- yale yale aliyoyasema obama kule ghana, africans tuache tabia ya kuwekeza kwenye majina ya viongozi, tujifunze kuwekeza kwenye sound policies hii thread na yaliyojiri ni mfano mkubwa sana wa maneno ya obama.
- among all, chadema sikutegemea kukutwa na haya inasikitisha sana, sawa huenda mmekubaliana na kuyamaliza, lakini swali la the big picture linapaswa kua ni under who´s expense? Somebody must pay for makubaliano yenu ya kumfanya zitto arudishe fomu, now who is that? Kama sio sisi wananchi wa tanzania?
- i mean, hii ndio mnaita demokrasia makini? Mimi nilifkiri demokrasia makini huanzia kwenye box la kura, kumbe inaweza kupatikana na busara za wazee wa chama? Yaani na nyinyi chadema mnakubaliana na tabia za ccm za busara za spika? Nimeona a lot of spinning humu mnapoteza muda bure, sana sana sasa mnawapa ccm uhuru wa kuzidi kutuchezea wananchi wa taifa hili, kama na ninyi mnafanya kwa nini wao wasifanye?
- yaaani mnaogopa mbowe kusimama na zitto tu? Lakini hamuogopi mbowe kusimama na rais wa sasa wa ccm? This is incredible, zitto alipofukuzwa bungeni wengi tumelia kuwa ameonewa, sasa mnakuja na hizi nonsense ambazo ni clear kwamba kumbe hakuonewa kufukuzwa bunge kama ninawasoma vizuri humu na hizi spin zenu! Hamna hata aibu! Hivi mafisadi walimtuma zitto kuchukua fomu ya chadema, sasa waliomtuma kuwapigia kelele mafisadi kule bungeni mpaka kufukuzwa ni nani hasa? Hivi hili taifa tumemkosea nini mungu? Sasa nani wa kumuamini tena hapa kati yenu chadema na ccm?
- simtetei zitto wala mbowe, ninaitetea demokrasia ambayo hapa imepigwa chini kwa manufaa ya watu binafsi huko chadema na sio ya chama, no way demokrasia makini sio kumzuia mgombea mwenye akili ya kitoto na ambaye hajamkomaa kiakili, demokrasia ni absolutely opposite ya hii theory kwa sababu inataka apewe nafasi apigwe na kura za wananchi, lakini sio kumzuia kugombea, kuna ubovu mnajaribu kuuficha, sijui ni nini hasa mnachojaribu kukificha chama cha demokrasia makini? What is it?
- yaani kweli mnajaribu ku-pull a monkey on us wananchi na huku tunaona kwa macho yetu kwamba mnachosema sio ukweli ila ni zile zile siasa za ccm? Mnakuja hapa kumchafua zitto na filimbi nyingi za kuwalaumu ccm, badala ya kusimama na kubeba msalaba wenu? Yes i said it huko chadema kuna uozo kama wa ccm, ila mnajaribu kuuficha na busara za wazee lakini hamsemi nani atakayelipia kwa sababu anytime ukiuminya ukweli lazima kuwe na price to be payed, ni simple life maths.
- mnaleta spin za ajabu hapa kumchafua zitto, sasa kwanini msiruhusu akajimalize kwenye uchaguzi kama kweli ni mchafu kama mnavyodai? Aibuu sana hii watu tulikua tunawaamini na kuwategemea kumbe ni wale wale ccm tu, hivi mimi nimesema mara ngapi hapa kwamba the best idea ni ku'do away na viongozi wote na kufuta vyama vyote na kuanza na upya, nilisema hayo kwa sababu ya kutomuamini anybody, i mean kosa la zitto ni nini hasa kuchukua fomu ya mwenyekiti?
- chadema kwa hili mmetuangusha wengi sana na mnanuka kama mafisadi ndani ya ccm tu, haya mafisadi kumbe yapo kote kote sasa dawa ni kuyajua yalioko chadema maana ya ccm yanajulikana tayari, maana hii ni aibu ya the century hata mki'spin vipi you are rotten kama mafisadi ya ccm tu, dawa ni kutunga katiba mpya ya kufuta vyama vyote vya siasa tanzania na marufuku viongozi wote wa sasa kugombea uongozi tena tukianza na vyama vipya, i mean this is the worst ever!
yaani chadema chama cha demokrasia makini kinamzuia mwanachama wake kugombea uongozi kwa sababu ya kumuogopa kama ccm na mrema, na kuanza kumuita majina kibao, ya kumchafua halafu eti atarudi bungeni tena kwa tiketi ya chama hicho na kuwa na heshima ile ile kutoka kwa sisi wananchi, halafu na chadema nayo itaendelea kuwa na heshima ile ile kama zamani, yaani kweli na ninyi chadema kama ccm mnatufanya sisi wananchi wa tanzania ni kama watoto wadogo tusio na akili!
shame on all of you mnaohusika na hii nonsense ya busara kama za spika! Kule ccm zile busara za spika ziligahrimu shillingi millioni 100 hela zetu wananchi walipa kodi, sasa chadema tuambieni huko kwenu hizi busara zitatumika hela ngapi na za nani?
respect.
field marshall es!