Kanda2,
Mkuu sijasema kuondolewa kwa Zitto ni haki.. jamani someni maandishi yangu. Nachosema mimi ni kwamba ipo sheria ktk kanuni za chaguzi kumuengua mgombea. Hoja yangu ni ktk kupinga msemo unatyaka kusema kuwa Demokrasia ni pale tu kila mtu (mwanachama) anaruhusiwa kugombea nafasi yeyote ya uongozi bila masharti fulani kuwepo..Ambavyo sii kweli!
Mkuu wangu nachoelewa mimi maswala haya yametokea siku za mwanzo za mikutano ya Chadema na naona kuna Kamati kuu kisha mkutano wa wazee! Hivi wewe unafikiria hao wazee ni wazee tu walezi chakari wa chama wanawahemea vijana!
Come on, Lolote lililotokea kwa Zitto tumeshasema yalikuwa makosa, katiba ya Chadema inaruhusu mgombea huyo kuchukua form.. Zitto hakuwa na mpango wa kugombea hadi alipofuatwa na wazee fulani na akajaza form akiwa Airport, kisha wazee wakamfuata na kumshauri imesha kuwa nongwa, soo, wamekipaka - hivyo itakuwa vizuri kama atachomoa... Naye akakubali Kuchomoa form yake..Hapa sioni tatizo liko wapi! na kama kuna tatizo tatizo ni Zitto mwenyewe.