Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
 
Yatasemwa mengi yaliyo nyuma ya pazia mkuu,tusubiri na tuone
 
Mzee ES na Mkandara,

Heshima kubwa iwe kwenu wakuu kwa kuweza kuja hapa mapema na kutoa maoni, wamarekani wanasema amsubiri mpaka jumatatu ili mpate matokeo ndio muanze kuzungumza " Monday morning quarterback."

Jamani kuna mtu mmoja muhimu sana huko Chadema , Kitila Mkumbo ; ningependa sana kujua his take on this issue. Wananchama it's about time now people must stand up and be counted.
 
Kwa kweli hata mimi siamaini kwamba CHADEMA ni wale wale...AKINA Mkuchika na makamba......I dont want to believe!! Duh...sasa itabidi next year nisipige kura...

Friends..I might be wrong..ila mimi mpaka hapa sijaona kosa la Zitto. Kwa sababu kama alivyosema FMES sioni kwa nini CHADEMA waogope kuwapambanisha wananchama wake Zitto na MBOWE..WHY???????????????????

Jamani kama Zitto akikubalika..si ndo demokrasia yenyewe?? KWA NINI WAZEE WA CHADEMA WAOGOPE?

Inasikitisha na inauma sana.
 
kamanda umemaliza kila kitu hapa.pia ukiweza soma gazeti la mwananchi.co.tz utaona maneno ya mama zitto kabwe.

Unajua hawa wazee wa chadema waliogopa kumpeleka kwenye penalty box zitto. Wakaona wacheze foul nje ya 18 kumbe ndio kosa kubwa.

Kibanda alisema kuwa mbowe alitafuta wanachama zaidi ya elfu kumi kigoma ambao zitto aliwakuta.sasa kama mbowe alitafuta watu wote hao.kwanini wasimpe fursa agombee halafu wamtoe nishai kwa kupata kura chini ya kumi?

Pia mods wamekuwa hawatendei haki kwani wamekusanya kila kitu kukificha hapa tunakosa mtiririko.kuna mada ya uchaguzi mkuu inajitegemea na kuna mada ya vijana wa chadema na uchaguzi.zote zinachaganywa ili kuwalinda mafisadi wa chadema waliamua kuibaka demokrasia.
 
 

mkuu umenena ...nimeona loophole mbaya sana ambayo inaweza kutumiwa na maadui wa zitto na maadui wa chadema ...ieleweke kuwa kila chama kina siri zake......na moja ya sifa ya kiongozi ni kuhifadhi...sasa siwaelewi watu wanaomshabikia zitto kuropoka wakati wanajuwa amejipotezea sifa ya kuaminika kuhifadhi mambo mazito..ukizingatia kati ya vijana wa umri wake ni front runner to presidency....sasa unafikiri watu wa usalama faili lake leo wataongezea comment gani....hasa ukizingatia uzito wa siri viongozi wanazobeba..

hapo nyuma nimewakumbusha kuwa pamoja na mrema kutofautiana na chama cha ccm ...hadi leo hajatoa siri hata moja zaidi ya viti ambavyo kila mtu alijuwa kama chavda..etc..hasa ukizingatia nafasi yake kama mkuu wa usalama ccm,mbunge ,waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu..

nahisi kuwa tutakuwa na tatizo la kiusalama huko mbeleni...kama idara ya usalama haitachukua jukumu la kutoa mafunzo ya maadili na uongozi kwa vijana wote wanaopata nafasi kubwa au ubunge hata wa upinzani...nimesikitika sana ...maneno ya kuropoka angetoa mtu kama hiza au aina yake nisingesikitiaka ...lakini zitto ni kijana tunayemtegemea ..kwenye hii safari...!!!..lazima awe na maadili ya uongozi ...kubalini kataeni sifa ya muhimu tunayoangalia kwa kiongozi ni kutunza siri!!!

wanaomshabikia mbona hawajiulizi kusikia siri zaidi ya tetesi kuhusu ...sokoine,kolimba.,na wengine wengi...??????.. au ccm hawana midomo???
 
Mzee ES,

Mimi nadhani kosa alilolifanya Zitto humu ndani leo ni kubwa kuliko la yeye kunyimwa kugombea . Wazee ni kweli walifanya kosa kutokumruhusu , lakini hata hivyo kosa la ku-call out Chadema dirty laundry is below the belt . Regardless of what they did, he shouldn't have done what he did.
 
 

- Mkulu PM, huyu Zitto alifikiaje kua naibu katibu mkuu wa Chadema? Unajua ninashindwa kuchambua sana post yako kwa sababu ya heshima yangu kwako, lakini naomba kukwambia kwamba the more you talk ku-justfy kumzuia Zitto ni more unaharibu sana mkuu.

- Ukweli ni kwamba kama CCM huko Chadema, sasa demokrasia imekufa rasmi na hii ishu.

Respect.

FMEs!
 
pole sana mzee kwanini hukumtuma kibanda akufanyie kazi kama mwanzo?hakuna siri aliyoitoa zitto kasema uozo uliopo.akausemee wapi na wazee wako wameshamfunga mdomo? Mama yake kamfuata slaa asuluhishe hadi leo slaa hajafanya kitu.mwache zitto amwage uoza hapa hapa jf. Pumzika mzee kipindi hiki.
Nakukumbusha maneno ya mbowe alisema vijana tusiwe waoga tuthubutu.zitto kathubutu.
 

- Kwa hiyo unsema ilikuwa sawa kwa Mwakyembe kutotoa ripot yote ya Richimonduli na kumnusuru Lowassa?

- Rufiji among all the people humu JF, kweli na wewe unaetetea kuuliwa kwa demokrasia ndani ya chama tena cha upinzani?

Respect.

FMEs!
 
tena ni mkakamavu kwa kipindi sikutegemea kama atapata courage ya kuja hapa kuleta utumbo wake.
hata mimi namuheshimu sana huyu mheshimiwa.
 

- Zitto aachiwe aseme yote tuyajue vizuri, ya kujiua kisiasa lisiwe tatizo la Chadema, bali la Zitto mwenyewe na besides hakluna jipya kwa tunaojua vizuri atakalolisema au alilokwisha sema so far!

- Mkuu Kanda2, tupo pamoja sana hapo!

FMEs!
 
 
tena ni mkakamavu kwa kipindi sikutegemea kama atapata courage ya kuja hapa kuleta utumbo wake.
hata mimi namuheshimu sana huyu mheshimiwa.

- Hii ni JF kumkoma nyani hatujawahi kuogopa mtu hapa wala ishu, tumewanyamazia toka majuzi tukidhani mtayamaliza huko Chadema kwa manufaa ya masilahi yetu wananchi,

- Sasa mmeharibu halafu mnajaribu tena kuja hapa JF ku-spin nonsense! Mkulu PM tumejaribu sana kuwaheshimu na hili lakini mlichofanya ni aibu kubwa sana, sasa muacheni Zitto ajimalizie zaidi, lakini jaribuni kukinusuru chama Chadema kwa kufunga midomo yenu sasa.

Ni ushauri wa bure tu, Zitto hana anything to lose ila ana everything to gain, hapa na hizi behavior zake naona inapaliliwa njia ya kwenda CCM hebu nyamazeni msijiabishe zaidi maana he is taking down the whole chama mnapozidi kumuandama. Nimewaambieni siku nyingi sana kwamba Chadema mna matatizo ya washauri kama CCM, how can you fight Zitto at this stage alipofikia? Halafu uka'expect ku-win?

Respect.

FMEs!
 
Zitto kishakula za mafisadi,anajiandaa kwenda CCM...hana lolote anatafuta kula tuu!
 
 
Field marshall ES,
Mkuu hakuna mtu anayezungumzia kuenguliwa kwa Zitto ktk kugombea uenyekiti. Kwanza ni swala la chama Chadema halikuhusu kitu wewe mbona Malecela alienguliwa.. Kuna majina kibao yaliernguliwa kabla jina la Mama Asha Rose Migiro halijapigiwa kura huko UN, tena Kenya wanalia hadi kesho kwani walitegemea mtu kutoka kwao kushika nafasi hiyo.. Kila sehemu ya taasisi duniani huwa na mchekecho wa majina unaoweza kuengua jina la mtu yeyote kutokana na mapungufdu wanayoyahitaji wao..Imetokea CCM, imetokea CUF imetokea UN na vyama kibao vya kisiasa hadi nchi zinazodai kuwa na demokrasia ya kweli. Mkuu, angalia nyumba yako huwezi kutuchagulia mke hata kidogo. Sifa za zinazotakiwa kugombea kiti cha mwenyekiti CCM haziwezi kuwa sawa na vyama vyote na demokrasia haiwezi kukiuka SIFA zinazomwezesha mgombea ku qualify..who knows pengine Zitto hakuwa na sifa hizo...

Pamoja na yote haya sisi tulikwisha elewa kitu gani kinafanyika, njama zote against Zitto zilijulikana lakini tatizo letu ni Zitto mwana JF sio wajinga wengine. tatizo ni pale kiongozi wetu huyu anapojibu mapigo ya paparazi kwa hamaki bila kufahamu kwamba naazidi kutuweka Uchi.. Hakujibu kwa kutumia hekima, alikichafua chama na wote waliokuwepo sawa na mke/mme anayekwenda hadithia marafiki zake negative vibes kuhusu mwenza au kinachofanyika ndani ya nyumba yake.. Ikiwa mashtaka ni halali nenda Polisi au vyombo vya sheria sio kuanika na kulia lia kwa majirani ukifikiria watakuonea huruma sana kumbe ndio kwanza unaharibu ndoa yako..Hizi ndizo lawama zetu kwa Mh. Zitto...Mkuu unajua fika kuwepo kwa watun kama hawa na wameharibu ndoa zao iwe mwanamke/ mwanamme..

Kama swala lilikuwa kuenguliwa kwa jina lake ingebakia kuwa somo hilo na lawama zake zingewafuata wahusika ktk kikako cha chama kwani hakijaisha bado. Tofauti na Lwakatare ambaye aliahidiwa mengi wakati wa kikao Zitto kabahatika kuyaona yote dhidi yake wakati wa kikao, hakuwa na sababu ya kulalamikia pembeni ktk magazeti.

Tumeona ya Spika Sitta ktk kikao cha CCM lakini kwa busara zake mzee hakuweka vitisho, matusi na kuvaa gloves tayari kurusha ngumi..kwa sababu maslahi ya chama chake yako mbele ya tuhuma alozushiwa. na bahati Ukweli umetoka na Mafiosadi haswa wanajulikana walichojaribu kufanya. Ndani ya Chadema pia wapo mafisadi na Zitto hana sababu wala haja ya kujilinda kwa maneno wala kukurupuka kudai yeye sii Fisadi..Kauli na Vitendo vyake pekee ndivyo vinaweza kumsafisha na wala hakugombea Uengozi ili kufurahisha watu. Kuna problem ndani ya chama ni jukumu lake kurekebisha tabia hizo zikome na kama atashindikana ktk vikao vyote vya vyama basi hana sababu wala haja ya kuendelea kukaa chama hicho. Na bila shaka Wapiganaji wengi tungemfuata.. nashindwa kuanmini kwamba hata Dr. Slaa mpiganai mwingine amewekwa ktk kundi baya halafu mtetezi mkubwa wa Mh. Zitto ktk kikao cha chama ametokea kuwa ni mama yake!.. Hii kweli inaingia akilini mkuu wangu?.. Kuna Ujinga unaendela na sii Zitto mwenyewe ila wapambe wake ndio wanaharibu kabisa!
 
Last edited:
Zitto kishakula za mafisadi,anajiandaa kwenda CCM...hana lolote anatafuta kula tuu!


ZAIDI ZITTI ANAPIGANIA DHAMIRA YAKE ....NA WALA HAYUPO KWA MAFISADI....msibebe nadharia za kampeni....

nimegundua kuwa wengi wanajaribu kuwapa CHADEMA na ZITTO wao ushauri mzuri lakini wengi pia wanakoleza moto petrol....zote hizi ni siasa!!

tatizo kubwa nililoona hapa ni kuwa mambo ya kujadiliwa na viongozi wa chama husika yamepata njia kuja hapa ..tofauti na siri za ccm ambazo huja hapa kama fununu[inakuwa haina uzito]...

pamoja na kuwa nidhamu ndani ya ccm inashuka lazima tukubali kuwa ni chama pekee cheme uwezo wa kujiendesha kama taasisi hadi sasa...ndio maana hata wakimsimamisha bubu kwenye uchaguzi wanashinda kwa sababu daima ....wao wanategemea mtandao wa kichama kuliko wanasiasa au siasa za msimu!!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…