Kwa sababu hao ni mafisadi .... na wanajaribu kumtoa Mwakyembe kule Kyela ili waweke fisadi mwenzao
Lakini damu ile yawalilia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sababu hao ni mafisadi .... na wanajaribu kumtoa Mwakyembe kule Kyela ili waweke fisadi mwenzao
Mkuu, CCM ni chama tawala wakati CHADEMA ni chama kinachokuwa. Ni matamanio yangu kuwa na chama ambacho kinaweza kuwa na nguvu kubwa kama ilivyo CCM ili kiweze kusaidia kuleta ustaarabu mpya na utawala bora nchini.
Maamuzi ya CCM si tu kuwa yana manufaa au madhara kwa Taifa zima, bali pia hupelekea mabadiliko ya haraka sana katika maisha ya kila mtanzania bila kujali imani yake kisiasa. Ndio maana ni lazima kusema sana endapo CCM (Chama kikongwe kabisa nchini) kinapofanya mambo yasiyoeleweka. Nakuhakikishia Mkuu, hata Kiongozi wa juu wa CCM angefanya aliyofanya Zitto leo hapa, response ingekuwa kama hii au zaidi kidogo.
Lakini damu ile yawalilia
Yap, damu ya vitoto vichanga vinakufa kila siku hospitalini kwa kukosa dawa inalia bila kukoma.
Damu ya Wangwe y walilia toka udongoni,hakika hakutabaki jiwe juu ya jiwe jingine
That is Zitto - he still has to learn how to control himself, this definitely is not a sign of maturity especially so for a contender to a political post. Cool down friend, only you can make or break you and in doing so you are killing the hopes of many. You dont correct a wrong by doing wrong !Wengine mnahoji credibility yangu. Bila hata soni mnadhani mimi ni mpumbavu sana wa kuweza kujiwekea bei, at my age! Mnajifanya mnajua, si lolote si chochote. Sisi ndio wawakilishi wenu. Tuulizeni. Tutawajibu. Tuulizeni tena. Tutawajibu. Tena na tena. Dont call us names. This stupidity kills the courage of some of us to question myths of our society. Lakini ninaelewa. Nchi imekuwa na wanasiasa wezi na waongo kwa muda mrefu sana. Hivyo trust to political class hakuna tena. Mpo paranoid. Kila mwanasiasa mnamwogopa masikini. Mnapata viongozi aina yenu Watanzania, kwani wengi ambao wanahoji humu pia hata ukimpa kijiji atakula mpaka bata wa kijiji
Hivi mtu ukishakuwa naibu katibu mkuu unakosa haki ya kumpigia kampeni mgombea unayemwamini hata kama umejivua majukumu yote ya kusimamia uchaguzi? Hivi hawa vijana wadogo kwa Zitto mwenye umri wa miaka 33 ni wapi hao? Kama Zitto alijitoa katika shughuli za kusimamia uchaguzi na yeye ni mjumbe wa mkutano wa vijana ni wapi amekosea? Na kati ya Zitto na ninyi ni kina nani ambao wamo katika timu ya kusimamia uchaguzi lakini pia wanakuwa mbele kupiga kampeni chafu dhidi ya Zitto na sasa mmekimbilia kwa watu wanaomuunga mkono?
Kwa taarifa yenu Zitto hakuwa na nia ya kufanya kampeni zaidi yakumsaidia kimawazo Kafulila hadi mlipojikusanya wote na baadhi yenu mkiwa wasimamizi wa uchaguzi kuenda kuanza kumfanyia kampeni mtu "wenu" eti kumuonyesha siasa Zitto. Hapo ndipo mlipo likoroga. Zitto alishakuwa tayari kujishusha na kum-approach Mbowe for genuine reconciliation lakini kwa utoto wenu mkajiona kuwa mmemshinda na mtaweza "kummaliza". That wa a big mistake kwenu lakini pia kwa maslahi ya chama chenu.
Hivi Mbowe amekaa kimya? Yaani mtu anayeongea nyumba ya pazia ndio amekaa kimya na huyu anayeongea bila ya kujificha ndiye amekuwa mbaya. Tatizo vijana mnakurupukia profession za watu. Unaibuka huko ulipo unajidanganya kuwa unajua spining bia ya kutambua uwezo na uthubutu wa unayemfanyia spining katika kujibu mashambulizi. Ulitaka uj umwage sumu yako halafu Zitto anyamaze afe kisabuni? Tena hapa Zitto amejicontroal sana maana ninyi ndio mnaojua ni nani na kutoka upande gani wamekuwa wakitumia rushwa katika uchaguzi huu.
Siri, yaleyale wtu wanatoka ndani ya CCM kushutumu ufisadi kina Makamba wanasema washugulikiwa kwa kuvuja siri za chama. Uozo na uvundo hauwezi kuwa siri na kuuficha ni kuwalaghai watanzania.
Yale yale, wanatokea watu wanawaeleza uovu wa MASIHA FEKI wenu wanaonuka ufisadi na kujidai kuwa wanapiga vita ufisadi huohuo, mnakimbilia kusema kuwa wanaosema uchafu wao watakuwa wametumwa na mafisadi. Hivyo hivyo ndani ya chama chenu mnapofanya mambo ya maovu yaliyopita kiwango cha uvumilivu wakitokea wenzenu kuyasema mabaya hayo mnakimbilia kutafuta mchawi nje ya nyumba...Hapa CCM msiwahusishe kwani ni wenyewe mmeamua kujigeuza asusa yao.
Kubalini makosa yenu, jifunzeni kujisahihisha halafu muanze upya na sio kutaka kushambulia mliowkosea ili kuhalalisha makosa mliyoyafanya na mnaendelea kuyafanya kama spining hii mliyoleta hapa
omarilyas
1. NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.
2. Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni.
3. Chama hiki si changu, wala si cha Mbowe, sisi tutaondoka chama kitabaki hapahapa na uamuzi wangu kugombea, ni jambo la kawaida wala sihitaji mpasuko au mgawanyiko, mwaka 1998 Bob Makani na Philemon Ndesamburo waligombea nafasi hii wakatofautiana, lakini baada ya uchaguzi, waliungana na kuendeleza chama, alisema Zitto.
4. Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi,
5. Alitamba kuwa anajiamini kuwa na uwezo katika kukiongoza chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa katika nafasi yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini, ameongoza kamati muhimu ya Bunge, ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyo na mashirika yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tano.
6. Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi?
7. Alisema amekuwa kwenye chama hicho tangu akiwa na umri wa miaka 16 na kupitia ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama hicho, hivyo anaamini sifa za kushika wadhifa huo anazo kwa kuwa anakifahamu vyema.
8. Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.
Hata hivyo, nikichaguliwa kuwa Mwenyekiti dhana hiyo ya ukabila itaacha kuwa na nguvu, alisema. .
Balantanda,
Nimesoma habari nzima iloandiikwa na kusema kweli Zitto ana kila haki ya kuteteta mtu wake. Upande wa Henge wanaonekana wahuni watupu na ajabu ktk kikao cha chama uhuni kaa huo umetokea.
Hata mimi naamini kabisa kama kulikuwepo na mshindi Dr Slaa alitakiwa kutangaza mshindi kisha kama kuna malalamiko ndipo chama kingebatilisha matokeo kulingana na ushahidi. Kinyume cha hapo inaonyesha wazi wazee walikuwa na mtu wao wamempanga kuchukua nafasi hiyo. Hakika ni ktk habari za Ulaji tu yaani wa Tarime walishabikia tarime na Kigoma kushabikia Kigoma kama vile chama kinataka kusambaza nguvu zake za uongozi kwa sehemu nyeti bila kutumia demokrasia..
Tatizo jingine lililojitokeza inaonyesha wazi vijana wengi Chadema hawana heshima na viongozi wao hasa wazee kaisi kwamba ngumi kwao ni njia rahisi ya kutafuta suluhu yaani kilichofanyika huko ktk mkutano mkuu ni Uhuni mtupu.. Utadhani walikuwa DDC wakiyarudi ya Msondo ngoma!
Mama Zitto afyatuka, uchaguzi Chadema wafutwa
MAMA mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto amesema, mwanae si fisadi na hanunuliki.
Amesema, viongozi katika makao makuu ya chama hicho ni 'wachafu', wanakiharibu chama.
Shida Salum amesema, Zitto hanunuliki na hawezi kununuliwa. Amesema leo Dar es Salaam kuwa, ofisi ya Makao Makuu ya Chadema itakiharibu chama hicho na anasikia aibu mwanae kutajwa kuwa ni mmoja wa mafisadi katika chama hicho.
Mwanachama huyo wa Chadema amesema, ofisi ya Makao Makuu Chadema imeingiliwa, na kwamba, chama hicho kimechafuka.
Salum ameyasema hayo mara baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kufungua mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA).
Mimi fomu ya Zitto niliifukiza nyumbani kwangu, Zitto sio fisadi, hanunuliki na hawezi kununuliwa, amesema mama Zitto.
Amesema,amekuwa katika chama hicho tangu mwaka 1992, na anasikia aibu sana zinapoibuka taarifa sasa kwamba mwanae ni miongoni mwa mafisadi.
Alisema amekuwa akifika katika ofisi ya makao makuu kila mara kuomba kuonana na Katibu Mkuu (Slaa) ili wazungumze kuhusu viongozi wanaomharibia chama,na wanaotaka kukigawa chama.
Siwezi kumkataa Zitto, katika uchaguzi huu ofisi imeingiliwa, jirekebisheni, chama kimechafuka, hali ambayo inafanya watu kukiogopa chama, amesema Mama huyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa kina mama waliofika kwa ajili ya uchaguzi huo.
Nakubaliana na wewe kuwa nilipaswa kuwa juu ya siasa zile. Nilijua Kafulila anapigwa vita na nguvu kubwa sana ndani ya chama. Nilitaka kuonyesha nguvu hiyo kuwa Kafulila naye ana watu. Ukitafsiri kuwa natoka naye Kigoma sawa, lakini Kafulila ni Mfipa wa Rukwa na mimi ni Muha wa Kigoma.
Ndugu yangu, matokeo hayakutangazwa. Basi yangetangazwa hata hayo ambayo hakufikia 50% ili kura zipigwe kwa wagombea 2 wa juu.
Kafulila meshinda kwa zaidi ya nusu ya kura. Walioshindwa hawataki kushinidwa.
Nilimpigia kampeni kafulila waziwazi bila kificho. Mimi sio mnafiki na ndio maana sikujihusisha na kusimamia ucahguzi ili nisiwe biased.
Mbona umekiri mwenyewe kuwa ulishiriki katika kumfanyia hila marehemu Wangwe? Ulikuwa wapi muda wote huu kuyasema yote haya? what goes around comes around kaka.
Umeshapoteza uaminifu miongoni mwa wananchi wengi kutokana na mambo ambayo umeyaweka wazi leo hii. Ungeshinda uenyekiti wa chama si ndio ungefanya madudu kabisa!! amakweli mgema ukimsifia, tembo hulitia maji
Hata sauli alipotokokewa alisimulia jinsi walivyowatenda vibaya vijakazi wa Bwana aliyasimulia tena na tena ktk mahubiri yake na alikuja kuwa shuhuda mzuri na mtume swafii kabisaa.
Leo hii Zitto kusimulia maavu hafanyi madudu bali anafanya lilo jema kabisa kuelekea ktk uongozi swafi
Na unafiki umekoma baada ya kuunza kuutaja unafiki alio ubeba siku nyingi ,