa kitaleta ukombozi katika nchi hii. Tunayoanza kuyaona sio dalili za chama kama hicho.
 
Sijui kama kuna dalili za kupona. Maana naona leo moto mpya umewashwa na kuuzima itakuwa gharama kubwa sana.

Sana sana kitakachotokea ni Zitto kwenda CCM (na kumuunga mkono Kikwete) kama ilivyokuwa mpango wake toka zamani. CHADEMA itaendelea kuwepo tu hata baada ya Zitto kuondoka.

Subiria kusikia Zitto akipewa ubunge wa kuteuliwa na uwaziri.
 
Mzimu wa Wangwe waiandama CHADEMA...Zitto,wat happened to Wangwe!??Naona katika kuporomoka kwako umeamua "kufa" na wengi.Politicians!
 
Mzimu wa Wangwe waiandama CHADEMA...Zitto,wat happened to Wangwe!??Naona katika kuporomoka kwako umeamua "kufa" na wengi.Politicians!

Hakuna cha mzimu wala pepo wa wangwe hapo. Zitto anatafuta pa kutokea ili arudi CCM.
 
Sasa nimeamini kuwa wananchi tuna safari ndefu ya kufika kanani...

Juzi CCM walikuwa na mtafaruku mkubwa kuliko huu wa CHADEMA ....wakapigana kwenye kamati kuu wametoka ..angalau hawakuja hapa kuanikana...

Wapinzani sasa mmejeuza jamboforums kuwa kamati kuu ya CHADEMA????....KWANINI mambo yenu ya ndani yasiishie ndani....hamuoni kuwa kwa mara nyingine mnawakatisha tamaa wananchi!!????

Tangu mwaka 1992 tunapambana tumeona wapinzani wakiendelea kuumizwa kwa mambo kama haya ...NCCR ya mwaka 1989 ilikuwa moto na wasomi wote ....lakini kumbe lilikuwa gari la UT la kusanya wapinzani waliokuwa wakichomoza....walishindwa kuifanya NCCR KUWA CHAMA PEKEE...

KAMAHURU na baadaye CUF ...baada ya kuungana na JAMES MAPALALA....yuko wapi mapalala?????

MREMA ..aliyevuma kama tsunami ...yupo wapi????

CHADEMA ambacho mwanzo kilikuwa chama wachache makini kisicho kuwa na watu....wengi ,miaka yote nyuma kilikuwa hakioneshi cheche..tunashukuru vijana mliochukua madaraka baada ya wazee...MTEI NA BOB MAKANI....miaka hii mitano tumeona mnapanuka na kuwapa matumaini wananchi kwa kasi ya ajabu .....sasa kwanini mnafikia kuja kuvuana nguo hapa....mmekosa vikao...

kwanini CHADEMA mnataka kuwasaliti watanzania??/

ni CHAMA gani hakina siri za ndani??? haata ndoa ina siri....na siri ni siri..???...miliosoma vitabu vya siasa mnajuwa ...wanachowashinda CCM ndio hicho...?? watu wao wameapa kutunza siri...hata waulizeni waliokuwa humo..watawambia...

chukulia mfano wa mtu kama MREMA ..Pamoja na uropokaji wake ...mambo aliyoyajuwa kwa kiapo ambayo anajuwa akiongea itakuwa kinyume hajapata kuyasema..nasema hivyo kwa sababu kuna mengi tumepata kumuuliza..anazungusha...!..anajuwa maana ya siri na adhabu ya kutowa siri anaijuwa!

Tena wapinzani mjuwe ikiwa umeenda ccm unaweza kuongea porojo zote lakini ukisema siri ambayo imekuwa rated secret...simply they kill you!!! mifano mnayo...!!!...sitaki wapinzani mfikie huuko lakini lazima mjuwe hamtakiwi kukwaruzana na kuwayumbisha wananchi namna hii......

CCM waanajuwa kuwagombanisha .....na wanaofanikiwa huzawadiwa vyeo lakini tayari wanakuwa wameshajiaharibia historia na kubeba usaliti...

watu kama ....lamwai,hizza,akwilombe.,kaborou[aliyekuwa kipenzi cha wananchi]....leo hii wakitokea mbele ya wananchi hata wanaona haya ...ukiachilia mtu kama hizza ambaye anajulikana ni mpiga domo...hawa wasomi wengine...dhamira zinawasuta....na tayari wamekosa uhalali mbele ya macho ya watu!!

....tunaomba vita dhidi ya ufisadi isitumike vibaya kuyumbisha wananchi...narejea maneno ya POLYCAP CARDINAL PENGO.."wanaopingana na ufisadi lazima wajiulize wanapigana toka moyoni au wanapigana kwa kuwa tu na wao wamekosa fursa ya kuwa mafisadi....""

CHADEMA MSIKUBALI KUTUMIWA NA MAFISADI AU HATA HAO MAKAMANDA WA MAFISADI...KWANI WANANCHI WOTE WANAJUWA NYIE NDIO WAAZILISHI WA HII VITA....MBOWE .,SLAA,...ZITTO NA WABUNGE WOTE WA CHADEMA ....SASA IWEJE LEO MNAKUBALI KUWA UNDERDOGS......ITAKUWA NI FURAHA SANA KWA MKIFARAKANA KAMA HIZI...NAPATA PICHA WANAKUNYWA MVINYO SASA.......

MSITUPELEKE HUKO!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom