Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Selous!Duh, Zitto haya ungemezea ingekuwa powa sana. Anyway akina Makamba ndo usiseme. Hapa wakulaumiwa ni wewe na Slaa kama sikosei. Anyway sijui katiba yenu inasemaje ila simply kuna UFISADI CHADEMA. Kesho magazetini watakunukuu.
Eehh, Malizeni halafu Zitto usisahau kuangalia pia friends and advisors wako. at this stage you should have advisors in sectorial. Your future is bright and people especially your friends wanakutumia kama ngazi. si kwa matakwa yao ila kwa priorities zao. Review wote ikiwezekana piga wote chini. Katika kipindi cha miaka mitatu hii wakubomoa ila naamini umejijenga wewe binafsi. cheki ishu ya DOWANS, kugombea tena ubunge, afrika mashariki na sasa uenyekiti. People have these in their mind. they will judge you.....Hizi siasa za upepo ni kwasababu tu watu wamechoka ila zikija siasa za kimarekani utakuwa kama vumbie, waaa haupo.
Mimi binafsi nakuelewa but tusifikishane kutoelewana.
Ndugu zangu,
Katika kipindi hiki sikutaka kabisa kuingia na kujibu hoja yeyote ndani ya JF kuhusiana na uchaguzi wa vijana Taifa. Hata hivyo mtaniwia radhi kujibu hili ili kuweka rekodi sahihi kutokana na upotoshaji ambao unafanyika kwa makusudi kabisa ili kushusha heshima yangu katika jamii.
Moja, mimi ni mumbe wa Baraza la Vijana la CHADEMA kwa nafasi yangu ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu wa kuchaguliwa kuwakilisha vijana na nikiwa Mbunge mwenye umri wa ujana (miaka 33). Hivyo kushiriki kwangu kwenye vikao ni jambo la kawaida kabisa kwani nina haki ya kupiga kura. Vile vile nina haki ya kuamua mgombea gani wa kumuunga mkono katika uchaguzi. Niseme waziwazi kuwa David Kafulila ndiye mgombea niliyemwunga mkono na kumfanyia kampeni waziwazi bila kificho chochote kile. Hii inatokana na tabia yangu ya kutokuwa mnafiki. Nilimwunga mkono David Kafulila na alishinda kwa kupata kura 99 dhidi ya kura 73 ambazo alipata mgombea mwingine John Heche ambaye alikuwa anaungwa mono na kundi lililonipinga kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Huyu aliyeandika post hii ni mmoja wa vijana wa makao makuu ya CHADEMA ambaye amekuwa akinipinga siku zote kwa chuki tu ya kuwa mimi nimepaata umaarufu wa kisiasa kuliko yeye na kundi lake.
Mama yangu mzazi ni mwanachadema. Ni kiongozi mwandamizi wa CHADEMA kutoka mkoa wa Kigoma na amekuwa msaada mkubwa wa chama katika Manispaa ya Kigoma. Ninaomba sana masuala yangu ya kisiasa na mahasimu wangu wasimhusishe mama yangu mzazi. Ninaomba sana sana mumuweke mama yangu pembeni. Mwandishi wa post hii tafadhali naomba usimhusishe mama yangu na tofauti zetu za kisiasa. Ninaomba sana hili liheshimiwe.
Pili, ni dhahiri kulikuwa kuna makundi katika uchaguzi wa BAVICHA. Mimi niliweka wazi msimamo wangu wa kumwunga mkono kafulila. Wakurugenzi wa Makao makuu ya chama kuanzia Katibu Mkuu mpaka wakurugenzi kama John Mnyika, John Mrema na hata maafisa kama Halima Mdee walikuwa wanampinga David Kafulila. Hawa wanaogopa uwezo wa Kafulila wa kukataa kutumika na kuwa independent katika maamuzi yake.
Hii sio mara ya kwanza kwa Kafulila kuzuiwa haki yake. Kijana huyu alipitishwa kugombea Ukurugenzi wa vijana na jina lake kwenda katika Kamati Kuu. Ajenda ya uteuzi wake ikasitishwa baada ya kuhofia kuwa atashinda. Mtindo huo huo wameutumia sasa kufuta uchaguzi na kuupeleka mbele mpaka baada ya miezi 6. Mimi nimekataa
1. Uchaguzi umefanyika.
2. Matokeo hayakutangazwa
3. Hakuna aliyekata rufaa
Hivyo, wazee wanapata wapi 'locus' ya kufuta uchaguzi?
Hata hivyo wenye mamlaka ya kufuta uchaguzi ni Kamati Kuu ya chama maana kuna taratibu za rufaa ndani ya chama chetu. Nimetaka Kamati Kuu iitishwe ili taratibu zifuatwe.
Huyu mtu aliyeleta post hii hapa anataka kuspin ili kupinda ukweli bila aibu.
David Kafulila kashinda round ya kwanza zaidi ya 50%. Wamekataa kutangaza matokeo na kuleta fujo kwenye mkutano.
Kuna tuhuma dhidi yangu kuwa nimetoa rushwa. Huku ni kutapatapa kwani tuhuma hizi zinatolewa bila ushahidi. Hivi huyu mwandishi na akili zake timamu anaweza kuweka akilini kwake kuwa mimi naweza kutoa rushwa hadharani? Eti nimevuta kiti na kuita watu kutoa rushwa. Bila adabu anamhusisha mama yangu mzazi.
Mama yangu ana maamuzi yake binafsi na mfano dhahiri ni uchaguzi wa chaha wangwe ambapo mimi nilimwunga mkono arfi na yeye akamwunga mkono Chacha wangwe waziwazi na bila kificho.
Uchaguzi wa vijana haukua na rushwa. Uchaguzi wa vijana wa chadema umefanyika kwa amani kabisa na matokeo hayakutangazwa kwa kuwa mgombea 'wao' hakushinda.
Wanasema eti Mtemelwa aliyekuwa ananiunga mkono alishindwa Temeke. Hawasemi watu waliowatuma kwa kutumia fedha za chama kugombea mikoa 15 na kutupwa chini na watu wanaoniunga mkono. Ukiwemo mkoa wa Dodoma na Shinyanga ambao walitumwa wakurugenzi wa chama kama Benson Kigaila na Erasto Tumbo na kushindwa. Habarindiyohiyo nakuomba ukumbuke kuwa baada ya uchaguzi kinachofuata ni ukaguzi wa fedha za chama katika kipindi hiki na jinsi zilivyotumika. Nashukuru Mungu kuwa ukaguzi huo sasa utafanywa na CAG
Katika spirit ya umoja na mshikamano wa chama tutamaliza suala hili katika Kamati Kuu ya chama.
Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.
Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.
Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!
Haya ambayo nimeyaandika hapa JF nimewaambia vijana hawa 'face to face' ili waache uwongo, uzandiki, majungu, fitna na chuki.
Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.
Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.
im failing to believe that wewe ni zito im sure sio wewe kama ni wewe basi huu ndo mwisho wako kisiasa na kweli hela za mafisadi zimekukolea baba,asante sana,sasa tusubiri mkombozi wa nchi hajachaguliwa,huna maana hata kidogo,sikutegemea km maneno haya ni yako,well if sio wewe samahani kwani humu ndani waeza watu kuingia kama wewe,so please jitokeze magazetini na everywhere uukane upuuzi huu,laa unaangamia kisiasa baba!unafulia taaaratibu kama mbatia
Nina mashaka kama Post hii kaandika Zitto mwenyewe ninayemfahamu. Nahisi kuna mtu ana Password yake ndio kaweka haya maneno hapa.
Ila kama niyeye mwenyewe na hajapiga mvinyo (NAJUA HUU NI MWEZI MTUKUFU) basi something wrong somewhere.
Mkuu Zitto, hakika hii inakuondolea sifa ya Kugombea Uenyekiti automatic yaani hufai!..maelezo yako ni dhahiri yanaonyesha wazi huna Hekima wala Busara kuongoza chama, kifupi hujakomaa kisiasa kabisaaa. Una papara, mwenye hasira na mwepesi kuropoka..Mkuu hukutakiwa kabisa kubwabwaja ovyo hapa kijiweni maneno haya kwani yanazidi kukufunga wewe ikiwa umeshakubali kujitoa ktk kugombea.
Maneno haya yalitakiwa kutangulia na hasa siku ya kikao cha chama. Na nakuomba sana ktk mkutano mkuu wa chama hii September, zungumza yote yaliyoko moyoni mwako, kuwa muwazi, mkweli na bayana tuhoji utendaji kazi wa hao wazee ama watu ambao unawafahamu kuhusika na mbinu hizi chafu za kupakaza.
Kulitumia jina la wangwe na uchafu wote mlofanya dhidi yake hakika umenichefua kichizi yaani kumbe kweli Zitto mlimfanyia Wangwe roho mbaya makusudi?..Hukuona ubaya wa kutenda ulotenda Ukajisafisha hadharani hadi siku ambayo umetendewa wewe ndipo unakuja na habari hizi za Wangwe tena ktk gazeti!..
Well itakuwa vizuri ukimalizia kabisa kutufahamisha maanake hakuna kitu ambacho sisi wananchi tunataka kuelewa zaidi ya Kifo CHA WANGWE kama kuna mkono wa mtu..Ikiwa wewe mkweli na unataka tukuamini basi tueleze yote mlomtendea Marehemu Wangwe ambayo wewe mwenyewe unakiri na ulikwenda simama mbele ya maiti na Kutubu..What real happen? wewe mwenyewe pamoja na Bi Asha ,mlifanya nini au mlicheza part gani mkuu come clean leo hii hapa hapa JF.
Duh, ama kweli mkuu wangu najua ulikuwa na haki ya kugombea kiti hicho lakini leo hii na maelezo haya yaonyesha wazi kwamba hufai kabisa... Na wala usije fikiria kuwa Wangwe alikuwa mtu mzuri vile vile..ila kwa walalahoi wasojua kwamba a sneetch ni Liability ktk taasisi yoyote na hafai kabisa..isipokuwa kwetu sisi Ndivyo Tulivyo (Watumwa wa akili), kumbe ktk jumuiya kama zetu nchi za nje watu hawa hamalizwa vibaya vibaya na hawapokelewi mahala popote.
Kifupi Zitto hakuna sifa hata kidogo unapokipaka chama chako na sidhani hata ukiondoka ama kwenda chama chochote utapokelewa kwa mikono miwili, laa utatumiwa tu na hakuna mtu wala chama kitakachokuamini. Watu kama Wangwe na wewe ni wa kuogopwa na kukaliwa mbali sana na sii kwa sababu unasema ukweli wako ila Mropokaji ni Liabiility ktk chama..Usifikirie unajenga mkuu wangu yaani duh! ama kweli Umri ni moja ya kigezo kikubwa sana ktk CV ya mtu..
duh zitto kwa uhakika tu na kama unaelewa huu ndo mwisho wa kuvuma kwako,nadhani umri unakuponza kichwa kikakua,sasa unaleta vurugu katika chama na wala hauleti uelewano,wewe kama kiongozi wa juu na mwenye akili na mtaka mageuzi hukupaswa kwanza kuwa na MAKUNDI sasa,unataka kutuambia ungeshinda uenyekiti ndo ungefanyaje?ungeadhibu wale usiowapenda then chama kinadhoofika,wewe kwa ufupi huwezi madaraka,hufai kabisa,kama umepewa hela kuharibu demokrasia si useme?
This is why CCM will always win in every election for many years to come.This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.
Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.
Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!
Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.
To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?
Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.
Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.
This is why CCM will always win in every election for many years to come.
CHADEMA is going down. And this time, it is going down for real and it is, because you leaders have chosen so. Wallah, wakati mnakua ndio mnapoanza kufifia? Every five years, we see new party arising and then slwly dying.
Mimi mara zote nimekuwa nikiamini kuwa chama mbadala katika nchi hii kinaweza (japokuwa kwa mbaaaali) kuwa CHADEMA. With this development, I wonder if the dream will ever come true. It is your party, Sir. Kill it if you want. And trust me, this is exactly how to do it.
Mkuu naomba kuuliza maswali madogo tu. Hivi ndani ya CHADEMA kama mgombea mmoja akidhulumiwa au kuhujumiwa katika uchaguzi hakuna taratibu za kufuata (ikiwemo kukata rufaa) ili kuhakikisha anapata haki yake? Na je, wewe kama kiongozi mkubwa kabisa ndani ya CHADEMA, hukuweza kutumia uwezo wako kuhakikisha mtu huyo anapata haki sahihi kwa kufuata kanuni sahihi za chama na hata kuweza kuona wanaohusika kuminya haki za mwanachama huyo wanachukuliwa hatua? Je, kama yote hayo hayakuwezekana, unadhani chama kina uwezo wa kuhakikisha yanawezekana katika siku chache zijazo?Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.
Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.
Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.
Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.
zitto duh! what a dissapointment!
yaani unakubali kuwa ulikuwa mmoja wa waliomzulia uongo chacha wangwe , kisha unakuja hapa unaropokwa!
ndio tukuone mwema sana kwa kuwa leo umesema ukweli baada ya kuzuliwa na wewe?
hufai kabisa kuwa katika siasa, kwa sababu hikma kwako ni sufuri......hata kama ulimzulia wangwe na umejutia, ulitakiwa uingie nalo kaburini.....kulisema hapa LEO hakusaidii chadema, hakukusaidii wewe wala wanachama wa chadema.
kisha unatoa shutuma kuwa chadema kuna ukabila pia ( rejelea maneno yako kuhusu nipashe,ippmedia na machame na mtei) .....
hivi hasa lengo lako ni nini pale unapoandika?
MkamaP,Hakuna cha mwisho
hao wanaoandika humu na kuleta habari ni viongozi wa juu wa chadema,ama kosa la kuisha kwa Zitto ni kujisajiri kwa jina lake halisi.?
Haishi mtu ukweli lazima tuuseme ukweli ,hakuna cha siri hizi siri mnazoongelea ni hizo za staili ya kumpoteza Wangwe ama siri zipi?
yawezekana kuwa zitto na kundi lake walitaka wachukue uongozi kamili wa chama.
zitto uenyekiti na wafuasi wake Baraza la wazee na Baraza la Vijana ili labda waendeshe chama kidemokrasia LAKINI njia walizotumia sizo!
wamesababisha vurugu la hali ya juu ndani ya chama, na badala ya kufanya damage control, ndio kwanza anakuja hapa anatuhadithia alivyomfanya chacha wangwe na kuzidi kukipaka matope chama kuwa kuna ubaguzi!
hivi zitto ulijitoa kugombea uenyekiti kwa kuwa ulete umoja ndani ya chama kweli? kwa sababu hii kuropokwa siri za chadema hapa JF hakuonyeshi kutafuta umoja, kunaonyesha kubomoa tu
Tumehuzunishwa sana na Makundi ya wakina Zitto na wenzake, Mambo kama haya yaishie ndani sio humo ndugu zangu. Hivyo kuna haja ya wakini Zitto kuwa makini na vitu na ngoma inayovuma kama hiyo wangalie isjie kupasuka..Maana kama watu wanashindwa kuwa makini sasa watu walio nje wataonekana vipi??MkamaP,
Mkuu tumesha elezwa kwamba mwandishi ni mmoja wa viongozi wa Chadema, sikushangaa wala kusikitishwa zaidi ya kusoma na kuelewa kinachoendelea.. hakutajwa jina la mtu wala watu wala habari za vifo..
Mkuu wapo wengi tunawafahamu humu JF kuwa ni viongozi wa Chama Chadema au hata CCM wamo humu kwa majina ya bandia.. Ifahamike tu kwamba JF wapo watu wa kila aina na baadhi tunafahamu iwe wanatumia majina yao au bandia tunawajua vizuri tu.
Sisi sio watoto wadogo mkuu wangu tunaweza kuchambua pumba toka ktk mchele tena kwa kupeta tu..Pumba zitamwagika ardhini na mchele kubakia ktk ungo.. ndio JF inavyofanya kazi zake.
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania WoteMkamaP,
Mkuu tumesha elezwa kwamba mwandishi ni mmoja wa viongozi wa Chadema, sikushangaa wala kusikitishwa zaidi ya kusoma na kuelewa kinachoendelea.. hakutajwa jina la mtu wala watu wala habari za vifo..
Mkuu wapo wengi tunawafahamu humu JF kuwa ni viongozi wa Chama Chadema au hata CCM wamo humu kwa majina ya bandia.. Ifahamike tu kwamba JF wapo watu wa kila aina na baadhi tunafahamu iwe wanatumia majina yao au bandia tunawajua vizuri tu.
Sisi sio watoto wadogo mkuu wangu tunaweza kuchambua pumba toka ktk mchele tena kwa kupeta tu..Pumba zitamwagika ardhini na mchele kubakia ktk ungo.. ndio JF inavyofanya kazi zake.
Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
...haya na leo napata kali zaidi zitto nae na mamaake ndani,hiki chama nadhani ni saccos
Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.