Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
mbowe ni mlutheri sio mkatoliki.hujui unachoandika.

Hivi karibuni askofu wa same kaondolewa kwenye nafasi yake kwa kudhaniwa ni jasusi kwa amri ya vatican.

Na hayo uliyajua wakati ukifanya uchunguzi mboga wa namna ya kuibadili same iwe sameistan (samistan) au sio?
 
rangi nyekundu ni ya chadema hata mwanachama wenu mpya mchukia ufisadi alipojiunga na nyinyi anatumia rangi nyekundu kila maandishi yake.mtizame mchukia ufisadi ni taliban nae? Kwanini asitumie kijana rangi ya migomba ya bukoba?

ha ha ha mbavu zangu ......

haya mambo ya kutumia muda mwingi kwenye suicide bombing madrasa naona yamekumaliza kabisa.
 
Kweli kabisa, Baba mkwe yule aliyesaini Buzwagi au yule aliyesaini Dowans? Likumbushe jamvi vizuri.

NI YULE MZEE ALIYEHARIBU UCHUMI WETU .YEYE KASOMA HISTORY AKALAZIMISHA AWE GAVANA WA BOT.AKAMSHAURI NYERERE TWENDE KUPIGANA NA UGANDA NA UCHUMI UTAYUMBA KWA MIEZI 18 TU. MZEE YULE ALIVYOKOSA ELIMU YA UCHUMI. NCHI IKAINGIA KWENYE NJAA NA UCHUMI KUYUMBA KWA ZAIDI YA MIAKA 18.

MZEE HUYU HUYU AMESHUTUMIWA NA CUF KUSHIRIKI KUIUNGUZA BOT KUPOTEZA USHAHIDI WA WIZI WA WACHAGGA.TUNAPOZUNGUMZIA EPA ILIANZA KWA MZEE HUYU NA GENGE LAKE.AU UNAWEZA KUMWITA BABA MKWE.upo?
 

Na baadaye akanyakua shule na hospitali zote za waislam kabla ya kumlazimisha Nyerere kuanzisha Bakwata. Baada ya hapo akawashika waislam wote na kuwaweka ndani kwa miezi kumi nane.

Hivi unajua kuwa sababu ya kumpiga Iddi Amini ilikuwa tu kwa vile Iddi Amin alikuwa muislam .... na na na na .... subiri nimalize .... na na na .. hivi unajua kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya kiislam kabla ya Nyerere ah no ..... subiri ... kabla ya wakoloni!? upo?
 
ha ha ha mbavu zangu ......

haya mambo ya kutumia muda mwingi kwenye suicide bombing madrasa naona yamekumaliza kabisa.
usipoteze mjadala mada ni Zitto au mnahisi ni TALIBAN ndio mkanyima uenyekiti.
 
Msiifisadi kupindukia wizara ya kilimo.

Naona unaleta ukabila sasa umeona Masatu mtu wa Musoma na kilimo yuko Wassira tayari wamekuwa mafisadi.

tunajua mbinu zenu kuondoa mjadala.
kama afanyavyo Mwafrika.sis tuko makini tunarudi kwenye mada kuu uchaguzi wa Chadema na udikteta wa vikongwe vinne ambavyo vilishindwa kutunza penseni zao sasa vinaishi kwa mgongo wa Chadema.
 
Wazee wa CHADEMA walimwaga Ugali kwa kusema Zitto fisadi naye kaamua kumwaga Mboga. Sasa hali imekuwa mbaya, itawachukua muda mrefu sana kuinuka walipoanguka.
 
Waambie kwanza hao chadema wafuate utaratibu.Mkuu nimekuuliza kosa la zitto ni kutumia humu jina lake halisi.?

Mkuu, tatizo hapa ni kuwa, Zitto pia ni CHADEMA. Labda kama unataka kutuambia kuwa ameshaachana nao.

Kuhusiana na kosa la kutumia jina lake halisi, mimi nakiri kuwa hilo ndilo kosa kubwa kabisa alilolifanya. Angekuwa ametumia jina la bandia, habari, shutuma na kauli alizozitoa zisingekuwa na nguvu kama ambavyo zimekuwa na nguvu baada ya kutumia jina lake halisi.

Natamani kuamini kuwa alisahau kuwa aliingia JF na kuandika yote aliyoandika akidhani ametumia jina tofauti. Kwa kuwa madhara aliyosababishia chama chake kwa kauli hizi ni makubwa sana kuweza kuyarekebisha kwa kipindi kifupi. Yanarekebishika tu endapo CHADEMA itachukua uamuzi mgumu wa kumuomba awaachie chama chao na atafute chama kingine. Ila atakapotoka na kuingia chama hicho (kingine), jina lake litafifia kabisa kwenye duru za kisiasa nchini.
 
Naona unaleta ukabila sasa umeona Masatu mtu wa Musoma na kilimo yuko Wassira tayari wamekuwa mafisadi.


Nani kasema kuwa Masatu ni mtu wa Musoma? Musoma haina mafisadi kama Masatu, huyu atakuwa tu mtu wa kisiwani mafia.

tunajua mbinu zenu kuondoa mjadala.
kama afanyavyo Mwafrika.sis tuko makini tunarudi kwenye mada kuu uchaguzi wa Chadema na udikteta wa vikongwe vinne ambavyo vilishindwa kutunza penseni zao sasa vinaishi kwa mgongo wa Chadema.

Mmezijua mbinu hizo na nani? ha ha ha ... punguza muda huko madrasa za suicide bombings labda utapata cha maana cha kuandika
 

Zitto na Kikwete are buddies ... habari ndiyo hiyo
 

Mkuu wangu Masatu, nyaraka za siri za serikali ambazo zinahusu uhujumu uchumi au uhujumu mwingine wowote ni nyaraka zinazotakiwa kufichuliwa ili kufichua uozo unaofichwa kwa kichwa cha siri kwenye nyaraka hizo. Mkuu, Serikali ikifanya maamuzi ambayo si sahihi, inatakiwa irekebishwe ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea. Suala hilo na hili la kimkakati la CHADEMA ni masuala tofauti sana. Ni tofauti zaidi pale ambapo kiongozi anaetakiwa ku-demonstrate high degree of confidentiality anapokiuka na kuweka hadhara mambo ambayo hayana tija kwa chama chake, kwake mwenyewe wala kwa wanaoyasikia zaidi ya kusababisha madhara kwa chama, kwake na wale wanaomsikiliza.

Mkuu, imani ni kitu hatari sana. Imani iliyoporomoka kuhusiana na CHADEMA kwa kauli chache zilizotoka kwa kiongozi wake wa juu Kitaifa, zimenyong'onyesha wengi hapa na nje ya JF.

Kuhusiana na NAPE na SITTA, siwezi kufananisha hatua za CCM kwa viongozi hao na hii ya ZITTO kwa chama chake. Hata kidogo. Kwanza tuzungumzie NAPE. Alichofanya kijana yule ni kuelezea yaliyoshindikana katika vikao halali ambavyo yalikuwa na madhara kwa umoja mzima wa Vijana. Hakutoa siri za chama, wala uhaini ambao chama unakifanya (kama upo) kama alivyofanya Zitto. Alichosema ni kuwa mkataba wa upangishaji wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM ulikuwa na makosa, na kuyataja. Aliishia hapo. Hilo si tatizo kwa wanachama wala kwa chama, isipokuwa kwa waliofaidika na upangishaji huo. Limekwisha.

Spika alishutumiwa na CC na NEC kwa kutimiza wajibu wake Kikatiba. Chama kilikosea kufanya hivyo kwa kuwa kiongozi huyo alikuwa akifanya kazi zake kwa mujibu wa sheria zilizopo. Vile vile, Sitta hakuamua kuilipua CC wala NEC kwa hatua walizotaka kumchukulia. Aliweka bayana tu kuwa atafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na hataogopa lolote. Unajua Mkuu, ukiwa ndani ya kanuni na sheria hakuna tatizo wala sababu za kuhofia jambo. Tatizo ni unapokiuka sheria hizo tu, au kanuni zilizowekwa kisheria.
 
Ha ha ha ha .... wanaccm hamdanganyiki?

Mtadaganyika mara ngapi?

IPTL, Richmond, Buzwagi, Meremeta, Tangold, EPA, BOT, nk

Mlitudaganya kuhusu chacha,mjumbe wa mashariki (Mtikila)akaleta habari njema ,mkamsulubu kwa kumponda mawe.

Hakika damu ya Wangwe ya walilia kutoka udongoni,hakuna jiwe litalobaki juu ya jiwe jingine.
 
Mlitudaganya kuhusu chacha,mjumbe wa mashariki (Mtikila)akaleta habari njema ,mkamsulubu kwa kumponda mawe.

Hakika damu ya Wangwe ya walilia kutoka udongoni,hakuna jiwe litalobaki juu ya jiwe jingine.

Na hayo yamethibitishwa na kijana msomi wa IT toka Poraandi ambaye amewekeza pesa zaidi ya bilioni moja kule Kyela.
 

Mkuu, umesema vizuri sana. Ila naomba niongezee kidogo tu.

Ushauri wa kuamua jambo hauhitaji vikao. Unaweza kushauriwa na mtu yeyote (hata mimi wa mtaani) na isiwe kosa kama utaukubali ushauri huo. Naamini (labda kama nitaambiwa tofauti) kuwa wazee hao walipokuwa wakitoa ushauri huo, Zitto hakulazimika kuukubali. Atakuwa aliukubali kwa hiyana yake na kwa kushawishika kwake.

Sisi wote tuliunga mkono uamuzi wake kidemokrasia kugombea, kama ambavyo tuliunga mkono uamuzi wake wa kujitoa. Yote mawili yalifanyika kidemokrasia kabisa. Hivyo sidhani kuwa kulikuwa na makosa yoyote katika mchakato huo. Kungekuwa na makosa kama angelazimishwa na chama chake kupitia mkutano (mfano wa CC, Mkuu) na kumtaka atoe jina. Nadhani hapo wangekuwa wamemnyima haki yake. Hatujui ushawishi gani ulitumika kumfanya akubali kutoa jina lake kwenye nafasi ya Mwenyekiti.
 

Acha kuchochea ukabila na chuki zisizo na maana. Unadhani nani anaefaidika na uharamia wako hapa?
 
Kanda2,
Mkuu joke ziache mbali kabisa...Hapa mkuu umetoka nje ya mstari..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…