Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Walimtenda nini?au na wewe uko katika lile kundi la kuogopa wafu? yeye alisema walimtenda kisiasa kumzima! kuwa anachukua hela CCM!!!

Yeye naye wanamfanyia the same thing, huoni anajikwepesha , huwa hauangalii movies kuwa majambazi wanaweza kukosana na kuweka wazi kila kitu??

This is good! inabaki kuwa ni somo kwetu wote kuwa tuangalie vitu in 3D, mTEI KUSEMA KUWA ccm WALIPENYEZA FEDHA SI KWELI; NANI HUYO, KIJANA GANI ALIYEKAMATWA NA CCM? huoni wanakibariki kuwa ni chama cha kikabila zaidi na Zito ameliona hilo, amekasirika! alijua yuko nao pamoja kumbe wako ng'ambo mbili tofauti

In politics you better be open sometime, walichofanya CHADEMA HAIINGII AKILINI, kuwa ajitoe ,mgombea awe mmoja! wakati wanalia demokrasia!

Zito alisema kama kujitoa wajitoe wote! which was good

Msaidieni huyo, mpeni moyo, hawa wapiganaji wasipotiwa moyo, tutaandika post kama hizi humu maisha yetu yoooote bila kuona mabadiliko!

Mtei mbona karopoka kwenye vyombo vya habari , au wewe unaona JF iko TZ nzima?

Or who is perfect??

Chadema ina wanachama wengi na sio Zitto peke yake. Kama Zitto anakipenda Chadema, basi natumaini atamuunga mkono yeyote yule atakayepewa nafasi ya uenyekiti wa chadema.
 
Mkuu hii sio movie..kinachoendela ktk uchaguzi mkuu sio sinema kabisa ila uharibifu wa wazi wazi..kama nzige walioingia shambani..
Kinachozidi kuharibu ni nyie Wapambe wake. Imefikiam sasa hivi mnaubeba msalaba kwa niaba yake na wakati huo huo kundi jingine linajikita kumharibia jina zaidi. Kifupi mkuu wangu hamkitendei mazuri chama hata kidogo.. Kama kuna vita ya Uongozi ndani ya Chadmea iwe Ukabila au Udini au lolote lile. Sehemu ya kuweka wazi mambo haya ni ktk mkutano huu.
JF haiwezi kumsaidia mtu ila inaweza kumtangaza mtu au kumharibia mtu pasipo ukweli kuwa wazi. Kama wewe unamuunga mkono Zitto kwa yote yanayomtokea basi itakuwa bora uwakilishe hoja hii ktk kikao na ijadiliwe kwa Uwazi bila kuficha hisia zenu hata kaa zinamhusu mzee Mtei mwenyewe..I would love to know the truth maanake tunasikia tu Chadema ni chama cha Ukabila, Udini na kadhalika lakini hatuna uhakika.. Sasa fikiria wananchi tuje kichagua chama ambacho viongozi wake wanabeba Takaba hizo rohoni..

Mkuu hii ndio huwa tunaita busara! Asante mkuu ubarikiwe
 
Wanapaswa kushauriwa haraka sana maana sasa naona kama vile anaenda kwa maamuzi yake mwenyewe. Inakupaswa kushauriwa kwanza na sio kama alivyofanya yeye

ninawaonea huruma akina Prof. Baregu, Lwakatare na watu wazima wengine wenye busara zao, wanaoshuhudia hili scamp kwa macho yao.
 
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi.
Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha.
Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.

Walimtenda nini?au na wewe uko katika lile kundi la kuogopa wafu? yeye alisema walimtenda kisiasa kumzima! kuwa anachukua hela CCM!!!

Yeye naye wanamfanyia the same thing, huoni anajikwepesha , huwa hauangalii movies kuwa majambazi wanaweza kukosana na kuweka wazi kila kitu??

This is good! inabaki kuwa ni somo kwetu wote kuwa tuangalie vitu in 3D, mTEI KUSEMA KUWA ccm WALIPENYEZA FEDHA SI KWELI; NANI HUYO, KIJANA GANI ALIYEKAMATWA NA CCM? huoni wanakibariki kuwa ni chama cha kikabila zaidi na Zito ameliona hilo, amekasirika! alijua yuko nao pamoja kumbe wako ng'ambo mbili tofauti

In politics you better be open sometime, walichofanya CHADEMA HAIINGII AKILINI, kuwa ajitoe ,mgombea awe mmoja! wakati wanalia demokrasia!

Zito alisema kama kujitoa wajitoe wote! which was good

Msaidieni huyo, mpeni moyo, hawa wapiganaji wasipotiwa moyo, tutaandika post kama hizi humu maisha yetu yoooote bila kuona mabadiliko!

Mtei mbona karopoka kwenye vyombo vya habari , au wewe unaona JF iko TZ nzima?

Or who is perfect??

Mkuu nimeweka alichosema Zitto kwa ajili ya reference. Naomba usome tena. Hilo swali unalouliza ingefaa aulizwe Zitto ndo anajua walichomtenda.
 
Kama uko upande wa Zitto na haya ndiyo unaandika, basi umethibitisha kuwa Zitto anatafuta pa kutokea ili aende chama la kijani.
kwanini aondoke Zitto na Mbowe abaki? Zitto yupo na atakuwepo lazima Change ipatikane Chadema itakuja Change chini ya Zitto.
Mwanakijiji naona hachangii kwenye mambo haya ya Chadema au hayupo hewani?
 
kwanini aondoke Zitto na Mbowe abaki? Zitto yupo na atakuwepo lazima Change ipatikane Chadema itakuja Change chini ya Zitto.
Mwanakijiji naona hachangii kwenye mambo haya ya Chadema au hayupo hewani?

Ha ha haha , Yaani hapa imebidi nicheke tu. Kwani tena hapa imeshakuwa ni ugomvi kati ya Zitto na Mbowe? Kwa nini ikisemwa kuwa Zitto aondoke basi inamaanisha Mbowe abaki?

Kwa nini isiwe Mtei, Makani, Slaa, Mnyika, na wengineo wabaki?

Hayo ya kutaka Mwanakijiji achangie hapa yanaonyesha jinsi ulivyo.
 
Mkuu, inatia faraja kuwa bado una imani kuwa chama chako kitaweza kuendelea kuwa imara hasa baada ya mambo hayo yaliyotokea na kufikia umma kwa njia ya magazeti na JF.

Kuna vitu vitatu ambavyo nahisi ingefaa kuwa itikadi yenu ndani ya chama. Uvumilivu, kuheshimiana na kulinda siri za chama chenu. Katika siasa (najua unafahamu sana tu), mambo hayo matatu hapo juu ndio silaha ya ukweli kwa mwanasiasa na kwa chama cha siasa popote duniani. Tafadhalini fahamuni kuwa umaarufu wa chama chenu umetokana na mambo hayo ambayo yalianza kuonekana, na sasa yanafifia kwa haraka. Kupanda mlima, ni kazi kuliko kushika. Maana unaweza kushuka kwa kujiachia tu.

Mkuu, ningependa ukaiga wanasiasa mashuhuri wa ndani na nje ya nchi. Wanasiasa ambao kwa uvumilivu na subira zao wamefanikiwa na kudumu kwa muda mrefu sana kwenye siasa. Ukiweza kufanya hivyo, si tu kuwa utakomaa kisiasa, bali pia utakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa jamii unayotaka kuihudumia. Nahofia kuwa wanasiasa wengin kutokana na kutokuwa wavumilivu, wamekuwa "POPOCORN POLITICIANS". Wanajitutumua kwa muda mfupi, mpaka wanapasuka halafu wanakuwa exposed inside out na kuishia kuwa useless. Ni hasara sana kutumia muda mrefu kujijenga kisiasa na baadae kuisha kiurahisi.

Mbona ccm wanapolinda mambo yao mnawashambulia??

Huu sasa ni uhuni
 
Mwanakijiji naona hachangii kwenye mambo haya ya Chadema au hayupo hewani?
Wakuu,

Mwanakijiji nimewasiliana naye ana issue flani nyeti anaifanyia kazi, hizi issues zote anazisoma lkn kwa sasa tumpe muda aweze kukamilisha analolifanya mida hii.

Kumradhi sikuwafahamisha, ni kwakuwa sikuona anayemwulizia
 
Ha ha haha , Yaani hapa imebidi nicheke tu. Kwani tena hapa imeshakuwa ni ugomvi kati ya Zitto na Mbowe? Kwa nini ikisemwa kuwa Zitto aondoke basi inamaanisha Mbowe abaki?

Kwa nini isiwe Mtei, Makani, Slaa, Mnyika, na wengineo wabaki?

Hayo ya kutaka Mwanakijiji achangie hapa yanaonyesha jinsi ulivyo.
Zitto aliomba nafasi akishindana na Mbowe sio hao uliwataja hao wanamwakilisha Mbowe.
 
Wakuu,

Mwanakijiji nimewasiliana naye ana issue flani nyeti anaifanyia kazi, hizi issues zote anazisoma lkn kwa sasa tumpe muda aweze kukamilisha analolifanya mida hii.

Kumradhi sikuwafahamisha, ni kwakuwa sikuona anayemwulizia
Asante kwa hekima yako sio kama huyu aliyenijibu huko juu.huyu jamaa ameshindwa kuelewa kuwa Top five wa jamii Forum ni Mwanakijiji.
 
Zitto aliomba nafasi akishindana na Mbowe sio hao uliwataja hao wanamwakilisha Mbowe.

Hao ni wana chadema kama alivyo Zitto. Yeye ni mtu mmoja tu kati ya mamilioni ya wana Chadema. Hayo mengine ni fixation zako kwa mtu mmoja badala ya chama.
 
Asante kwa hekima yako sio kama huyu aliyenijibu huko juu.huyu jamaa ameshindwa kuelewa kuwa Top five wa jamii Forum ni Mwanakijiji.

Sasa kama Mwanakijiji ni top five then what .... wanachama wengine wote wajifungie uvunguni ili kupisha top five?
 
Wakuu,

Mwanakijiji nimewasiliana naye ana issue flani nyeti anaifanyia kazi, hizi issues zote anazisoma lkn kwa sasa tumpe muda aweze kukamilisha analolifanya mida hii.

Kumradhi sikuwafahamisha, ni kwakuwa sikuona anayemwulizia

Mkuu kwa bahati mbaya hukuweza kupitia thread hii https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/37697-yuko-wapi-mzee-mwanakijiji.html. Mwanakijiji hawezi kusahaulika au kutouliziwa ktk wakati mgumu kama huu. Asante kwa taarifa.
 
Sakata hili linanikumbusha mpambano wa Nyerere vs Sykes enzi za TAA/TANU!
 
Mkuu hii sio movie..kinachoendela ktk uchaguzi mkuu sio sinema kabisa ila uharibifu wa wazi wazi..kama nzige walioingia shambani..
Kinachozidi kuharibu ni nyie Wapambe wake. Imefikiam sasa hivi mnaubeba msalaba kwa niaba yake na wakati huo huo kundi jingine linajikita kumharibia jina zaidi. Kifupi mkuu wangu hamkitendei mazuri chama hata kidogo.. Kama kuna vita ya Uongozi ndani ya Chadmea iwe Ukabila au Udini au lolote lile. Sehemu ya kuweka wazi mambo haya ni ktk mkutano huu.
JF haiwezi kumsaidia mtu ila inaweza kumtangaza mtu au kumharibia mtu pasipo ukweli kuwa wazi. Kama wewe unamuunga mkono Zitto kwa yote yanayomtokea basi itakuwa bora uwakilishe hoja hii ktk kikao na ijadiliwe kwa Uwazi bila kuficha hisia zenu hata kaa zinamhusu mzee Mtei mwenyewe..I would love to know the truth maanake tunasikia tu Chadema ni chama cha Ukabila, Udini na kadhalika lakini hatuna uhakika.. Sasa fikiria wananchi tuje kichagua chama ambacho viongozi wake wanabeba Takaba hizo rohoni..
Binafsi naona Kosa la Zito ni kuanika Siri za Chama hadharani(JF),ndo maana anashambuliwa kama mpira wa kona.Pia ikumbukwe kwamba mara baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA na kujitoa mengi mabaya juu yake yamesemwa hadharani ambayo kwa namna moja ama nyingine yamemchafua machoni mwa jamii(tuhuma kama anatumiwa na mafisadi,mtoa rushwa nk),na mbaya zaidi baadhi ya tuhuma hizi zilikuwa zikitolewa na viongozi/wazee wa CHADEMA...Zitto aliona kila mtu anamtenga/anamuona msaliti,kwamba jambo lolote baya litakaloitokea CHADEMA yeye ndo ataonekana chanzo..So ili aisulubiwe peke yake akaamua kumwaga ukweli wa yote yaliyo nyuma ya pazia hapa jamvini(Watoto wa mjini wanasema,wewe ukimwaga ugali mi namwaga mboga,ngoma inakuwa droo),mambo ambayo kimsingi yalitakiwa yabaki kuwa ni siri ya chama,hayakutakiwa kutoka nje...Zitto wewe ni mwanasiasa mzuri sana ndugu yangu,cha msingi punguza jazba,ukiendelea na jazba hautafika kokote(huu ni mtizamo wangu tu),tafuta washauri wazuri na uwatumie ipasavyo....
 
Last edited:
Mkulu Zitto,

Ni wewe umeandika hayo! Siamini! Naomba Mungu waandishi wanaochukua habari hapa JF wasiione hii, maana wakiiweka kwenye media sijui utapita wapi?

Yaano mkuu unaandika in plural kuwa mlimtenda Wangwe kwenye public from kama hii, kisha ulitaka kuwa mwenyekiti wa chama? Are u kidding us or what?

Okay, sijui imekaaje lakini huoni kama inaweza kuwa activate polisi kufatilia what exactly hapenned?

Yaani unadhani hapa Jf watu watakuona wa maana kwa 'kuropoka' huku ulikofanya? OOh my God, nadhani tulikuwa hatukufahamu vizuri,

na tutajuuuuuuuuuuta kukuufahamu! au mtu kaiba password?

Hili bandiko will go down in history be it your rise or ur fall.

CHADEMA CHADEMA Wangwe yuko wapi?

Hatujui kwani sisi CHADEMA ni walinzi wa WANGWE?

Mbona damu yake yalilia toka udongoni? aaha hatujui hiyo ni siri ya chama .
 
CHADEMA CHADEMA Wangwe yuko wapi?

Hatujui kwani sisi CHADEMA ni walinzi wa WANGWE?

Mbona damu yake yalilia toka udongoni? aaha hatujui hiyo ni siri ya chama .

Ha ha ha ha , lini umehama CCM kwenda Chadema? Au kwa vile Mwakalinga anasuasua kule Kyela?
 
Chadema ina wanachama wengi na sio Zitto peke yake. Kama Zitto anakipenda Chadema, basi natumaini atamuunga mkono yeyote yule atakayepewa nafasi ya uenyekiti wa chadema.
Mkuu,na hili la CHADEMA kuwa na mgombea mmoja wa uenyekiti wa Taifa unalizungumziaje???,si bora Zitto angebaki tu ili kuleta ushindani na kuangalia kama Mwenyekti wa sasa anakubalika miongoni mwa wana CHADEMA badala ya kuwachagulia wana CHADEMA Mwenyekiti(kwangu mimi kitendo cha Zitto kujitoa na kumwacha Mbowe peke yake ni sawa na kuwachagulia wana CHADEMA Mwenyekiti),kuna nini hapa???,ama ndo tunarudi enzi zilee za kupigia kura Sura na kivuli...Inasikitisha sana,demokrasia iko wapi hapa??,CHADEMA kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinatakiwa kiwe mfano wa kuigwa katika suala zima la democracy(Ijitofautishe na vyama vingine ambavyovenyewe na demokrasia ni sawa na mbingu na ardhi)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom