Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.

Mkuu, CCM ni chama tawala wakati CHADEMA ni chama kinachokuwa. Ni matamanio yangu kuwa na chama ambacho kinaweza kuwa na nguvu kubwa kama ilivyo CCM ili kiweze kusaidia kuleta ustaarabu mpya na utawala bora nchini.

Maamuzi ya CCM si tu kuwa yana manufaa au madhara kwa Taifa zima, bali pia hupelekea mabadiliko ya haraka sana katika maisha ya kila mtanzania bila kujali imani yake kisiasa. Ndio maana ni lazima kusema sana endapo CCM (Chama kikongwe kabisa nchini) kinapofanya mambo yasiyoeleweka. Nakuhakikishia Mkuu, hata Kiongozi wa juu wa CCM angefanya aliyofanya Zitto leo hapa, response ingekuwa kama hii au zaidi kidogo.

kwa hiyo ccm ndio model ya chadema?
 
Licha ya sakata hili kutukumbusha mpambano wa (1) Nyerere v Sykes wakati wa TAA/TANU pia unatukumbusha makubaliano ya (2) Nyerere & Kawawa wakati wa Uhuru! Modeli ya 2 ilisaidia sana kuijenga TANU vijijini katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Na Modeli ya 2 ilisaidia kuleta Uhuru japo iliacha hisia kali za chama kutekwa nyara na aliyekaribishwa chamani.
 
Chadema yachafuka,mgombea atishia kuchoma kisu, uchaguzi vijana waahirishwa
broken-heart.jpg
Na Waandishi Wetu

HALI ya kisiasa ndani ya Chadema imezidi kuchafuka baada ya uchaguzi wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha) kuahirishwa kwa miezi sita, huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo (jina tunalo) akitishia kumchoma kisu mwanachama anayeaminika kuwa kambi ya naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe.

Wakati hatma ya uchaguzi huo ikiwa bado njia panda, mizengwe imezidi kutikisa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake baada ya mmoja wa wagombea anayeaminika kuwa upande wa Zitto kunusuruka kung'olewa.

Joto zaidi linaloonyesha hali tete ndani ya Chadema, lilipandishwa na hatua iliyotangazwa jana mchana na katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa ya kuahirisha uchaguzi huo hatua ambayo ilipingwa na Zitto na msemaji wa chama hicho David Kafulila ambao wanataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi na kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), ambacho inasemekana kinafanyika leo.

Wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya uenyekiti wa Bavicha ni John Heche, Dadi Igogo na David Kafulila ambaye licha ya kuwa ofisa habari wa chama hicho, anatarajiwa kuwania ubunge Jimbo la Kigoma Kusini mwaka 2010.

Akitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo jana, Dk Willibrod Slaa alisema uchaguzi huo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo.

“Mimi kama katibu nimeshauriana na kamati ya wazee ya chama nikiongozwa na Mzee (Edwin) Mtei, Bob Makani na Balozi (Christopher) Ngaiza tumeubatilisha uchaguzi huo, hivyo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo,” alisema Slaa.

“Tumeamua hivi kwa sababu kwanza kufanya uchaguzi ni gharama, tunatumia karibia Sh50 milioni ambazo zinaweza kujenga zahanati moja. Jamani hapa tutawaeleza nini Watanzania.

“Wajumbe walidai kuwa uchaguzi ulijaa rushwa, lakini niliwambia waandike malalamiko kwa maandishi na ujumbe mfupi na wamenipatia nitayafanyia kazi na yatatolewa maamuzi na vyombo husika.”

Lakini Zitto alipinga uamuzi huo akisema katibu mkuu hana mamlaka ya kutoa tangazo hilo na kwamba nanlaka hayo ni Kamati Kuu (CC).

"Lakini pia, chombo pekee chenye uwezo wa kufanya uamuzi huo ni Kamati Kuu, sasa inakuaje chombo kingine kichukue uamuzi tena bila matokeo kutangazwa wala mgombea kukata rufaa," alisema Zitto.

Alifafanua kuwa uamuzi huo umetokana na baadhi ya watu kukataa matokeo hayo baada ya kuweka mbele maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama kwa kuwa jambo la msingi katika suala hilo ni matokeo hayo kutangazwa kwanza kabla ya kuahirisha uchaguzi.

"Jambo la kwanza ni kutangaza matokeo na baadaye kama kuna mgombea alikuwa akipinga, anaweza kukata rufaa, lakini matokeo hayajatangazwa wala hakuna aliyekata rufaa," alifafanua Zitto.

Kutokana na utashi wa katiba, Zitto alisema tayari amemwomba katibu mkuu kuitisha mkutano wa CC kujadili suala hilo.

"Nimemwomba Dk Slaa aitishe kikao cha Kamati Kuu tujadili hii hali maana kama viongozi hatutakuwa na busara na chama kitavurugika," alionya.

Alipoulizwa nini mustakabali wa Chadema kutokana na matukio hayo ya vurugu yanayotikisa chama, alijibu: "Viongozi tusipotumia busara chama kitavurugika, lakini tukitumia busara na kuweka maslahi ya chama mbele, tutaweza kutatua haya mambo kwa urahisi."

Zitto alihoji: "Kwanini wazee wasitumie busara kama walizotumia kuniomba mimi nijitoe kwa kutaka wagombea wengine wajitoe au wakubali matokeo kwa kumwachia Kafulila?
"Tukiwa na busara; tukiheshimu demokrasia, tutaweza kuvuka salama. Naamini hilo tu ndiyo suluhisho la kukivusha chama salama."

Naye Kafulila alipinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi kabla ya kutangaza matokeo akisema anataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ambayo anaamini, yalimpa ushindi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kafulila alisema haoni sababu ya kutotangazwa kwa matokeo hayo ambayo anaamini alishinda licha ya kutokubalika na sehemu kubwa ya wajumbe wa sekretarieti na wabunge wa viti maalum.

"Ukiangalia hata hayo mambo ya karatasi kuongezeka, utaona labda ulikuwa ni mpango maalumu wa kumwangusha mtu fulani, lakini imeshindikana," aliongeza.
"Kwa kifupi, sikubaliani na uamuzi huo ninachotaka kwanza matokeo yatangazwe na pia baraza halina mamlaka hayo. Hiyo ni kazi ya Kamati Kuu."

Habari zinadai kuwa tangu John Mnyika kuondoka kwenye wadhifa wa uenyekiti wa vijana wa Chadema, kumekuwa na mkakati wa kumdhibiti Kafulila unaofanywa na baadhi ya vigogo wa Chadema kutokana na mgombea huyo kuonekana mwiba kwao.

Kafulila anasemekana kuwa ni mtu anayepinga waziwazi mambo yanayoendeshwa kinyume na taratibu na amekuwa hahofii viongozi wa juu yake kueleza msimamo wake.

Wakati hayo yakiendelea, vurugu zaidi zimezidi kutikisa chama hicho na jana zilifikia katika hatua ya mgombea mmoja wa nafasi ya uenyekiti wa vijana kutaka kumchoma kisu mwanachama ambaye alikuwa akimtetea Zitto Kabwe asitukanwe na mgombea huyo.

Kabla ya kufikia hatua ya kutishiana visu, mgombea huyo alikuwa akibishana na baadhi ya wafuasi wa Kafulila kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema zilizo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Wakati Mwananchi inafika kwenye ofisi hizo majira ya saa 7:00, vurugu zilikuwa zimeshapoa tangu saa 5:00, lakini wanachama walikuwa wamekaa kwenye vikundi wakijadili matukio mbalimbali ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mgombea huyo na mwanachama mmoja anayedaiwa kuwa anamuunga mkono Kafulila, walirushiana ngumi kwanza na baadaye ndipo mgombea huyo alipotoa kisu na kumtishia.

Mashuhuda hao walidai kwamba mara baada ya mgombea huyo kutoa kisu, wanachama wengine waliokuwa karibu waliingilia kati na kumtoa eneo hilo.

Mwanachama anayedaiwa kutishiwa kisu aliiambia Mwananchi kuwa alikuwa akimsihi mgombea huyo kuacha kumsema vibaya Zitto kwa kuwa malalamiko yote ya uchaguzi wa juzi yako ngazi za juu za chama hicho.

Mwanachama huyo alifafanua kwamba baada ya kumwambia mgombea huyo maneno hayo, alipandisha ghadhabu zaidi na kuanza kutukana.

“Sasa mimi nilivyoona anamtukana Zitto, nilimwambia aache lakini hakusikia; alikuwa anasema Zitto wako na Kafulila walishirikiana kumwibia kura. Kutokana na kuendelea kuongea ovyo, tulishikana na alivyoona muziki ni mnene alinitolea kisu na kutaka kunichoma,” alidai.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa juzi alilazimika kurudi katika ukumbi wa uchaguzi wa Bavicha mnamo saa 6:20 usiku ili kutuliza ghasia zilizoibuliwa na wajumbe mara baada ya kupata habari kuwa kura 20 ziliongezeka katika nafasi ya mwenyekiti.

Wajumbe hao ambao walionekana kuwa upande wa mgombea wa nafasi hiyo, John Heche ambaye ni diwani wa Tarime Mjini, walipinga matokeo kabla hayajatangazwa hali iliyomlazimu msimamizi wa uchaguzi huo, Charles Mwera, ambaye pia ni mbunge wa Tarime, kutoyatangaza.

Dk Slaa, ambaye aliondoka kwenye ukumbi huo juzi saa 7:00 mchana, alirejea kwa mara ya pili saa 6:20 usiku, vurugu zikiendelea baada ya Heche kumpiga ngumi mbili ofisa wa kurugenzi ya uchaguzi ya Chadema, Ali Chitandana na kumlazimu kufanya kazi kubwa kuzituliza.

“Jamani wajumbe nawaomba muwe watulivu kila kitu kilichotokea nimepewa taarifa na Mnyika, kwa hiyo kama kuna mtu ana malalamiko ayaandike na kuyawasilisha makao makuu ya chama kesho (jana) asubuhi ili niyafanyie kazi,” alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao walimweleza wazi Dk Slaa kuwa hawajalipwa fedha zao za posho hali iliyomlazimu katibu huyo mkuu kumwagiza Mtunza Fedha kuwalipa wajumbe hao kutoka mikoa mbalimbali nchini usiku huohuo.

“Wewe Mtunza Fedha walipe wajumbe posho zao; jamani nimeshamwagiza atawalipa wote ila wale ambao wameshakata tiketi kwa ajili ya kusafiri watarudishiwa fedha zao kesho (jana) kwa sababu hamuwezi kuondoka kwa kuwa uchaguzi huu unaweza kurudiwa, lakini yote yatajulikana mara baada ya viongozi kukutana,” alisema Dk Slaa.

“Kwa kweli, nimesikitika sana hiki kitendo kilichotokea leo ni aibu kwa chama. Hapa wapinzani na magazeti yatapata pa kusemea.

Hiki chama ni cha demokrasia; nahitaji kujua kila kitu kilichotokea ili vifanyiwe maamuzi na yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa katiba ya chama.” Habari hii imeandikwa na Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Musa Mkama na Fred

Source: Gazeti la Mwananchi
 
In 1994, one year before the 1995 General Election, the rise and popularity of NCCR- Mageuzi had to be checked, its very roots shaken and its strength weakened. One man accomplished this but to this very moment very few of us understood the irony and to this day many are still not ready to accept this fact for what it was. True believers of multiparty democracy flip flopped and banked their faith to one man who initially had spearheaded the battle against the wana maageuzi. Overnight, in spite of his earlier stand, he became not only the hero but was elevated to wear the crown as the 'camelot' of mageuzi. As expected and supported by history, the dreams and aspirations of many turned into dust and 14 years later, history is bound to repeat itself.

Chadema right now, one year before the upcoming General Election, is an enigma to the status quo as has been witnessed by recent events, and has to be contained. Recently many indications and tell-tale signs have stared at us right in the face, but like the ostrich we have buried our heads in the sand. There is a move afoot and it will be a wonder if Chadema survives it but whichever way it ends, Chadema will never be the same again. One man, Zitto himself through his behaviour that can only be described as erratic, cannot escape the scenario that is unfolding and if anything his actions have fueled it. I am beginning to have some real doubt about him and after going through most of his posts in this forum, his continued claim that he cant be bought casts a dark shadow over him.

This was Zitto's answer to JF members who questioned his support to Dowans Deal earlier this year.
Wengine mnahoji credibility yangu. Bila hata soni mnadhani mimi ni mpumbavu sana wa kuweza kujiwekea bei, at my age! Mnajifanya mnajua, si lolote si chochote. Sisi ndio wawakilishi wenu. Tuulizeni. Tutawajibu. Tuulizeni tena. Tutawajibu. Tena na tena. Dont call us names. This stupidity kills the courage of some of us to question myths of our society. Lakini ninaelewa. Nchi imekuwa na wanasiasa wezi na waongo kwa muda mrefu sana. Hivyo trust to political class hakuna tena. Mpo paranoid. Kila mwanasiasa mnamwogopa masikini. Mnapata viongozi aina yenu Watanzania, kwani wengi ambao wanahoji humu pia hata ukimpa kijiji atakula mpaka bata wa kijiji
That is Zitto - he still has to learn how to control himself, this definitely is not a sign of maturity especially so for a contender to a political post. Cool down friend, only you can make or break you and in doing so you are killing the hopes of many. You dont correct a wrong by doing wrong !
 
Daaah Omary this is too low...

Pole kaka!

Hivi mtu ukishakuwa naibu katibu mkuu unakosa haki ya kumpigia kampeni mgombea unayemwamini hata kama umejivua majukumu yote ya kusimamia uchaguzi? Hivi hawa vijana wadogo kwa Zitto mwenye umri wa miaka 33 ni wapi hao? Kama Zitto alijitoa katika shughuli za kusimamia uchaguzi na yeye ni mjumbe wa mkutano wa vijana ni wapi amekosea? Na kati ya Zitto na ninyi ni kina nani ambao wamo katika timu ya kusimamia uchaguzi lakini pia wanakuwa mbele kupiga kampeni chafu dhidi ya Zitto na sasa mmekimbilia kwa watu wanaomuunga mkono?

Kwa taarifa yenu Zitto hakuwa na nia ya kufanya kampeni zaidi yakumsaidia kimawazo Kafulila hadi mlipojikusanya wote na baadhi yenu mkiwa wasimamizi wa uchaguzi kuenda kuanza kumfanyia kampeni mtu "wenu" eti kumuonyesha siasa Zitto. Hapo ndipo mlipo likoroga. Zitto alishakuwa tayari kujishusha na kum-approach Mbowe for genuine reconciliation lakini kwa utoto wenu mkajiona kuwa mmemshinda na mtaweza "kummaliza". That wa a big mistake kwenu lakini pia kwa maslahi ya chama chenu.



Hivi Mbowe amekaa kimya? Yaani mtu anayeongea nyumba ya pazia ndio amekaa kimya na huyu anayeongea bila ya kujificha ndiye amekuwa mbaya. Tatizo vijana mnakurupukia profession za watu. Unaibuka huko ulipo unajidanganya kuwa unajua spining bia ya kutambua uwezo na uthubutu wa unayemfanyia spining katika kujibu mashambulizi. Ulitaka uj umwage sumu yako halafu Zitto anyamaze afe kisabuni? Tena hapa Zitto amejicontroal sana maana ninyi ndio mnaojua ni nani na kutoka upande gani wamekuwa wakitumia rushwa katika uchaguzi huu.




Siri, yaleyale wtu wanatoka ndani ya CCM kushutumu ufisadi kina Makamba wanasema washugulikiwa kwa kuvuja siri za chama. Uozo na uvundo hauwezi kuwa siri na kuuficha ni kuwalaghai watanzania.



Yale yale, wanatokea watu wanawaeleza uovu wa MASIHA FEKI wenu wanaonuka ufisadi na kujidai kuwa wanapiga vita ufisadi huohuo, mnakimbilia kusema kuwa wanaosema uchafu wao watakuwa wametumwa na mafisadi. Hivyo hivyo ndani ya chama chenu mnapofanya mambo ya maovu yaliyopita kiwango cha uvumilivu wakitokea wenzenu kuyasema mabaya hayo mnakimbilia kutafuta mchawi nje ya nyumba...Hapa CCM msiwahusishe kwani ni wenyewe mmeamua kujigeuza asusa yao.

Kubalini makosa yenu, jifunzeni kujisahihisha halafu muanze upya na sio kutaka kushambulia mliowkosea ili kuhalalisha makosa mliyoyafanya na mnaendelea kuyafanya kama spining hii mliyoleta hapa

omarilyas
 
- Duh! Wakuu nilikuwa safari kidogo, naona nimepitwa na mengi sana hapa, ingawa nikiwa safari jana niliongea na Mzito mmoja wa CCM, akaniambia Chadema wana akili sana sio kama sisi CCM, sikujua ana maana gani sasa labda nisome hii thread mwanzo mpaka mwisho, inaelekea kuna yaliyojiri huko!

- Anyways tupo pamoja wakuu!

Respect.

FMEs!
 
Balantanda,
Nimesoma habari nzima iloandiikwa na kusema kweli Zitto ana kila haki ya kuteteta mtu wake. Upande wa Henge wanaonekana wahuni watupu na ajabu ktk kikao cha chama uhuni kaa huo umetokea.
Hata mimi naamini kabisa kama kulikuwepo na mshindi Dr Slaa alitakiwa kutangaza mshindi kisha kama kuna malalamiko ndipo chama kingebatilisha matokeo kulingana na ushahidi. Kinyume cha hapo inaonyesha wazi wazee walikuwa na mtu wao wamempanga kuchukua nafasi hiyo. Hakika ni ktk habari za Ulaji tu yaani wa Tarime walishabikia tarime na Kigoma kushabikia Kigoma kama vile chama kinataka kusambaza nguvu zake za uongozi kwa sehemu nyeti bila kutumia demokrasia..
Tatizo jingine lililojitokeza inaonyesha wazi vijana wengi Chadema hawana heshima na viongozi wao hasa wazee kaisi kwamba ngumi kwao ni njia rahisi ya kutafuta suluhu yaani kilichofanyika huko ktk mkutano mkuu ni Uhuni mtupu.. Utadhani walikuwa DDC wakiyarudi ya Msondo ngoma!
 

1. NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.

2. Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni.


3. “Chama hiki si changu, wala si cha Mbowe, sisi tutaondoka chama kitabaki hapahapa na uamuzi wangu kugombea, ni jambo la kawaida wala sihitaji mpasuko au mgawanyiko, mwaka 1998 Bob Makani na Philemon Ndesamburo waligombea nafasi hii wakatofautiana, lakini baada ya uchaguzi, waliungana na kuendeleza chama,” alisema Zitto.

4. Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi,

5. Alitamba kuwa anajiamini kuwa na uwezo katika kukiongoza chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa katika nafasi yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini, ameongoza kamati muhimu ya Bunge, ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyo na mashirika yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tano.

6. “Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi?

7. Alisema amekuwa kwenye chama hicho tangu akiwa na umri wa miaka 16 na kupitia ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama hicho, hivyo anaamini sifa za kushika wadhifa huo anazo kwa kuwa anakifahamu vyema.

8. Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.

“Hata hivyo, nikichaguliwa kuwa Mwenyekiti dhana hiyo ya ukabila itaacha kuwa na nguvu,” alisema. .

- Duh! haya makubwa haya kumbe yalifikia kuwa haya?

Respect.

FMEs!
 
Balantanda,
Nimesoma habari nzima iloandiikwa na kusema kweli Zitto ana kila haki ya kuteteta mtu wake. Upande wa Henge wanaonekana wahuni watupu na ajabu ktk kikao cha chama uhuni kaa huo umetokea.
Hata mimi naamini kabisa kama kulikuwepo na mshindi Dr Slaa alitakiwa kutangaza mshindi kisha kama kuna malalamiko ndipo chama kingebatilisha matokeo kulingana na ushahidi. Kinyume cha hapo inaonyesha wazi wazee walikuwa na mtu wao wamempanga kuchukua nafasi hiyo. Hakika ni ktk habari za Ulaji tu yaani wa Tarime walishabikia tarime na Kigoma kushabikia Kigoma kama vile chama kinataka kusambaza nguvu zake za uongozi kwa sehemu nyeti bila kutumia demokrasia..
Tatizo jingine lililojitokeza inaonyesha wazi vijana wengi Chadema hawana heshima na viongozi wao hasa wazee kaisi kwamba ngumi kwao ni njia rahisi ya kutafuta suluhu yaani kilichofanyika huko ktk mkutano mkuu ni Uhuni mtupu.. Utadhani walikuwa DDC wakiyarudi ya Msondo ngoma!

taratibu mtaanza kumwelewa zitto

Niliyoipenda ni hiyo eti tukashikana akaona mziki mkubwa kachomoa kisu. duu hii kali kweli afadhali ya kina Nape na Nchimbi.japo wote wahuni
 
Chadema mmejitahidi kidogo, hongereni sana, maana uslama wa taifa na mashushushu wao walikuwa wana 'warm up' kufanya kile ambacho kingeitwa "operation sambaratisha" ambayo ingeifanya Chadema kuingia uchaguzi mkuu wa 2010 wakiwa kila mtu na "jezi" yeke uwanjani. Keep it up....sasa naona wamebakia "..du!..tumewakosa..."
 
Mama Zitto afyatuka, uchaguzi Chadema wafutwa
MAMA mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto amesema, mwanae si fisadi na hanunuliki.

Amesema, viongozi katika makao makuu ya chama hicho ni 'wachafu', wanakiharibu chama.

Shida Salum amesema, Zitto hanunuliki na hawezi kununuliwa. Amesema leo Dar es Salaam kuwa, ofisi ya Makao Makuu ya Chadema itakiharibu chama hicho na anasikia aibu mwanae kutajwa kuwa ni mmoja wa mafisadi katika chama hicho.

Mwanachama huyo wa Chadema amesema, ofisi ya Makao Makuu Chadema imeingiliwa, na kwamba, chama hicho kimechafuka.

Salum ameyasema hayo mara baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kufungua mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA).

“Mimi fomu ya Zitto niliifukiza nyumbani kwangu, Zitto sio fisadi, hanunuliki na hawezi kununuliwa,” amesema mama Zitto.

Amesema,amekuwa katika chama hicho tangu mwaka 1992, na anasikia aibu sana zinapoibuka taarifa sasa kwamba mwanae ni miongoni mwa mafisadi.

Alisema amekuwa akifika katika ofisi ya makao makuu kila mara kuomba kuonana na Katibu Mkuu (Slaa) ili wazungumze kuhusu viongozi wanaomharibia chama,na wanaotaka kukigawa chama.

“Siwezi kumkataa Zitto, katika uchaguzi huu ofisi imeingiliwa, jirekebisheni, chama kimechafuka, hali ambayo inafanya watu kukiogopa chama,” amesema Mama huyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa kina mama waliofika kwa ajili ya uchaguzi huo.

- Whaaat? Yamekua haya tena? Ohhh My God!

FMEs!
 
Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.

Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.

Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.

Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.

Mbona umekiri mwenyewe kuwa ulishiriki katika kumfanyia hila marehemu Wangwe? Ulikuwa wapi muda wote huu kuyasema yote haya? what goes around comes around kaka.

Umeshapoteza uaminifu miongoni mwa wananchi wengi kutokana na mambo ambayo umeyaweka wazi leo hii. Ungeshinda uenyekiti wa chama si ndio ungefanya madudu kabisa!! amakweli mgema ukimsifia, tembo hulitia maji
 
Mbona umekiri mwenyewe kuwa ulishiriki katika kumfanyia hila marehemu Wangwe? Ulikuwa wapi muda wote huu kuyasema yote haya? what goes around comes around kaka.

Umeshapoteza uaminifu miongoni mwa wananchi wengi kutokana na mambo ambayo umeyaweka wazi leo hii. Ungeshinda uenyekiti wa chama si ndio ungefanya madudu kabisa!! amakweli mgema ukimsifia, tembo hulitia maji

Hata sauli alipotokokewa alisimulia jinsi walivyowatenda vibaya vijakazi wa Bwana aliyasimulia tena na tena ktk mahubiri yake na alikuja kuwa shuhuda mzuri na mtume swafii kabisaa.

Leo hii Zitto kusimulia maavu hafanyi madudu bali anafanya lilo jema kabisa kuelekea ktk uongozi swafi

Na unafiki umekoma baada ya kuunza kuutaja unafiki alio ubeba siku nyingi ,
 
- Yale yale aliyoyasema Obama kule Ghana, Africans tuache tabia ya kuwekeza kwenye majina ya viongozi, tujifunze kuwekeza kwenye sound policies hii thread na yaliyojiri ni mfano mkubwa sana wa maneno ya Obama.

- Among all, Chadema sikutegemea kukutwa na haya inasikitisha sana, sawa huenda mmekubaliana na kuyamaliza, lakini swali la the big picture linapaswa kua ni under who´s expense? Somebody must pay for makubaliano yenu ya kumfanya Zitto arudishe fomu, now who is that? kama sio sisi wananchi wa Tanzania?

- I mean, hii ndio mnaita demokrasia makini? Mimi nilifkiri demokrasia makini huanzia kwenye box la kura, kumbe inaweza kupatikana na busara za wazee wa Chama? Yaani na nyinyi Chadema mnakubaliana na tabia za CCM za busara za Spika? Nimeona a lot of spinning humu mnapoteza muda bure, sana sana sasa mnawapa CCM uhuru wa kuzidi kutuchezea wananchi wa taifa hili, kama na ninyi mnafanya kwa nini wao wasifanye?

- Yaaani mnaogopa Mbowe kusimama na Zitto tu? Lakini hamuogopi Mbowe kusimama na rais wa sasa wa CCM? This is incredible, Zitto alipofukuzwa bungeni wengi tumelia kuwa ameonewa, sasa mnakuja na hizi nonsense ambazo ni clear kwamba kumbe hakuonewa kufukuzwa bunge kama ninawasoma vizuri humu na hizi spin zenu! Hamna hata aibu! Hivi mafisadi walimtuma Zitto kuchukua fomu ya Chadema, sasa waliomtuma kuwapigia kelele mafisadi kule bungeni mpaka kufukuzwa ni nani hasa? Hivi hili taifa tumemkosea nini Mungu? Sasa nani wa kumuamini tena hapa kati yenu Chadema na CCM?

- Simtetei Zitto wala Mbowe, ninaitetea demokrasia ambayo hapa imepigwa chini kwa manufaa ya watu binafsi huko Chadema na sio ya chama, no way demokrasia makini sio kumzuia mgombea mwenye akili ya kitoto na ambaye hajamkomaa kiakili, demokrasia ni absolutely opposite ya hii theory kwa sababu inataka apewe nafasi apigwe na kura za wananchi, lakini sio kumzuia kugombea, kuna ubovu mnajaribu kuuficha, sijui ni nini hasa mnachojaribu kukificha chama cha Demokrasia makini? What is it?

- Yaani kweli mnajaribu ku-pull a monkey on us wananchi na huku tunaona kwa macho yetu kwamba mnachosema sio ukweli ila ni zile zile siasa za CCM? Mnakuja hapa kumchafua Zitto na filimbi nyingi za kuwalaumu CCM, badala ya kusimama na kubeba msalaba wenu? Yes I said it huko Chadema kuna uozo kama wa CCM, ila mnajaribu kuuficha na busara za wazee lakini hamsemi nani atakayelipia kwa sababu anytime ukiuminya ukweli lazima kuwe na price to be payed, ni simple life maths.

- Mnaleta spin za ajabu hapa kumchafua Zitto, sasa kwanini msiruhusu akajimalize kwenye uchaguzi kama kweli ni mchafu kama mnavyodai? Aibuu sana hii watu tulikua tunawaamini na kuwategemea kumbe ni wale wale CCM tu, hivi mimi nimesema mara ngapi hapa kwamba the best idea ni ku'do away na viongozi wote na kufuta vyama vyote na kuanza na upya, nilisema hayo kwa sababu ya kutomuamini anybody, I mean kosa la Zitto ni nini hasa kuchukua fomu ya Mwenyekiti?

- Chadema kwa hili mmetuangusha wengi sana na mnanuka kama mafisadi ndani ya CCM tu, haya mafisadi kumbe yapo kote kote sasa dawa ni kuyajua yalioko Chadema maana ya CCM yanajulikana tayari, maana hii ni aibu ya the Century hata mki'spin vipi you are rotten kama mafisadi ya CCM tu, dawa ni kutunga katiba mpya ya kufuta vyama vyote vya siasa Tanzania na marufuku viongozi wote wa sasa kugombea uongozi tena tukianza na vyama vipya, I mean this is the worst ever!

Yaani Chadema chama cha demokrasia makini kinamzuia mwanachama wake kugombea uongozi kwa sababu ya kumuogopa kama CCM na Mrema, na kuanza kumuita majina kibao, ya kumchafua halafu eti atarudi bungeni tena kwa tiketi ya chama hicho na kuwa na heshima ile ile kutoka kwa sisi wananchi, halafu na Chadema nayo itaendelea kuwa na heshima ile ile kama zamani, yaani kweli na ninyi chadema kama CCM mnatufanya sisi wananchi wa Tanzania ni kama watoto wadogo tusio na akili!

Shame on all of you mnaohusika na hii nonsense ya busara kama za Spika! Kule CCM zile busara za Spika ziligahrimu Shillingi Millioni 100 hela zetu wananchi walipa kodi, sasa Chadema tuambieni huko kwenu hizi busara zitatumika hela ngapi na za nani?

Respect.

Field Marshall Es!
 
Hata sauli alipotokokewa alisimulia jinsi walivyowatenda vibaya vijakazi wa Bwana aliyasimulia tena na tena ktk mahubiri yake na alikuja kuwa shuhuda mzuri na mtume swafii kabisaa.

Leo hii Zitto kusimulia maavu hafanyi madudu bali anafanya lilo jema kabisa kuelekea ktk uongozi swafi

Na unafiki umekoma baada ya kuunza kuutaja unafiki alio ubeba siku nyingi ,

- Haya niliyasema siku nyingi sana nenda kwenye thread za ile ishu, mkanishupalia sana hapa na uchunguzi wangu, sasa mnaona mwenyewe Zitto amekubali,

- Mkulu Ushiwarombo uko wapi maana wewe ndiye uliyekua mbishi sana kwamba ninatunga zile habari za kupatikana kwa text messages kuhusu computers kati ya yule kijana aliyeko jela na mbunge mmoja maarufu sana, sasa si uona haya ya leo yanajisema yenyewe! Aibuu!

Respect.

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom