Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
Kama wanashindwa kuwa na Hekima tutawafundisha, maana wanapotaka kwenda huko siko kuzuri sana, Kuna haja ya kuwa na Hekima kubwa sana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mwakani, Majeraha yoyote yale wanaweza kutumiwa na CCM na Kuharibu sifa ya CHADEMa ambao wao wameijenga kwa muda mrefu sana. Sasa kama wao wanashindwa tutawaelekeza cha kufanya katika hekima na Busara zote na Sio hivi kama wao wanaenda sasa hiviWakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
Zitto arudi kwa wenzie aombe radhi kwa kuleta details zao huku JF halafu waanze upya. It is not too late jamani. We can still win!!!
JF ni sehemu ambapo tunaongea kwa uwazi, hatumfichi mtu kwa hilo zitto hajakosea. Kama kuna anayelalamika kwa kusemwa humu JF naye amwage hapa nyanga zake tuzichambue.
Na Tena sasa naona kama Busara wanazidi kukosa. Tutawafundisha kwa maslahi ya Tanzania na CHADEMA. Ni vitu vya aibu sana kuona mambo kama haya katika wakati kama huu muhimu sana kwa CHADEMA.Wakini Zitto inapaswa kuvunja makundi yao haraka sana kwa faida ya chama na Watanzania Wote
Umesema kweli kabisa kwa sababu Zitto anaweza kuyaona makosa upande wa pili tu lakini yeye kashindwa kutazama jinsi watu wake wanavyopiga kampeni chafu against chama..Ebu someni habari aloandika zote hapa kisha tudini mkasoma kule - Kitabu cha Wangwe chaanika Ukweli tunaotakiwa kuujua.
Moja kwa moja utagundua kwamba hizi habari zinatoka ndani ya Chadema na sio CCM.. kisha utaanza kujiuliza tunakwenda wapi na how bad things are! yaani demokrasia ni nguvu na uwezo wa mtu kugombea nafasi ya Uongozi jamanai.. Hivi kweli mama Migiro alichukua form kugombea nafasi yake au alipendekezwa kwanza! Kina Salim wakati wa UN walipigwa vita lakini uume ni kuvumilia na kuanza upya .. Malecela jina lake lilienguliwa ktk kugombea Urais, Salim alinyimwa kura kurudiwa mara tatu, yote haya ni machafu ya siasa, huwezi sema haikutumika Demokrasia kwa sababu tu mtu fulani hakuhusishwa kutokana na mapungufu yake..Kuenguliwa jina la mgombea kutokana na mapungufu yake ni sehemu ya Demokrasia inayozungumziwa..
Kukomaa kwa mtu kisiasa ni uwezo wa kutambua yote haya, kuweka maslahi ya chama mbele ya maslahi binafsi, na yale ya Taifa mbele ya maslahi ya chama.
Ukweli unaoanikwa hapa ni kuonyesha wagombea wote wanathamini maslahi yao binafsi mbele ya chama..Ufisadi sio Uporaji na wizi pekee ila ni pamoja na uharibifu kama huu.
Mkandara hueleweki kosa gani Zitto kafanya? Robin Cook aliyekuwa waziri wa nje wa Labour aliweka wazi uozo wa Chama chake kwenda Iraq.soma ROBIN COOK THE POINT OF DEPARTURE ISBN 0-7432-5255-1
plz mwache Zitto yeye wamemzuia na mgombea wake kazuiliwa haki iko wapi?
soma maelezo yake kasema kuna kundi lililofanya hila asiwe Mwenyekiti Taifa. tafrisi nyepesi kazuiliwa huna haja ya kuuliza swali hili.Zitto amezuiliwa au kajitoa?
Pole sana ndugu yangu. Naelewa feelings zako na za wengine humu ndani. Ninawahakikishia kuwa tutainuka, tutajipakusa vumbi na kukimbia tena pamoja. Mchakato huu waweza kuwa na matokeo ya kukikuza na kukikomaza chama sana. Tunajifunza katika changamoto hizi. Hatuwezi kukubali kuingia katika historia ya kuua CHADEMA. Kuna masuala fulani fulani ya msingi kabisa kuhusu mahusiano yetu na marafiki zetu ambayo lazima tuyashughulikie asap.
Deep in my heart i believe truth will prevail and the party will come up strong.
soma maelezo yake kasema kuna kundi lililofanya hila asiwe Mwenyekiti Taifa. tafrisi nyepesi kazuiliwa huna haja ya kuuliza swali hili.
CHADEMA haiendi kokote mkuu.
Mkuu kwani kwenda Iraq ilikuwa mbinu ya chama against huyo Robin Cook?Mkandara hueleweki kosa gani Zitto kafanya? Robin Cook aliyekuwa waziri wa nje wa Labour aliweka wazi uozo wa Chama chake kwenda Iraq.soma ROBIN COOK THE POINT OF DEPARTURE ISBN 0-7432-5255-1
plz mwache Zitto yeye wamemzuia na mgombea wake kazuiliwa haki iko wapi?
Mkuu naomba kuuliza maswali madogo tu. Hivi ndani ya CHADEMA kama mgombea mmoja akidhulumiwa au kuhujumiwa katika uchaguzi hakuna taratibu za kufuata (ikiwemo kukata rufaa) ili kuhakikisha anapata haki yake? Na je, wewe kama kiongozi mkubwa kabisa ndani ya CHADEMA, hukuweza kutumia uwezo wako kuhakikisha mtu huyo anapata haki sahihi kwa kufuata kanuni sahihi za chama na hata kuweza kuona wanaohusika kuminya haki za mwanachama huyo wanachukuliwa hatua? Je, kama yote hayo hayakuwezekana, unadhani chama kina uwezo wa kuhakikisha yanawezekana katika siku chache zijazo?Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.
Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.
Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.
Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.
Sijui kama kuna dalili za kupona. Maana naona leo moto mpya umewashwa na kuuzima itakuwa gharama kubwa sana.
Mzimu wa Wangwe waiandama CHADEMA...Zitto,wat happened to Wangwe!??Naona katika kuporomoka kwako umeamua "kufa" na wengi.Politicians!
Sasa mbona kunakuwa na malumbano kama haya jamani??Zitto amezuiliwa au kajitoa?