Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Kimsingi Kabwe kajitoa kwa shinikizo kali la wazee vinginevyo walishapania kumtenga kitu ambacho kiingeisambaratisha CHADEMA. Kwa maana hiyo naona ni bora wangeondoa neno demokrasi kwenye chama hicho kwani hakuna demokrasia yoyote hapo. Kama ndo hivi wanatufundisha nini sisi wadanganyika?
 
Kitendo kinachoendelea chadema kinasikitisha sana wanademokrasia. Kwa waliYoyafanya viongozi na wazee wa Chama, inaonyesha hakuna umakini wowote zaidi ya uhuni, woga, ghiliba, uchu wa madaraka na kuabudu watu.

Haya ndiyo mambo tunayoyakataa na tunayoyapinga, woga na vitisho eti kwa sababu analindwa mwenyekiti asipingwe kwa sababu ya neno umoja wa chama, huo ni upuuzi na yeyeto aliye ukubali ni mpuuzi, na kama Zitto alitoa jina ili amwachie Mbowe free ride naye hajui analofanya kwani hio sio demokrasia, kwani hakuna demokrasia ya chumbani.

Chadema wasifanye unafiki wala wasiendeshe chama chumbani kwa mtu. Viongozi waje watueleze je hii ni taasisi ya watu wachache au chama cha siasa. Mfumo haujengwi bila ushindani, kwani Mbowe ni nani asiwe na upinzani, nani kasema duniani kuna mtu ambaye ni sahihi 100% .

Naomba viongozi wote wa chadema wanachama wa JF waje watueleze chama hiki kina katiba au la, na kama kuna katiba je ni nani anatakiwa kuifuata, na vile vile watueleze kwanini wanakataa mabadiliko na kutisha wanachama wasigombee nafasi ndani ya chama, na watueleze wazi ni wangapi tayari wametishwa au form zao kutupwa kwa sababu tu wanaonekana ni tishio kwa viongozi waliopo, vilevile waseme ni lini watakuwa tayari kuona mabadiliko bila kulindana, hii ni sera na utamaduni wa CCM. Waseme wazi nini kinaogopwa na kwanini alindwe mtu mmoja.

Demokrasia ya chumbani haiwezi kukuza chama, wengi tumejiunga na chama kuweza kuwa huru na kufanya uchaguzi wa huru na haki, uchaguzi wa ndio na hapana ni ukomonisti, ujinga, upumbavu, wizi, na uzezeta wa demokrasia.
Zitto kujitoa ni kuonyesha uzaifu na kutokomaa kisiasa. Siasa za kutoa majina ili kuwaenzi baadhi ya watu hazina nafasi kwenye demokrasia ya kweli.

Kwa hatua hii ya chadema bado mageuzi yana safari ndefu sana, naomba vyama hivi vya upinzani vifukuze wazee wote waliokulia ndani ya mfumo wa chama kimoja kwani hao ni matatizo tu, wamechoka, wamechakaa na hawana tena uwezo wa kufikiri. Ni afadhali kuanza upya kuliko huu uchafu wa kiini macho unaoendelea. Siasa za kupeana mgao wa ruzuku haziwezi kumsaidia mtanzania wala kumkomboa. Siasa za kulindana ili kupata posho hazina manufaa yoyote kwa mtanzania masikini, ni aheri mtafute kazi za kufanya kuliko kuwaibia wananchi kwa jina la mageuzi.

MNAUDHI, MNASIKITISHA, NA MNAKATISHA TAMAA. RUZUKU NI RUNGU LA DEMOKRASIA. KWANINI KUDANGANYA WANANCHI MNATAKA MABADILIKO WAKATI NINYI WENYEWE MNAOYAOGOPA. KALAGHABAO.
 
Naomba niseme kwamba mimi sio mwana Chadema. Si mwanchama wa chama chochote cha siasa. Ninachojali ni udhoofu wa sasa wa hali ya siasa na maendeleo ya Tanzania.

Nategemea CCM wangolewe na upinzani mwakani. Na kutokana na hali ilivyo, tegemeo langu ni kwamba Chadema itaongooza wapinzani ili waikomboe nchi toka kwenye mikono ya hao wanaozidi kuiangamiza.

Mbinu zozote za kuigawa Chadema zinanichukiza. Mbinu za kuwagawa Watanzania waliojiunga na JF ili kushirikiana kuleta mabadiliko, zinaniudhi. Kwa maoni yangu, ni CCM ndiyo inaweza kuwa na mipango ya kuwagawa Watanzania, hasa hawa walioko hapa JF.

Support inayopata Chadema hapa sio kitu kidogo. Kama kukiweko na habari za kupotosha hapa na kuwahimiza wana JF kwamba Chadema imekuwa chama cha kidikteta, na wana JF wengi wakahadaika kirahisi, basi sina budi kusikitika sana.

I do not have the latest news, as I live half a world away from Dar. But from what I have read on JF, there was no ban on Zitto’s wish to be the Chairman of Chadema. Why was the fact that he was advised to withdraw presented as dictatorship? Why was there a rush to persuade people that Chadema is bad? Why should I not suspect that there are evil intentions?

I call on all of us to set this matter aside and revert to our initial focus on how to bring change to our motherland.
ni wapi uliwahi kuona uncontested post kwenye siasa hasa za vyeo vya juu, kama SIO NCHI za kisocialist. Mimi niu mwana Chadema hai na hii hali siiafiki wala siipendi hili ni kaburi,tusiwasingizie wapinzani wetu kwa uoza wetu na ujinga wetu. Kwa nini ashauriwe kutoa form, je ni kweli Chadema ni Zitto peke yake aliyechukua hiyo form? come on now. we have to clean our own first.
 
Mwanzoni nilikuwa nafikiri tuache Demokrasia ichukue mkondo wake lakini baada nikashtuka Zitto laiti angepita basi CHADEMA ingeshuka umaarufu kama NCCR.
 
Kina elekea wanachama wake wengi ni wa familia fulani...........yaani chama cha wanafamilia
 
Chama cha wanafamilia cha mashemeji, wakwe ndugu wa kiume na wakike......habari ndo hiyo na kwa staili hii ccm itaendelea kuwabamiza hakika!!!!!!
 
Mwaka huu mtaongea mengi sana waacheni wana CHADEMA kama mnavyo waacha wana CCM. CHADEMA haitaki mamluki ili wakibomoe chama kwa mgongo eti wa domokrasia wapi na wapi jama tumeshtukia janja ya nyani.
 
No is too early to make such comments, let us wait, baada ya muda tutajua kama ni right or not. Let us not be controlled by our emotions and ambitions!
 
Chama cha wanafamilia cha mashemeji, wakwe ndugu wa kiume na wakike......habari ndo hiyo na kwa staili hii ccm itaendelea kuwabamiza hakika!!!!!!
Nyie nanyi mmetuchosha kwa hoja zenu dhaifu, mmevaa miwani yenye vioo vya mbao kiasi kwamba ukweli hamuuoni? Safu ya uongozi Chadema ni familia ya nani? Njooni na hoja za msingi.
 
haiwezekani wajumbe na viongozi wote wawe kabila moja.

mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dsm ni John Guninita sio mzaramo au mtu wa Dsm.anatoka Musoma.
Mwenyekiti wa Uwt mkoa wa Dsm ni Z.madabida ni mtu wa Rufiji.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Dsm ni Said kijana wa Tabora.

Mbona Hujamtaja Mweneyekiti wa Chadema mkoa wa Dar Es Salaam?

Vile vile siyo Mbaya ungetutajia Wajumbe wa CCM au Chadema na Viongozi wao wa Mkoa wa Mara
 
No is too early to make such comments, let us wait, baada ya muda tutajua kama ni right or not. Let us not be controlled by our emotions and ambitions!
Naungana Kabisa na wewe maana huwezi kufanya CHADEMa itumbukie kwenye mgogoro kama vyama vingine siku za yuma, Lazima tuwe makini sana na watu kama hawa.. Maana huwa napata shida sana kusikia mambo haya. Mimi naungana na watu wote walifikia uamuzi wa kujitoa kwa Zitto ili CHADEMA iwe imara
 
hivi, hii ina tofauti gani na ile ya ccm ya Rais kugombea bila kupingwa ili kumalizia awamu yake ya pili ya Uongozi wake wa nchi. lipi baya zaidi la ccm au chadema, ama yote sawa ama hayafanani hata kidogo?
 
Hatuongelei uongozi pekee asilimia kubwa hasa hao wazee wa chama hicho ni familia moja wakina mtei na wenzake
 
Salamu kwenu wana JF. Natumaini nyote mu beheri waa afya, na leo tunaanza tena wiki ya mikiki mikiki kusaka riziki.

Ninatambua uchangiaji wa wana JF kuhusu ChaDEMA Taifa na Kilimanjaro.

Wasiwasi wangu hapa ni kuwa wachangiaji wengi ni wana CCM and so, wanajaribu kujifanya wachambuzi na viongozi wa kudhani lipi lafaa na bora kuliko lingine. Lakini wangepewa nafasi, holaaaaa!

1. Kwa taarifa yenu, Zitto alichukua form ili kuonyesha kuwa kuna makundi chadema lakini sivyo,.......it was a strategy kuwafungisha midomo wasioipenda chadema. Makubaliano yalikuwa CHUKUA FORM afu UJITOE. This is politics.

2. Uongozi wa Chadema kilimanjaro mbona unawaumizeni vichwa sana...wakati watu waligombea na kupewa kura....nyie mlitaka mwana mbilimbi aende na kupewa chama? Hivi political thinking za wengine zikoje? Ungepewa uongozi wewe na babayako ao another family member, ungekataa,,provided uliomba? Najua hamuwapendi wachaga, lakini ukweli haufichiki kuwa they are eligible and capable!

3. Chadema ni chama cha Demokrasia ya maendeleo, na Zitto amedhihirisha hilo,,,,,"najitoa chama kisigawanyike" hakuwa presurised. Kwa taarifa zenu, nilikuwa kwenye kikao cha wazee na najua kilichojiri. Mliotaka Ya lipumba na Safari yajiri chadema, poleni.
[/QUOTE]

Chadema hakiwezi kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo.Labda mwenzetu akili yako haina akili.Lazima mkubali mumefulia,kwa mtindo huututaongozwa na ccm muda wote.
 
"Naomba viongozi wote wa chadema wanachama wa JF waje watueleze chama hiki kina katiba au la, na kama kuna katiba je ni nani anatakiwa kuifuata, na vile vile watueleze kwanini wanakataa mabadiliko na kutisha wanachama wasigombee nafasi ndani ya chama, na watueleze wazi ni wangapi tayari wametishwa au form zao kutupwa kwa sababu tu wanaonekana ni tishio kwa viongozi waliopo, vilevile waseme ni lini watakuwa tayari kuona mabadiliko bila kulindana, hii ni sera na utamaduni wa CCM. Waseme wazi nini kinaogopwa na kwanini alindwe mtu mmoja."

Kinepi,
Jibu lako kuhusu demokrasia ndani ya CHADEMA liko wazi kama ukisoma hapo chini kutoka kwenye tangazo la mkutano wa CHADEMA ambalo limetolewa na Katibu Mkuu Dr Slaa:


"Hivyo basi tunapenda kuwafahamisha Wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa hii ndio ratiba yetu rasmi ya kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa Chama na pia ni hatua muhimu sana katika Mapambano yetu dhidi ya Mafisadi na Ufisadi na kuhamasisha uwajibikaji na kutetea rasilimali za Taifa.

Ni muhimu ikazingatiwa kuwa ndani ya CHADEMA kila Mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yeyote ile kwa mujibu wa Katiba ya Chama,hivyo basi kila Mwanachama atumie haki yake ya kidemokrasia kuchukua fomu .
"

Ahsante sana kwa ushirikiano wenu.

………………
Dr. Willibrod P. Slaa (Mb)
Katibu Mkuu.
19/08/2009.
-----------------

Swali ambalo unatakiwa ulifanyiage homework ni kuwa unaamini maneno hayo kama ndio truth, the whole truth, nothing but the truth au machale yamekucheza kama mimi? Kazi kwako!
 
kujitoa kwa zitto kwa ushauri wa wazee wa chama ni pigo kwa demokrasia...shaka yangu ni kuwa hii inaweza kuiathiri chadema in the long term kwani zile tuhuma kuwa unahitaji kutoka kaskazini mwa Tanzania ili uwe kiongozi wa juu zitapata nguvu kwa staili hii ya demokrasia.
 
kujitoa kwa zitto kwa ushauri wa wazee wa chama ni pigo kwa demokrasia...shaka yangu ni kuwa hii inaweza kuiathiri chadema in the long term kwani zile tuhuma kuwa unahitaji kutoka kaskazini mwa Tanzania ili uwe kiongozi wa juu zitapata nguvu kwa staili hii ya demokrasia.

Asante mkuu yaaani hii imejidhihirisha wazi kabisa......aibuuuuuuuu!!!
 
tatizo hapa si Zitto kuchukua form na kugombea, la hasha au Zitto ni nani hata kidogo. Tatizo ni kwanini wanatumia njia za dikteta kuengua wagombea, na kama mtu ni mamluki au pandikizi hizi si njia sahihi za kuenguana, kwani nani anauhakika 100% nani pandkizi. Kinachotisha ni jinsi demokrasia wanayoitetea na vile wanavyoifanya.

Hizi ni kauli za kuchoka akili eti tunadumisha mshikamano kwa hiyo akifa kiongozi wengine wote hawafai kwani wao watakivuruga chama. basi Chadema hawana haja ya kugawa kadi za chama na wabadilishe katiba kwamba uongozi si kwa wanachama wote.

Kama wagombea wote ni viongozi wa ngazi za juu, halafu wanasema watakigawa chama ina maana chama chenyewe na viongozi wake hawajui nini wanakifanya. Kwanini waendeshe chama kwa divide and rule. Mimi sihitajii demokrasia ya namna hii. Kuogopana kwa sababu za kijinga ni upuuzi. Chama kikiwa na sera madhubuti na kikifuata katiba yake ni rahisi kudhibiti upumbavu hata ukifanywa na Mwenyekiti. Ndio maana nchi zenye demokrasia ya kweli haziogopi kiongozi kwani kiongozi hayupo juu ya katiba anaweza kutolewa muda wowote. Ila kwa uongozi huu wa kupanga mafiga yetu macho. kazi kubwa tunayo mbele.
 
Ndugu Kanda2, for me Utaifa ni zaidi ya Ukabila, I don't care ni nani anayefight kwa ajili ya Mama zako/zangu wanaojifungua kwa tabu, i don't give a shit as to who ana fight against Ufisadi awe Mzaramo, awe Mchagga, awe Msukuma I don't give a damn.
 
Una maana mambo ya ngoswe aachiwe ngoswe?

Yep..kama yeye sio CHADEMA atakuwa hana input. Maana huenda hata haujui mchakato wao wa uchaguzi..sasa post kama hizi zinaweza hata kufikia page ya 50 lakini ukichunguza hamna input..Hii ndio hatari niliyoiona.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom